Wallace Karia: Kuna ma-Tundu Lissu wa kwenye mpira

Kuna mzee mwenzangu kanitumia ile clip ya Wallace,nadhani ni makosa ya kiufundi katika Public Speaking,Wallace hana ujuzi wa kuongea kwenye hadhira ya watu.Anadhani kukonga nyoyo za watu ni kuongea kwa ukali na kuhamaki.

Inawezekana kalitumia hilo neno la "Matundu Lissu wa kwenye Soka" akidhani ni kauli rahisi na nyepesi.Hili ni doa,FIFA na mashirikisho mengine ya michezo duniani hawakuwa wajinga kukataza alama,ishara,nembo na kauli za kisiasa kuingizwa katika soka,wanajua hisia ya siasa inavyoweza kuwasambaratisha watu hata walio timu moja katika soka.

Kwa imani ya mpira wa Tz,kwa heshima ya familia ya soka Tz,ninadhani...na si tu kudhani,bali ninaona Wallace anaweza kuomba radhi kwa kauli iliyopokelewa tofauti.

Kuliingiza jina la Lissu katika hotuba ya kuwakemea kina Wambura,ni kuonyesha kuwa Lissu ni kama Wambura.
 
Hawa watu kila siku jina Lissu likitajwa huwa wanaweweseka!! Kama mlishindwa kumuua kwa kuwa Mungu hakutaka, hata huko msikotaka U-Lissu usiwepo utakuwepo tu!!
 
Kila mwaka kwa kadri tunavyokuwa tunaukaribia uchaguzi, CCM huwa na uwezo mkubwa sana wa kuwajaza ujinga baadhi ya watanzania wenzetu, ukichanganya na masuala ya uraia unaelewa ni kwa nini kasema hivyo!!
Tunaelewa issue yake ya uraia ipo Uhamiaji. Janja yake kujipendekeza itakuja kugharimu sana siku za baadaye.
 
huyo jamaa ana madudu mengi ya ubadhilifu na amejitengenezea system ya kifalme pale TFF, no justice kwenye ile taasisi, anamshambulia Tundu lissu ili apate excuses kwa mkuu kwa anayoyafanya pale...

Sent using Jamii Forums mobile app

Kwa Tanzania kauli kama hizi za kulalamika siyo ajabu kabisa....Malinzi likuwa mbaya, sasa ni Karia, huko nyumba Tenga naye baadhi walimuona ni 'mfalme'..mradi tu watanzania hatuna jema kabisa...ni kulalamika tu mtindo mmoja...
 
Nimemsikiliza huyo msomali Hakuna uhusiano kabisa aseme kama wanataka apewe uraia,hio clip imetumwa Kwa bosi wake FIFA ijulikane kama ni kauli yake au ya chama anachokiongoza,yajulikana yeye ni kada asichanganye ukada na kazi
 
Yani mnalilia demokrasia ilhali mnakataza watu wasiseme views zao, mnavyoambiwa lisu anabomoa zaidi ya kujenga, mnabisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani ifike sehemu Mungu siku moja

Afanye Muujiza CCM isambaratike nakuanguka

TL awe pale magogoni, najiuliza

1. Musiba
2. Makonda
3. Kalia

Watajisikiaje? Watafanyaje? Wataficha wapi nyuso zao?

Kwa huyu wa kwenye Soccer namuona akipunguza kura zake na sidhani atarudi tena
 
Kumtajataja Lissu Hata Mahala Si Sahihi Huko Ni Kujikombakomba Aonekane Ni Kada Mtiifu Wa Upande Ule. Ni Aibu Sana
 
NATANGAZA RASMI KUCHUNGUZA URAIA WA KARIA KUANZIA SASA , MAJIBU NITAYAWEKA HAPA JF NA KUIKABIDHI MAHAKAMA YA UMMA
 
Tatizo wewe unataka post za kukufurahisha tu ambazo hazigusi upande unaoushabikia, hivyo utapata tabu sana
Nashani hukumuelewa,umeweka uzi bila kufafanua tuhuma za karia dhidi ya lissu ni zipi.Ni kama habari isiyo na kichwa cha habari.
 
Karia hawezi kabisa kukuza mpira Tanzania.. Sijui alipataje hii nafasi
 
Tanzania ile research ya 3 katika 4 niwehu

Tuikubali kabisa kwamba katika 4 ni MTU 1 mwenye akili Timamu

Ikiwa viongozi wengi tunaowachaguwa wehu/vichaa.... Wanahabari wehu/vichaa

Taifa letu haliko salama.
 
Kwa hiyo anayoyasema Lisu ni ukorofi.
Akamshambulie huyo lisu wake kwa kutumia wasiojulikana wa soka.
Mi ningepata tusi moja tu ningemtukana.
Huyu kiongozi hopeless.
 
WANATUMIKA VIBAYA! Anadhani akisema hivyo ndio ile tuhuma ya kunyang'anywa uraia na kisha kurudishiwa itafutika nafsini MWAKE.
KINA KARIA WAKO WENGI.... TANZANIA TUNAYOIJUA INAENDELEA KUANGAMIA KWA WATU WAKE KUKOSA MAARIFA
 
Nimemsikiliza huyo msomali Hakuna uhusiano kabisa aseme kama wanataka apewe uraia,hio clip imetumwa Kwa bosi wake FIFA ijulikane kama ni kauli yake au ya chama anachokiongoza,yajulikana yeye ni kada asichanganye ukada na kazi
KAULI ISIYOPENDWA:
NI VEMA KARIA AKAJIUZULU SOKA NA KUINGIA KWENYE SIASA, LA SI HIVYO MICHEZO INAYOSIMAMIWA NA TFF HERI IKASUSIWA ILI IJULIKANE SOKA NI MCHEZO AU SIASA.
 
Ameniudhi sana. Anafurahia yaliyomkuta Lisu na huenda anapenda huyo wambura yamkute ya Lisu
 
Huyo karia ndo amemfanya mwenzake malinzi anasota rumande hadi leo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…