Wallace Karia hapaswi kurejea katika nafasi yake baada ya kuonyesha failure na upendeleo wa wazi katika sakata la derby

Wallace Karia hapaswi kurejea katika nafasi yake baada ya kuonyesha failure na upendeleo wa wazi katika sakata la derby

MwananchiOG

JF-Expert Member
Joined
Apr 4, 2023
Posts
2,507
Reaction score
4,943
Ukisema maendeleo kidogo yaliyopatikana katika soka la Tanzania limechangiwa na Wallace karia, ninapinga.Maendeleo ya soka nchini kwa kiasi kikubwa yamechangiwa na wadau wa michezo wakiwemo wafadhili, ambao kwa namna moja ama nyingine nina uhakika wallace karia hajachangia au kama amechangia ni kwa 1%.

Wallace karia ni aina ya kiongozi asiyemsikivu, mwenye jeuri, kiburi na majigambo.

Mfano mdogo, katika sakata la derby, alipokuwa akihojiwa na waandishi wa habari kuhusu hatma ya mchezo wa derby alijibu "watu waache utoto" , Hili si jibu linalopaswa kutolewa na kiongozi wa ngazi ya juu kama TFF.

Nina uhakika 100% kama si serikali kuingilia TFF na kusaidia katika kufanya maamuzi, mpaka leo jambo hilo asingeweza kutatua.

Tatu, huyu ni aina ya kiongozi mwenye kiburi. Baada ya uvunjifu mkubwa wa kanuni uliofanywa na bodi ya Ligi, watendaji wakuu akiwemo CEO Almas kasongo, Mwenyekiti wa bodi, Steven Mguto walijiuzulu (ambapo pia inasemekana walitaka kujiuzulu mapema ila Karia aliwakingia kifua huku akijua wazi walivunja kanuni, mpaka serikali ilipolazimisha ndipo akakubali, huku yeye akiendeleza kiburi kwa kung'ang'ania kiti huku akijua amefanya makosa na ameshindwa kusimamia uwajibikaji).

kwa kifupi, KARIA MUST GO!
 
Na kwa nini agombee kwa awamu ya 3, na wakati watangulizi wake wote waliheshimu utaratibu wa kuongoza awamu mbili pekee! Au anataka kusema yeye ni bora sana kuliko Leodgar Tenga, rais wa kwanza wa TFF iliyotokana na ile FAT ya Ndolanga?
 
Anasaidia kupunguza kura za CCM kwa wingi kwenye uchaguzi wa mwaka huu 2025

 
Karia kuwekwa na serikali hapo TFF hakuna wa kumtoa.
 
Na kwa nini agombee kwa awamu ya 3, na wakati watangulizi wake wote waliheshimu utaratibu wa kuongoza awamu mbili pekee! Au anataka kusema yeye ni bora sana kuliko Leodgar Tenga, rais wa kwanza wa TFF iliyotokana na ile FAT ya Ndolanga?
Una Katiba ya TFF inayoongelea Vipindi vya Urais? Kama unayo ebu tuwekee tuone ilianza mwaka gani.
 
Kalia ndio ameshindwa kutofautisha ushabiki wake kwa Simba uongozi wa TFF,, mgogoro wa derby ulikuwa so wakufika kwa Rais wa nchi....he proved extremely failure as leader!

Kaua program nzuri ya kukuza vipaji vya vijana ya Malinzi, huku ajifunika shuka la mafanikio ya Simba na Yanga ,infact hamna mwendelezo mzur wa kukuza vipaji hatuoni akina Dickson job , kibabage ,duchu wengine wakizalishwa.......

Kweli Kuna mafanikio kiasi kwa senior timu za Taifa stars, mfano ushiriki wao kwenye afcon ,chan ...lakini katika mafanikio hayo huuwezi kuzitoa Simba, Yanga na Azam namna zilivowekeza na kupata squad nzur ya timu ya Taifa

Aisee....Kalia vipindi viwili vimemtosha, hiki cha tatu anaongeza kasahau nini......??? He must go now....
 
Back
Top Bottom