Viol
JF-Expert Member
- Dec 15, 2009
- 25,420
- 18,298
Rais wa TFF Wallace Karia amesema wachezaji watakaosafiri kwenda nje hawataruhusiwa kurudi nchini.
Amesema wachezaji wa kigeni watakaosafiri kwenda kwao katika kipindi hiki ambacho ligi imesimama hawataruhusiwa kushiriki ligi ikiwa sehemu ya tahadhari dhidi ya virusi vya Corona.
Wakuu hii imekaaje, hebu tupeane updates za wachezaji waliosafiri.
Maana Kagere kaenda kwao, Luis kaenda kwao, fraga kaenda kwao.
========
WALLACE Karia, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) amesema kuwa wachezaji wote wa kigeni wanaotumika ndani ya Tanzania iwapo wataondoka nchini hawataruhusiwa kurudi tena nchini kwa ajili ya tahadhari dhidi ya Corona.
Karia amesema kuwa, Ligi Kuu Bara imesimamishwa na Serikali ikiwa ni sehemu ya kuchukua tahadhari kwa ajili ya Virusi vya Corona hivyo wanaondoka na kwenda nje ya nchi huko hawatambui aina ya maambukiza yapo kwa kiasi gani.
"Hawajapewa likizo wachezaji bali ligi imesimama kwa ajili ya tahadhari ambayo inachukuliwa kwa sasa, kwa wachezaji wa kigeni watakaokwenda kwenye nchi zao katika kipindi hiki ambacho ligi imesimama, hawataruhusiwa kushiriki ligi ikiwa ni sehemu ya tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona.
"Tutawasiliana na mamlaka husika ili kuona namna gani tutawazuia na hawataweza kushiriki kwenye ligi iwapo hali itatulia kwani tahadhari kuchukuliwa ni muda wote na sio muda mfupi," amesema.
Chanzo: salehjembe.blogspot
And Azam sport 2