Wallace Karia: Wachezaji watakaosafiri nje hawataruhusiwa kurudi

Viol

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2009
Posts
25,420
Reaction score
18,298
Rais wa TFF Wallace Karia amesema wachezaji watakaosafiri kwenda nje hawataruhusiwa kurudi nchini.

Amesema wachezaji wa kigeni watakaosafiri kwenda kwao katika kipindi hiki ambacho ligi imesimama hawataruhusiwa kushiriki ligi ikiwa sehemu ya tahadhari dhidi ya virusi vya Corona.

Wakuu hii imekaaje, hebu tupeane updates za wachezaji waliosafiri.

Maana Kagere kaenda kwao, Luis kaenda kwao, fraga kaenda kwao.

========

karia.PNG

WALLACE Karia, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) amesema kuwa wachezaji wote wa kigeni wanaotumika ndani ya Tanzania iwapo wataondoka nchini hawataruhusiwa kurudi tena nchini kwa ajili ya tahadhari dhidi ya Corona.

Karia amesema kuwa, Ligi Kuu Bara imesimamishwa na Serikali ikiwa ni sehemu ya kuchukua tahadhari kwa ajili ya Virusi vya Corona hivyo wanaondoka na kwenda nje ya nchi huko hawatambui aina ya maambukiza yapo kwa kiasi gani.

"Hawajapewa likizo wachezaji bali ligi imesimama kwa ajili ya tahadhari ambayo inachukuliwa kwa sasa, kwa wachezaji wa kigeni watakaokwenda kwenye nchi zao katika kipindi hiki ambacho ligi imesimama, hawataruhusiwa kushiriki ligi ikiwa ni sehemu ya tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona.

"Tutawasiliana na mamlaka husika ili kuona namna gani tutawazuia na hawataweza kushiriki kwenye ligi iwapo hali itatulia kwani tahadhari kuchukuliwa ni muda wote na sio muda mfupi," amesema.

Chanzo: salehjembe.blogspot

And Azam sport 2
 
Huyu anakurupuka wenye mamlaka ya kuzuia watu kurudi ni serikali labda yeye angesema hawatacheza ligi imesimamishwa kwanini wasirudi kwao
 
Hapo Karia kakurupuka. Serikari bado haijatangaza kufunga mipaka kwa wageni wanaoingia nchini.
 
Mchezaji wa nje ni kwamba ana work permit. Hata Uhamiaji haiwazuii kuingia kwa sasa.

Huyu Msomali kila akifungua mdomo, anatoa fungus tu.

Sijui ana elimu gani huyu. Ni kichaa kichaa.
 
Nimeamini TFF ni genge la wahuni. Nchi yenyewe haijafunga mipaka. Wageni wameruhusiwa kufanya kazi zao. yeye anaropoka tu. Huyu amesoma na amewahi kuwa DED. Je, asingesoma angefafanaje. DED mzima hajui kama maamuzi ya chini hayatakiwi kupingana na sera ya nchi.
 
Hajielewi mbona hakuongea Kabla wakati wanahailisha ligi ndio aseme saivi wakati watu wamesha safiri ngoja tuangalie hii movie ndio kwanza inaanza sijui itaishaje.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio maana nchi hii imo vitani bila ya jemadari wa kuongoza haya mapambano dhidi ya coronavirus,na hii yote inaishia pale mlangoni Magogoni,ilitakiwa our no 1 awe amashatoa msimamo wa nchi kuhusiana na mapambano haya,ameshaunda kamati maalum ya kuwajibika day to day kuhusiana na pandemic hii,mawaziri wa home affairs,afya,nje,ndio walitakiwa wawe kwenye kamati hii,pia our no 1 ilitakiwa awe ameshakutana na viongozi wote wa kitaifa wa kidini ili wote wawe wanaongea lugha moja ili wananchi waelewe uelekeo ni wapi,pia our no 1 ilitakiwa awe ameshakutana na viongozi wote wa kitaifa wa vyama vya kisiasa ili mapambano haya ni ya kiinchi sio kisiasa kwa hiyo wote waunganishe juhudi zao kukabiliana na pandemic hii,ILA my no 1 for one way or another amepuuzia janga hili na matokeo yake kila mtu anatamka vyake,mpaka mjinga mjinga huyu wa chama cha soka anakuja na tamko lake wakati uwezo wa kumzuia mtu kuingia nchini ni la wizara ya mambo ya ndani(uhamiaji),ndugu zangu this pandemic its not a joke na athari yake itaichukua nchi yetu more than 15yrs to recover kiuchumi,maana hata BOT wapo kimya hata wameshindwa kutamka to lower our repo rate ili kulinda uchumi na sarafu yetu!!uaga umewatawala,watanzania wenzangu please jitahidi kujiweka safi hasa mikono yetu , social life zetu ziache kabisa,etc etc ,nawa nawa nawa mikono kwa sabuni na tumia hand sanitiser.
 
