Wallace Karia: Kuna ma-Tundu Lissu wa kwenye mpira

IKIRIRI

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2018
Posts
2,734
Reaction score
3,023
Ni kauli ya Rais wa TFF Leo Arusha akitoa hotobu mbele ya mkutano mkuu,kauli yake nadhani anamlenga Michael R wambura kwamba ni mkorofi analengo la kuharibu mpira.

Nimeshangaa kwann kamuhusisha mh Tundulisu? Mkutano wake naamini unawanachana wa itikadi tofauti ,naamini amewakera wale wa chadema.

Kwa tafsiri yangu Wallace karia amemkosea sana Mh tundu lisu..maana yake Mh lisu ni mkorofi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo jamaa ana madudu mengi ya ubadhilifu na amejitengenezea system ya kifalme pale TFF, no justice kwenye ile taasisi, anamshambulia Tundu lissu ili apate excuses kwa mkuu kwa anayoyafanya pale...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwenye mkutano mkuu wa TFF huko Arusha, Rais wa TFF kachafua hali ya hewa.

Kafananisha ubadhirifu ndani ya TFF na Utundu Lissu.

Sijui kala maharage ya wapi huyu Msomali. Alikuwa anaongea kama proper Somali Warlord.

Eti wataoleta Utundu Lissu ndani ya TFF atawashughulikia. Anataka kuiweka TFF ndani ya CCM badala ya kuwa neutral kwenye siasa. Ipo siku itamgharimu pakubwa. Atajikuta Mogadishu. Akumbuke ya yule Mkenya.
======

Katika mkutano mkuu wa mwaka wa Shirikisho la soka nchini (TFF), Rais Wallace Karia amewaonya wale wote wanaojifanya ni kina Lissu wa mpira na kuweka wazi kuwa hatacheka nao.

Karia ameeleza kwa manufaa ya mpira wa Tanzania ni lazima viongozi wawe na nidhamu na kuheshimu kanuni na miongozo ya mpira duniani vinginevyo ataendelea kuwafungia.

“Siwezi kuwachekea wanaojifanya akina Lissu kwenye mpira wetu, nitaendelea kuwafungia ili mpira wetu uwe salama'', amesema Karia katika hotuba yake.

Mbali na hilo Karia ameeleza mipango mbalimbali ya shirikisho hilo katika kuinua mchezo wa soka ikiwemo kuanzisha ligi mbalimbali za vijana.

Uongozi wa Karia ulichanguliwa mwaka 2017 katika uchaguzi mkuu uliofanyika jijini Dodoma ambapo Karia alichaguliwa kuwa Rais huku makamu akiwa ni Michael Wambura lakini ameshafungiwa maisha kujihusisha na soka.
 
Habari Kwahisani ya: eatv news

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hahahahah!!anatafuta chaka la kujifichia kwani anajua akitaja jina hilo ,kuna huruma lazima itamshukia hahahaha!!maji yamezidi unga
 
Hoja ya Wambura ippo verry strong Karia hakuwapa FIFA hukumu ya mahakama.

Wambura atarejeshwa TFF labda mahakama ikiingiliwa na siasa
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rais wa TFF Karia,ni vizuri ukafahamu kuwa sehemu pekee ambayo inawaweka pamoja watu wa dini,itikadi za kisiasa,makabila,jinsi,umri,vipato,rangi n.k ni soka.

Unapokuwa kiongozi ni vizuri kulifahamu hilo na siku zote kiongozi bora huakikisha anawaweka pamoja watu anaowaongoza bila kujali tofauti zao.

Karia ni vizuri sana haya mambo ya kwenye Siasa ukajiepusha nayo na kuhakikisha hayaingii kwenye soka.

Si huwa unaona pale Taifa kwenye soka,Januari Makamba na Zitto Kabwe wanakaa pamoja na kujadili mikakati ya namna Simba inavyoweza kushinda.

Huko ndipo Mwigulu Nchemba na Freeman Mbowe wanajifungua Chemba na kupanga mikakati ya ushindi bila kujali tofauti zao za kisiasa.

Karia usiingie siasa kwenye soka,utaipasua TFF na utashindwa mapema. Na Dotto Bulendu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anacha kuongelea mpira analeta siasa.
Anadai TFF ya kabla yake ilikuwa na ubadhirifu mwingi. Msomali kasahau alikuwa Makamu was Rais chini ya Malinzi.
Na Anasahau kwa Katiba ya TFF.Makamu Mwenyekiti ndo Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha ya TFF.Karia aache Usanii.Ndo Maana anapambana na Wambura maana Ndo Mwenyekiti Kamati ya Fedha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wako Arusha Naura Spring Eti Kubadili Katiba Ili Walete Maendeleo Ya Mpira Wa Kisayansi.
.......
Mpira wa kisayansi hauletwi kupitia Katiba, ni lugha ya kuwachanganya wajumbe kwa wasilahi ya watawala.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inavyoneekana wapinzani wa Lissu kisiasa wamemshindwa kwa hoja,ndiyo mana wanawatumia wajinga wasiyojitambua kumchafua Lissu, pasipo kuelewa ndo wanajizika wenyewe, karia umejivunjia heshima na watu wamekudharau sana kwa kauli yako
 
Aachane na soka akajiunge kwenye siasa kama anaipenda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…