Greatest Of All Time
JF-Expert Member
- Jan 1, 2017
- 23,620
- 52,790
Kwani GSM wanasemaje?Rais wa TFF, Wallace Karia amesema ligi za Mkoa wa Dar Es Salaam zimekosa mvuto na umaarufu kwasababu ya michuano ya Ndondo Cup ya Clouds Fm.
Pia akaenda mbali zaidi kwa kusema, Ndondo Cup zinatuharibia wachezaji wa ligi kuu kwani wengi huumia wakiwa wanacjeza huko kwenye viwanja vibovu.
Sasa tutaanza kuwa wakali dhidi ya Ndondo Cup.
My take:
Karia baada ya kumfungia Dauda naona vita bado inaendelea, je Karia ataweza kuibuka na ushindi dhidi ya Dauda na Clouds Fm kwa ujumla? Yapi maoni yako?
Kauli yake imeenda too personal!Badala ya yeye kuwaza jinsi ya kuboresha ligi ya mkoa ili iwe bora na maarufu kuliko Ndondo Cup ya Clouds yeye anawaza kuua vilivyofanikiwa. Hapa kuna sehemu ya kufikiri kwa kiwango duni. Viwanja vya ligi kuu ni vibovu, mfano kiwanja cha Sokonne Mbeya au Manungu havifai kwa matumizi lakini hatujasikia akilizungumzia hilo. Ukiangalia jinsi Ndondo Cup inavyoendeshwa hakika lazima uwapongeze waandaaji wake. Hakuna makandokando mengi kama haya aliyonayo Karia na ligi kuu yake.