Wamachinga hawasaidii Tanzania!

Wamachinga hawasaidii Tanzania!

Namshukuru Raisi kuwa mkweli na mwenye maono na kukubaliana na mimi "" Hawalipi kodi"
Wewe kama ndio mshauri wa Rais you are hopeless

Machinga wanasaidia stock turnover over ya walipa kodi wakubwa na wazalishaji kwenda haraka ambayo inamaanisha kodi kubwa kukusanywa kwa wafanya biashara wakubwa na wenye viwanda

Umesikia wewe kidesiki officer Lofa wa serikali
 
Wamachinga sio wa kulaumiwa. Serikali ndo ya kubebeshwa lawama. Kama serikali ingekuwa na sheria na sera nzuri kuhusu kilimo basi vijana wengi wangekimbilia huko. Hapa TZ utakuta mkulima kapambana lakini siku ya mavuno anakutana na serikali inayompangia auze vipi mazao yake ambapo serikali haikumsaidia chochote hadi siku ya mavuno. Pia badala ya serikali kuwekeza kwenye vyuo vya ufundi inaenda kufanya miradi isiyo na maana yoyote. Kwa mfano hela za kujenga daraja la coco beach zingeweza kuboresha vyuo vingapi vya VETA? WAMACHINGA wako pale kupambana na ugumu wa maisha uliosababishwa na serikali yao wenyewe.
 
Mimi sikutafuti hii topic ni yangu!. Nimesema ukweli tu. Tusipoteze muda kubishara ukweli badala yake toa mawazo yako kama unapingana na mimi na Raisi Samia kwenye hili jambo ili tusaidie nchi yetu.
Sioni chochote kipya ulichogundua wewe ambacho unataka nikipinge au nikiunge mkono hapa.
Ninachoona ni juhudi zako tu za kuhalalisha uonekane una hoja.

Hata hivyo, nadhani unayo matatizo makubwa katika ufahamu wako.

Mada yako inasema "Wamachinga hawasaidii Tanzania"

Sijasikia mahali popote ndani ya aliyosema rais kuhusu kukubaliana nawwe juu ya hilo.

Mbona unajitweza sana kutaka kujionyesha kwamba rais amesikia habari hii toka kwako kabla hajaizungumzia, na wewe unatafuta cheo huko serikalini? Si ndio tutakuwa tumekwisha kama nchi?
 
kama kawaida tunaanza kueleweka sasa!!
 
Mleta mada utakuwa mfanyakazi wa serikali siku ukifungua Duka la jumla ukitumbuliwa nk ndio utajua machinga ni nani kuwa wanachukua bidhaa toka eneo lako choka Mbaya lisilo na wateja kupeleka eneo la wateja ili wewe ujidai kulipa pango na kodi na kujitia majidai kuwa uko prime business area ambalo hata TRA wanatolea mimacho kumbe hawajui wanaolimbatisha chati hilo eneo sio location walipo ni machinga wabeba bidhaa kuzunguka nazo masoko yaliko

Kwahiyo kariakoo imekuzwa na wamachinga?[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Sawa waweza sema machinga hawalipi kodi lakini ndio wasababishaji wa stock turnover ya wafanya biashara wakubwa walipa VAT kwenda haraka na kuagiza mzigo mwingine VAT and custom duty taxable ndio wanakimbiza tax turnover kwa Kukimbiza haraka sales turnover
Mleta mada ukikariri notice hukuelewa masomo

Kwani hivyo vitu vikiuzwa madukani hatutanunua? Kwani wamachinga wao wanapatia wapi? Wamachinga waondolewe barabarani wakafanye kazi zao kwa utaratibu
 
Watanzania wengi hawajui kwamba Wamachinga hawasaidii nchi yetu badala yake wanatumika kwa siasa pekee. Watanzania wanashangilia wamachinga ambao hawalipi kodi halafu wanalalamika wenyewe kuongezewa kodi!

1. Hawalipi kodi yeyote ya maana na vibali vya machinga ni kama kukejeli Watanzania.

2. Wachafuzi wa mazingira. Hivi hizi gharama za usafi analipa nani hasa kwa watu wasio lipa kodi.

3. Wanauza vitu vya kijinga ambavyo havina msaada wowote wa maana kwa viwanda vyetu wala sera muhimu kama kilimo, elimu au afya.

4. Wanasaidia viwanda vya china sio Tanzania hebu tukaangalie kama vitu vya machinga ni vya Tanzania! Utakuta ni majalala ya kichina hivyo tunasaidia wachina na sio Tanzania.

5. Wanaua wafanyabiashara wadogo ambao wanalipa kodi maana wameweka magenge ambayo hayana mpangilio mbele ya biashara nyingine

Wameanza kunielewa
 
Kweli ni laaana kwa taifa,
 
Huu uzi ni wa kipumbavu. Machinga wapo kila mahali hata huko China na Ulaya. Cha msingi ni kudhibiti tu movements zao na sio kuwaondoa kwasababu kuwaondoa kilazima ni mwanzo wa kutetereka usalama wa nchi hii. Mimi naona twende nao tu hivyohivyo kibishi kwasababu hata huko kwenye kilimo mbolea haishikiki.
 
Back
Top Bottom