Walter Elias Disney: Baba wa filamu za animation na mwanzilishi wa kampuni maarufu duniani ya 'Disney'

I am Groot

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2018
Posts
3,929
Reaction score
10,747

Walter Elias Disney
Alizaliwa Chicago 1901, Disney alianza mapema sana kuvutiwa na maswala ya uchoraji. Aliingia kwenye madarasa ya sanaa ya michoro waksti wa utoto wake na alipotimiza miaka 18 alifanikiwa kupata kazi aliyokuwa kama commercial illustrator.

Alihamia California mapema miaka ya 1920 na kufungua studio yake 'Disney Brothers studio' kwa kushirikiana na kaka yake aliyeitwa Roy. Mwaka 1928 alitengeneza character wake wa kwanza aliyempa jina la Mickey Mouse, na ndiye aliyempa mafanikio ya mwanzoni. Kadri studio ilivyoendelea kukua, teknolojia pia iliendelea kuimarika, alianza kuboresha kazi yake kwa kuongezea sauti na rangi kwenye katuni alizokuwa akizitengeneza.

Disney anashikilia rekodi ya kushinda tuzo 22 za Oscar kutoka nomination 59, golden global 2, Emmy Awards na nyinginezo nyingi.

Matokeo ya maendeleo ya teknolojia ya animation ilipozidi kukua alitambulisha zake za mwanzo zenye
ubora kama;


Snow white and the seven dwarfs (1937)



Pinocchio na Fantasia (1940)


Dumbo (1941)


Bambi (1942)


Filamu zaidi za animation na (live action) ziliendelea kutoka baada ya vita kuu ya 2 ya dunia kama;

Cinderella (1950) na Mary Poppins (1964) zilizompatia tuzo ya Academic Award.

Disney alikuwa mtu wa aibu na mwenye kupenda utulivu. Pamoja na hayo alikuwa ni mvutaji mkubwa wa sigara na inasemekana ndicho kilicho sababisha umauti wake baada ya kugundulika na kansa ya mapafu. Alikufa mwaka 1966.

Amebaki kama alama muhimu katika historia ya animation.Kazi zake za filamu zimeendelea kuonyeshwa, na katika jina lake studio na kampuni zake zimeendelea kusimamia ubora wa hali ya juu katika bidhaa zake hasa zijulikanazo entertainment, Disney park zake pia zimeendelea kukua kiukubwa na wingi wa namba za watembeleaji katika nchi kadhaa alizojiwekeza.
 
Bingwa sana huyu. Jina litaishi muda mrefu kuliko aliyezaa watoto 10 na mataifa mbalimbali.
 
Legend wa ukweli huyu nguli nakubali Sana hasa hustle zake,alishawahi filisika ila akarudi Kwa kishindo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…