Wallace Karia: Ligi za Dar zimekosa mvuto kwasababu ya Ndondo Cup

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2017
Posts
23,620
Reaction score
52,790
Rais wa TFF, Wallace Karia amesema ligi za Mkoa wa Dar Es Salaam zimekosa mvuto na umaarufu kwasababu ya michuano ya Ndondo Cup ya Clouds Fm.

Pia akaenda mbali zaidi kwa kusema, Ndondo Cup zinatuharibia wachezaji wa ligi kuu kwani wengi huumia wakiwa wanacjeza huko kwenye viwanja vibovu.

Sasa tutaanza kuwa wakali dhidi ya Ndondo Cup.

My take:
Karia baada ya kumfungia Dauda naona vita bado inaendelea, je Karia ataweza kuibuka na ushindi dhidi ya Dauda na Clouds Fm kwa ujumla? Yapi maoni yako?

9325F878-FCB7-4AFE-B8DF-1A92BF3C70B1.jpeg
 
Kwani GSM wanasemaje?
 
Badala ya yeye kuwaza jinsi ya kuboresha ligi ya mkoa ili iwe bora na maarufu kuliko Ndondo Cup ya Clouds yeye anawaza kuua vilivyofanikiwa. Hapa kuna sehemu ya kufikiri kwa kiwango duni. Viwanja vya ligi kuu ni vibovu, mfano kiwanja cha Sokonne Mbeya au Manungu havifai kwa matumizi lakini hatujasikia akilizungumzia hilo. Ukiangalia jinsi Ndondo Cup inavyoendeshwa hakika lazima uwapongeze waandaaji wake. Hakuna makandokando mengi kama haya aliyonayo Karia na ligi kuu yake.
 
Huyu jamaa amalize tu muda wake atembee. Binafsi simkubali hata kidogo. Ni mtu wa kuendekeza sana fitna na visasi kwa mtu yeyote yule anayetaka kuingilia ulaji wake pale TFF.
 
Anafanya Haya Kwasababu Anajua Hana Cha Kupoteza.

Ila Tanzania Tunahitaji Ndondo Cup Kila Kijiji, Hatuwezi kukaa Na Kutegemea Ligi Kuu.

Mbona Ulaya EPL na Ligi zingine hazijapoteza Mvuto?

Timu Ya Taifa Anaiona?

Ligi Kuu Ilipo Ukiwatoa Wachezaji wa Nje Ina Mvuto Tena?

Ni Ujinga Tuuuu
 
Hana akili huyo msomali ndondo cup imetoa wachezaji kibao wanafanya vizuri ligi kuu akiwemo idi nado wa azam sasa yeye anaangalia upande mmoja tu.
 
Hapa amekwama kwa kweli mashindano kama yale ya uhai Cup yalitoa vipaji kibao Kabla hayajafa,
Kwa sasa hii ndondo ni muhimu Sana kama tunataka vipaji vilivyopo mtaani.
 
Badala ya yeye kuwaza jinsi ya kuboresha ligi ya mkoa ili iwe bora na maarufu kuliko Ndondo Cup ya Clouds yeye anawaza kuua vilivyofanikiwa. Hapa kuna sehemu ya kufikiri kwa kiwango duni. Viwanja vya ligi kuu ni vibovu, mfano kiwanja cha Sokonne Mbeya au Manungu havifai kwa matumizi lakini hatujasikia akilizungumzia hilo. Ukiangalia jinsi Ndondo Cup inavyoendeshwa hakika lazima uwapongeze waandaaji wake. Hakuna makandokando mengi kama haya aliyonayo Karia na ligi kuu yake.
Kauli yake imeenda too personal!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: K11
Back
Top Bottom