Mkuu kuna reason behind,wachezaji wana permit ya kufanya kazi hapa,wameitwa kutumikia timu za taifa kama Kagera aliitwa,shibob aliitwa,the same hata wachezaji wetu walioitwa timu ya taifa walienda kuweka kambi.

Wachezaji wameshaondoka anakuja kutangaza kwanini hakutangaza kabla? Isitoshe kagere ndo mfungaji anaongoza kwa magoli,mbona ule upande wa pili hamna aliondoka,hata hivo upande wa pili wangeondoka hawana viwango.

Tusubiri ila hata hivo kwa hii simba plan imefeli wachezaji wapo wengi halafu wote wapo on fire
Nimeamini TFF ni genge la wahuni. Nchi yenyewe haijafunga mipaka. Wageni wameruhusiwa kufanya kazi zao. yeye anaropoka tu. Huyu amesoma na amewahi kuwa DED. Je, asingesoma angefafanaje. DED mzima hajui kama maamuzi ya chini hayatakiwi kupingana na sera ya nchi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu system yote haipo makini
Ndio maana nchi hii imo vitani bila ya jemadari wa kuongoza haya mapambano dhidi ya coronavirus,na hii yote inaishia pale mlangoni Magogoni,ilitakiwa our no 1 awe amashatoa msimamo wa nchi kuhusiana na mapambano haya,ameshaunda kamati maalum ya kuwajibika day to day kuhusiana na pandemic hii,mawaziri wa home affairs,afya,nje,ndio walitakiwa wawe kwenye kamati hii,pia our no 1 ilitakiwa awe ameshakutana na viongozi wote wa kitaifa wa kidini ili wote wawe wanaongea lugha moja ili wananchi waelewe uelekeo ni wapi,pia our no 1 ilitakiwa awe ameshakutana na viongozi wote wa kitaifa wa vyama vya kisiasa ili mapambano haya ni ya kiinchi sio kisiasa kwa hiyo wote waunganishe juhudi zao kukabiliana na pandemic hii,ILA my no 1 for one way or another amepuuzia janga hili na matokeo yake kila mtu anatamka vyake,mpaka mjinga mjinga huyu wa chama cha soka anakuja na tamko lake wakati uwezo wa kumzuia mtu kuingia nchini ni la wizara ya mambo ya ndani(uhamiaji),ndugu zangu this pandemic its not a joke na athari yake itaichukua nchi yetu more than 15yrs to recover kiuchumi,maana hata BOT wapo kimya hata wameshindwa kutamka to lower our repo rate ili kulinda uchumi na sarafu yetu!!uaga umewatawala,watanzania wenzangu please jitahidi kujiweka safi hasa mikono yetu , social life zetu ziache kabisa,etc etc ,nawa nawa nawa mikono kwa sabuni na tumia hand sanitiser.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa kakurupuka sana nadhani anaona aibu sasa hivi
Mchezaji wa nje ni kwamba ana work permit. Hata Uhamiaji haiwazuii kuingia kwa sasa.

Huyu Msomali kila akifungua mdomo, anatoa fungus tu.

Sijui ana elimu gani huyu. Ni kichaa kichaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kuna reason behind,wachezaji wana permit ya kufanya kazi hapa,wameitwa kutumikia timu za taifa kama Kagera aliitwa,shibob aliitwa,the same hata wachezaji wetu walioitwa timu ya taifa walienda kuweka kambi.

Wachezaji wameshaondoka anakuja kutangaza kwanini hakutangaza kabla? Isitoshe kagere ndo mfungaji anaongoza kwa magoli,mbona ule upande wa pili hamna aliondoka,hata hivo upande wa pili wangeondoka hawana viwango.

Tusubiri ila hata hivo kwa hii simba plan imefeli wachezaji wapo wengi halafu wote wapo on fire

Sent using Jamii Forums mobile app
Just imagine wewe mtu mmoja unawaza hivi. Inakuwaje taasisi nzima imewaza ule upuuzi
 
Back
Top Bottom