Wamachinga hawasaidii Tanzania!

Namshukuru Raisi kuwa mkweli na mwenye maono na kukubaliana na mimi "" Hawalipi kodi"
Wewe kama ndio mshauri wa Rais you are hopeless

Machinga wanasaidia stock turnover over ya walipa kodi wakubwa na wazalishaji kwenda haraka ambayo inamaanisha kodi kubwa kukusanywa kwa wafanya biashara wakubwa na wenye viwanda

Umesikia wewe kidesiki officer Lofa wa serikali
 
Wamachinga sio wa kulaumiwa. Serikali ndo ya kubebeshwa lawama. Kama serikali ingekuwa na sheria na sera nzuri kuhusu kilimo basi vijana wengi wangekimbilia huko. Hapa TZ utakuta mkulima kapambana lakini siku ya mavuno anakutana na serikali inayompangia auze vipi mazao yake ambapo serikali haikumsaidia chochote hadi siku ya mavuno. Pia badala ya serikali kuwekeza kwenye vyuo vya ufundi inaenda kufanya miradi isiyo na maana yoyote. Kwa mfano hela za kujenga daraja la coco beach zingeweza kuboresha vyuo vingapi vya VETA? WAMACHINGA wako pale kupambana na ugumu wa maisha uliosababishwa na serikali yao wenyewe.
 
Mimi sikutafuti hii topic ni yangu!. Nimesema ukweli tu. Tusipoteze muda kubishara ukweli badala yake toa mawazo yako kama unapingana na mimi na Raisi Samia kwenye hili jambo ili tusaidie nchi yetu.
Sioni chochote kipya ulichogundua wewe ambacho unataka nikipinge au nikiunge mkono hapa.
Ninachoona ni juhudi zako tu za kuhalalisha uonekane una hoja.

Hata hivyo, nadhani unayo matatizo makubwa katika ufahamu wako.

Mada yako inasema "Wamachinga hawasaidii Tanzania"

Sijasikia mahali popote ndani ya aliyosema rais kuhusu kukubaliana nawwe juu ya hilo.

Mbona unajitweza sana kutaka kujionyesha kwamba rais amesikia habari hii toka kwako kabla hajaizungumzia, na wewe unatafuta cheo huko serikalini? Si ndio tutakuwa tumekwisha kama nchi?
 
kama kawaida tunaanza kueleweka sasa!!
 

Kwahiyo kariakoo imekuzwa na wamachinga?[emoji23][emoji23][emoji23]
 

Kwani hivyo vitu vikiuzwa madukani hatutanunua? Kwani wamachinga wao wanapatia wapi? Wamachinga waondolewe barabarani wakafanye kazi zao kwa utaratibu
 

Wameanza kunielewa
 
Kweli ni laaana kwa taifa,
 
Huu uzi ni wa kipumbavu. Machinga wapo kila mahali hata huko China na Ulaya. Cha msingi ni kudhibiti tu movements zao na sio kuwaondoa kwasababu kuwaondoa kilazima ni mwanzo wa kutetereka usalama wa nchi hii. Mimi naona twende nao tu hivyohivyo kibishi kwasababu hata huko kwenye kilimo mbolea haishikiki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…