Wamachinga Simu 2000 wamshukia Albert Chalamila, wasema kauli kuwa machinga wanatakiwa kustaafu miaka mitatu ilhali wanasiasa hawastaafu inashangaza

Wamachinga Simu 2000 wamshukia Albert Chalamila, wasema kauli kuwa machinga wanatakiwa kustaafu miaka mitatu ilhali wanasiasa hawastaafu inashangaza

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Kamati ya maboresho ya Soko la Simu 2000 chini ya mwenyekiti wake pamoja na wafanyabiashara na wadau wa stendi wa Simu 2000 wameongea na waandishi wa habari leo Julai 17, 2024 kuhusu yaliyojiri tangu kumaliza kikao chao na mkuu wa Mkoa, Albert Chalamila.

Mosi, mwenyekiti amesema wafanyabiashara sio wavamizi kwenye eneo hilo bali waliletwa na Serikali. Wamesema kitendo cha Mkuu wa Mkoa kusema pale sio kwa mama zao na baba zao haikuwa kauli ya kiungwa na haikupaswa kutolewa na Kiongozi ambaye amepewa dhamana na Serikali ya kuhudumia wananchi kwa niaba.

Mwenyekiti amesema wao ni watanzania na baba na mama yao ni Tanzania na walipo ni sehemu yao maana wao ni sehemu ya watanzania kwasababu ipo kwenye ardhi ya Tanzania.

Mwenyekiti: Hawa viongozi tumewapa dhamana ya kuongoza na kusimamaia kero na changamoto zetu pamoja na mapungufu kama aliyaona mkuu wa Mkoa hakupaswa kuzungumza kauli kama zile ya kwamba Machinga sasa anatakiwa akae miaka miwili au mitatu awe amestaafu kuwa machinga, atoke sehemu kama hizi aende sehemu zingine.

Unajiuliza, hawa ni viongozi ambao wanaishi kwa kodi zetu, wanakaa miaka mitano mpaka kumi basi kwanini yeye hakuona umuhimu wa kutoa ushauri kwamba sasa wakuu wa mikoa kwasababu mikoa iko michache Tanzania na watanzania ni wengi na wao wanapenda kuwa viongozi, wanufaike na keki ya Taifa, kwanini asiwe wa kwanza kutoa mapendekezo sasa mkuu wa mkoa anatakiwa kukaa miaka miwili/mitatu baada ya hapo amuachie mtu mwingine.

Akaona hawa wamachinga ambao walikuwa wanakaa kwenye jua kwa muda mrefu, wamekuja sokoni kujitafuta anadhani miaka miwili inatosha kuacha umachinga na akatufute fremu, sijajua taaluma ipi ya uchumi inakubaliana na hili jambo.

Anasema mmefinywa na waume zetu mnajiliza hapa unafiki, kweli unamwambia mtu jambo analia machozi unamwambia ni mnafiki! Yale machozi ya wafanyabiashara waliona ni adha wanaenda kupitia kupitia huu mradi ndio maana walianza kupata picha ya nini kinafata kwasababu wameshahangaika muda mrefu. Walikuwa Ubungo wakatolewa, walikuwa wapi wakatolewa, wameshanyang'anywa mizigo sana, wameletwa sokoni wameambiwa sasa kaeni hapa ni sehemu rasmi, tena inakuja kwamba hapa sio sehemu rasmi.

Karakana ni muhimu kuliko wafanyabiashara wadogo wadogo, hii inaweza ikajenga picha sasa viongozi wa nchi yetu hawajali tena mtu wa hali ya chini na kuna wafanyabiashara walinifata wakaniambia kwelie angekuwepo marehemu haya maneno yasingewezwa kuzungumzwa.

Kauli za nitaamuru polisi wapige push up juu ya migongo yenu zilikuwa ni fedheha, ni udhalilishaji na ni kutweza utu wa mtu.

Tunaomba kutumia fursa hii kumuomba mkuu wa mkoa kwamba hizi kauli asizitumie tena mahala popote ndani ya nchi yetu kwasababu pia zinaifanya Serikali ipate taswira mbaya kwa wananchi wake na kauli zile zinaweza zikajenga chuki baina ya Serikali na viongozi.

View: https://www.youtube.com/live/naKo4HNboMs
 
images (7).jpeg
 
Ndiyo wasomi wetu hao kina Makala halafu ulonganishe na kina Makonda ambao wanaitwa wajinga!
CCM wote ni sawa. Wamelewa madaraka. Hivi mnadhani mkuu wa mkoa anaweza kukurupuka na kutoa amri na kejeli za aina hiyo bila kutumwa na aliyemteua? Nimesikia hao wafanya biashara wajinga kabisa wakisema ''rais wao msikivu'' awasikilize na watampa ''mitano tena''. Kweli hawa ni mananga wa kutupwa. Badala ya kupigana kuondoa tatizo la Tanzania ambalo ni uongozi mbovu wa CCM, wao wanajipendekeza kwa kusema wanampa ''mitano tena''. Ndiyo maana hata kiazi Chalamila anawakebehi kwa sababu amaeona ni wajinga kupitiliza.
 
Rais hawezi kumtuma mkuu wa mkoa akaongee ujinga kama ule.

Acha kumsingizia Rais kwa mambo yanayofanywa na watu wenye mihemko wasiojua nini chakusema.

Kama Rais angekuwa anamtuma kwanini Rais alimwambia Chalamila aache tabia yake ya ujeuri na Chalamila akakiri ameacha?
 
Mbowe ni tajiri watoto wake wapo Ulaya
Wanataka maandamano yakikaribia Mbowe atume nauli warudi kuandamana.Yaani watu wajinga ni vituko.Tajiri asiye na shida ya kula anawasemea na kuwapigania wanataka na watoto wake wawepo.Ina maana hata Mbowe akiwaajiri na akitaka awalipe ujira wao nadhani watataka familia ya Mbowe nayo ilipwe.
 
Rais hawezi kumtuma mkuu wa mkoa akaongee ujinga kama ule.

Acha kumsingizia Rais kwa mambo yanayofanywa na watu wenye mihemko wasiojua nini chakusema.

Kama Rais angekuwa anamtuma kwanini Rais alimwambia Chalamila aache tabia yake ya ujeuri na Chalamila akakiri ameacha?
RC ni mwakilishi wa nani?
 
Wanataka maandamano yakikaribia Mbowe atume nauli warudi kuandamana.Yaani watu wajinga ni vituko.Tajiri asiye na shida ya kula anawasemea na kuwapigania wanataka na watoto wake wawepo.Ina maana hata Mbowe akiwaajiri na akitaka awalipe ujira wao nadhani watataka familia ya Mbowe nayo ilipwe.
Wabaki na shida zao ziwapige haswa
 
Back
Top Bottom