Ukisema maendeleo kidogo yaliyopatikana katika soka la Tanzania limechangiwa na Wallace karia, ninapinga.Maendeleo ya soka nchini kwa kiasi kikubwa yamechangiwa na wadau wa michezo wakiwemo wafadhili, ambao kwa namna moja ama nyingine nina uhakika wallace karia hajachangia au kama amechangia ni kwa 1%.
Wallace karia ni aina ya kiongozi asiyemsikivu, mwenye jeuri, kiburi na majigambo.
Mfano mdogo, katika sakata la derby, alipokuwa akihojiwa na waandishi wa habari kuhusu hatma ya mchezo wa derby alijibu "watu waache utoto" , Hili si jibu linalopaswa kutolewa na kiongozi wa ngazi ya juu kama TFF.
Nina uhakika 100% kama si serikali kuingilia TFF na kusaidia katika kufanya maamuzi, mpaka leo jambo hilo asingeweza kutatua.
Tatu, huyu ni aina ya kiongozi mwenye kiburi. Baada ya uvunjifu mkubwa wa kanuni uliofanywa na bodi ya Ligi, watendaji wakuu akiwemo CEO Almas kasongo, Mwenyekiti wa bodi, Steven Mguto walijiuzulu (ambapo pia inasemekana walitaka kujiuzulu mapema ila Karia aliwakingia kifua huku akijua wazi walivunja kanuni, mpaka serikali ilipolazimisha ndipo akakubali, huku yeye akiendeleza kiburi kwa kung'ang'ania kiti huku akijua amefanya makosa na ameshindwa kusimamia uwajibikaji).
kwa kifupi, KARIA MUST GO!