Wallace Karia: Wadau wafuate sheria za mpira, waache kushindana na mamlaka wataumia

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF Wallace Karia amewataka Wadau wafuate sheria zilizowekwa katika mpira na kuacha kushindana na mamlaka kwani wataumia.

"Taasisi ya TFF ina miongozo na kanuni ili kufanya mambo yake yaende kama inavyotakiwa na Wadau wote wapite njia moja"

"Ili kufanikiwa hilo, lazima kuwe na vyombo vya ndani vinavyosimamia kila mdau kuwaweka kwenye mstari mmoja"

"Wale wanaotoka nje ya mstari ndiyo hukutana na adhabu mbalimbali, inayofungia ni TFF na siyo Karia"

"Kwahivyo ukishindana na mamlaka utaumia, wanafamilia wa soka wanatakiwa wafute kama mamlaka inavyotaka"

"Kuna watu wanasema eti TFF kazi kufungia, hao ambao walikuwa hawafungii walifika wapi? Hizo document za kufungia sikusaini mimi. Ukiona unataka kubwabwaja basi ukae pembeni".


Wallace Karia akieleza nia ya kutoa mafunzo kwa Wadau kwa waandishi wa habari na michezo kwa ujumla chini ya Cecafa.
 
Tuchambue Kauli za Rais wa Boli au tuache kama ilivyo..!
 
Manara asijazwe bichwa na watu wasiokuwa na vision ya kiutawala wakiamini michambo na kebehi kwa kiongozi vinaweza kumuondoa kwenye kiti

Hersi pia naye ajiangalie mara mbili namuona namna anavyo jaribu kufukuza paka kutumia mkono wenye shombo.

Manara ni toxic na mnafiki aliyetayari ku shift tatizo lake binafsi kulifanya ni tatizo la taasisi.

Mwanzo ilionekana Manara ana matatizo na TFF kwa kile alichokifanya, lakini hakutaka iishe ikiwa hivyo.

Saizi kafanikiwa kuihusisha mpaka Club mpaka viongozi wajuu wote waone TFF ndio adui yao.

So sad hadi humu pia wapo member baadhi washakuwa poisoned wote wanalalamika TFF ya Karia inaichukia Yanga

Binafsi ningeweza kuwaelewa endapo malalamiko hayo dhidi ya TFF yangeanza siku nyingi kabla ya sekeseke la Manara kufungiwa, lakini tangu Manara kafungiwa nauona unafiki wa watu wanaosema TFF ya Karia inaichukia Yanga bila kuhusisha na tukio la Manara.

Kabla ya uongozi wa Karia kuna watu wamefungiwa mpaka miaka 20 na faini za maana kwa sheria hizo hizo, leo hii mtu akifungiwa miaka miwili aonekane kaonewa?
 
unajiuliza hivi Manara ana kitu gani special kwenye soka zaidi ya kebehi na vijembe, kiasi cha kuonekana kufungiwa kwake ni hasara kwa soka? mbona kuna makocha (watu wenye impact) wamefungiwa bila taharuki. Alifungiwa Boniphace Wambura atakuwa huyu msukule?
 
Manara anaringia ualibino wake tu,lakini ajue hata wanyama pori maalbino wapo aache ujinga
 

Attachments

  • 1661411950795.jpg
    29.5 KB · Views: 5
  • FB_IMG_1629996568355.jpg
    20 KB · Views: 7
Naamini huu ujumbe ulishafika sehemu yake, siku hizi yule albino yupo kimya simsikii tena.

Eti "nikitoka hapa naenda zangu kwenye harusi Kigogo" akawachezee wajinga wenzie.

Hawa TFF na ile Kamati ya Maadili nao siwaelewi, ile hukumu ya Hersi na Manara wanasubiri nini kuitolea maamuzi? au wameshalainishwa?
 

Hersi naye apigwe ban tu hakuna jinsi nyingine,lazima mamlaka ziheshimiwe hawataki waende Burundi.
 
Manara na Hersi wanahusikaje moja Kwa moja kwenye hili alilolizungumza Karia?

Au umetumwa na Karia kuelezea kile alichokuwa anakilenga?
 
Fanyeni fujo zenu koote!! Ila mkiigusa tu Yanga kama Yanga, basi mjiandae kwenda na maji. Kuanzia huyo Karia wenu, mpaka Moo na Barbara wake.

Iguswe mara ngapi? Si mlisema mnaandamana hadi Ikulu kumuona Rais ili Haji Manara afunguliwe mbona mumeufyata? Mikwala ya kizamani hiyo fuateni sheria tu mtaishi kwa raha na amani.
 
Fifa inakataza kubwabwaje ?

Kubwabwaje na Different opinions ndio raha ya Soka..., Ukitaka gentleman acts hamia kwenye Golf....
 
Iguswe mara ngapi? Si mlisema mnaandamana hadi Ikulu kumuona Rais ili Haji Manara afunguliwe mbona mumeufyata? Mikwala ya kizamani hiyo fuateni sheria tu mtaishi kwa raha na amani.
Wananchi wataandamana wakiona maslahi yao yanakandamizwa na Wallace Karia! Maana tunamfahamu kwa kina yeye ni nani. Ila hawawezi kuandamana kwa sababu ya Haji Manara.

Kwanza huyu ni mwanachama mwenzenu. Alikuja Yanga kama mwajiriwa tu wa GSM. Na ni baada ya kushindwa kuvumilia yale malipo ya laki 7 mliyo mlipa kwa mwezi.
 

Wenzako wako tayari kuandamana kwa ajili ya Haji Manara. Tatizo lenu mna hofu ya kitu kisichopo, huyo Karia anayo mapungufu yake lakini siyo kiwango mnachokihisi nyie kwani anajua kabisa kuwa yeye ni Rais wa TFF na TFF haiwezi kuwepo bila uwepo wa vilabu vya mpira hasa Simba na Yanga hivyo hawezi kuwa na nia ovu na Club yenu kwa kiwango mnachowaza nyie.
 
Maslahi gani?

Kila kitu kinaendeshwa na sheria, ukitaka maslahi yako yazidi kuwepo basi hakikisha hukiuki sheria zilizowekwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…