barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,880
Kuna mzee mwenzangu kanitumia ile clip ya Wallace,nadhani ni makosa ya kiufundi katika Public Speaking,Wallace hana ujuzi wa kuongea kwenye hadhira ya watu.Anadhani kukonga nyoyo za watu ni kuongea kwa ukali na kuhamaki.
Inawezekana kalitumia hilo neno la "Matundu Lissu wa kwenye Soka" akidhani ni kauli rahisi na nyepesi.Hili ni doa,FIFA na mashirikisho mengine ya michezo duniani hawakuwa wajinga kukataza alama,ishara,nembo na kauli za kisiasa kuingizwa katika soka,wanajua hisia ya siasa inavyoweza kuwasambaratisha watu hata walio timu moja katika soka.
Kwa imani ya mpira wa Tz,kwa heshima ya familia ya soka Tz,ninadhani...na si tu kudhani,bali ninaona Wallace anaweza kuomba radhi kwa kauli iliyopokelewa tofauti.
Kuliingiza jina la Lissu katika hotuba ya kuwakemea kina Wambura,ni kuonyesha kuwa Lissu ni kama Wambura.