Wallace Karia: Kuna ma-Tundu Lissu wa kwenye mpira

Kaongea tena kutoa ufafanuzi. Mi nadhani ndiyo sasa kaharibu kabisa. Zero brain kabisa. Huyo Msomali tafadhali angalieni video clip. Hata kiswahili ni majanga
 
Namshauri tundulissu amburuze FIFA bila huruma ili wawe na adabu washenzi hawa
 
Kwanza tff ni washenzi wamewahi kunikataa nikiwa nje natumia vocha kuwapigia waniwekee sawa mambo eti nirudi kwanza yaaani wapuuzi kabisa

Lakin Mungu mwema balozi alinisaidia shida yangu hawasikilizi wao wanahukumu tu..bila kujiridhisha ovyo kabisa #kiria out
 
Kuandika post kama hizi tu haiyoshi, ifike wakati tuchore mstari. Huyu mtu hakukosea ni dhamira yake ndiyo maana kwenye kauli yake ya kuomba msamaha kasema alichomaanisha Lisu anahangaika na kuikashifu serikali, na Wambura anafanya hivyo hivyo kwa serikali.
 
Yaani bora Lisu ,Karia ana deal na Wambura ambaye ana roho ya paka zaidi ya Lisu na Wambura ana sababu na hoza za msingi ambazo hazijajibiwa.Huyu mpuuzi ili anyooke inatakia wapatikane akina Wambura wengine kama watano watunyooshee TFF.Alafu ile barua ya kufungiwa Wambura na FIFA naona kama kuna mchezo umefanyika,sababu juzi tu hapa FIFA wamewaambia TFF waeleze sababu ya kumfungia Wambura.
 
Huyo msomali koko Leo amethibitisha ni jinsi gani hajui lengo na umuhimu wa kuendeleza taasisi anayo iongoza ... !!!

Amesahau kuwa lengo la kuendeleza taasisi hiyo ni kuwaweka watu pamoja bila kujali matabaka yao, itakadi zao, imani zao na hisia zao mbalimbali katika jamii kwa ngazi ya mtaa, Kijiji, wilaya, taifa na hata dunia kwa ujumla na ikibidi ulimwengu mzima ...

Pumbavu kabisa ...


Sent using Jamii Forums mobile app
 
karia amesoma dot na kungundua ili mzee baba ajue naye yupo na asikumbuke zile milioni hamsaa alizosema watazitotea tutndu lolote zitapoliwa kizembe,ni kuibuka na kashifa za mwamba lissu.

nadhani jiwe hataulizia tena zile milioni hamsaa,maana karia, kasha mshambulia lissu kwamba ni mchochezi.

ili utoboe zama hizi ni kutafuta kiki kwa gharama yoyotee,hasa kuuzodoa upinzani
 
*CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA). TAARIFA KWA UMMA- KUHUSU KAULI YA KUFEDHEHESHA ILIYOTOLEWA NA RAIS WA TFF*
Tumepokea kauli yenye ukakasi mkubwa iliyotolewa na Rais wa Chama cha Mpira wa miguu Tanzania (TFF) Ndugu Karia kuwa atawashughulikia wale wote ambao wataleta " U-Tundu Lissu" kwenye mpira.

Kauli hii inapaswa kutazamwa kwa umakini mkubwa Kwani imebeba ujumbe mahususi kuwa watu aina ya Tundu Lissu wanastahili kushughulikiwa kwenye sekta zote.

Kwetu sisi kama Chama ni Kuwa watu aina ya 'Tundu Lissu' na wenye 'U-Tundu Lissu' ni wale wote ambao wenye mtazamo na uwezo wa kuhoji, wanaotaka utawala wa sheria ufuatwe na wanaotaka sheria na Katiba ziheshimiwe na kuhakikisha kwamba kila mmoja anakuwa sawa mbele ya sheria na zaidi kila mwenye maoni na mawazo tofauti asikilizwe.

Sasa kauli ya Karia inatufanya tujiulize maswali mengi kama vile , inawezekana anawajua waliomshughulikia Tundu Lissu na ndio maana anataka kuwatumia kushughulikia 'Tundu Lissu' walioko kwenye mpira n.k.

Kutokana na kauli hii tunatafakari kuchukua hatua zifuatazo kama hataomba radhi;

1.Kusimamisha mahusiano na ushirikiano wowote na TFF ikiwemo kuwataka Wanachama wetu kutokushiriki matukio yote yanayoandaliwa na TFF.

2. Kususia bidhaa zote zenye nembo na au zinazotolewa na TFF zikiwemo jezi za timu za Taifa na nyinginezo.

3. Kuchukua hatua dhidi ya Makampuni ambayo yataendelea kushirikiana na TFF ikiwemo Kususia bidhaa zao, kwani watakuwa wanaunga mkono taasisi inayoongozwa kwa ubaguzi wa kisiasa.

4. Kuwashawishi wadau wa mpira kokote kusitisha mahusiano na TFF Kwani inaendeshwa kisiasa na kibaguzi.

Tunamtaka Ndugu Karia aombe radhi hadharani na aeleze UMMA kauli yake ilimaanisha nini na kama anaona ni haki kwa Lissu kupigwa risasi na ndio njia sahihi ya kushughulikia changamoto za kwenye Mpira.

*John Mrema*
*Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje -CHADEMA*

02 Februari, 2019

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanini umembagua kwa kumuita Msomali
Kwani siyo Msomali, kumuita mtu Mmakonde au Mnyamwezi au Msambaa au Mpare ni kumbagua? Hapo inaongelewa origin au ethnicity, Karia ni Msomali na atabaki kuwa Msomali(ethnic Somali) mpaka kufa kwake. Unaweza kubadili dini au nationality lakini hauwezi kubadili origin, kabila au ethnicity.
 
Kalikoroga... Na mamlaka za kuchukua hatua ziko kimya tuli kabisa

Jr[emoji769]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…