Wamachinga Simu 2000 wamshukia Albert Chalamila, wasema kauli kuwa machinga wanatakiwa kustaafu miaka mitatu ilhali wanasiasa hawastaafu inashangaza

Wamachinga Simu 2000 wamshukia Albert Chalamila, wasema kauli kuwa machinga wanatakiwa kustaafu miaka mitatu ilhali wanasiasa hawastaafu inashangaza

Kamati ya maboresho ya Soko la Simu 2000 chini ya mwenyekiti wake pamoja na wafanyabiashara na wadau wa stendi wa Simu 2000 wameongea na waandishi wa habari leo Julai 17, 2024 kuhusu yaliyojiri tangu kumaliza kikao chao na mkuu wa Mkoa, Albert Chalamila.

Mosi, mwenyekiti amesema wafanyabiashara sio wavamizi kwenye eneo hilo bali waliletwa na Serikali. Wamesema kitendo cha Mkuu wa Mkoa kusema pale sio kwa mama zao na baba zao haikuwa kauli ya kiungwa na haikupaswa kutolewa na Kiongozi ambaye amepewa dhamana na Serikali ya kuhudumia wananchi kwa niaba.

Mwenyekiti amesema wao ni watanzania na baba na mama yao ni Tanzania na walipo ni sehemu yao maana wao ni sehemu ya watanzania kwasababu ipo kwenye ardhi ya Tanzania.

Mwenyekiti: Hawa viongozi tumewapa dhamana ya kuongoza na kusimamaia kero na changamoto zetu pamoja na mapungufu kama aliyaona mkuu wa Mkoa hakupaswa kuzungumza kauli kama zile ya kwamba Machinga sasa anatakiwa akae miaka miwili au mitatu awe amestaafu kuwa machinga, atoke sehemu kama hizi aende sehemu zingine.

Unajiuliza, hawa ni viongozi ambao wanaishi kwa kodi zetu, wanakaa miaka mitano mpaka kumi basi kwanini yeye hakuona umuhimu wa kutoa ushauri kwamba sasa wakuu wa mikoa kwasababu mikoa iko michache Tanzania na watanzania ni wengi na wao wanapenda kuwa viongozi, wanufaike na keki ya Taifa, kwanini asiwe wa kwanza kutoa mapendekezo sasa mkuu wa mkoa anatakiwa kukaa miaka miwili/mitatu baada ya hapo amuachie mtu mwingine.

Akaona hawa wamachinga ambao walikuwa wanakaa kwenye jua kwa muda mrefu, wamekuja sokoni kujitafuta anadhani miaka miwili inatosha kuacha umachinga na akatufute fremu, sijajua taaluma ipi ya uchumi inakubaliana na hili jambo.

Anasema mmefinywa na waume zetu mnajiliza hapa unafiki, kweli unamwambia mtu jambo analia machozi unamwambia ni mnafiki! Yale machozi ya wafanyabiashara waliona ni adha wanaenda kupitia kupitia huu mradi ndio maana walianza kupata picha ya nini kinafata kwasababu wameshahangaika muda mrefu. Walikuwa Ubungo wakatolewa, walikuwa wapi wakatolewa, wameshanyang'anywa mizigo sana, wameletwa sokoni wameambiwa sasa kaeni hapa ni sehemu rasmi, tena inakuja kwamba hapa sio sehemu rasmi.

Karakana ni muhimu kuliko wafanyabiashara wadogo wadogo, hii inaweza ikajenga picha sasa viongozi wa nchi yetu hawajali tena mtu wa hali ya chini na kuna wafanyabiashara walinifata wakaniambia kwelie angekuwepo marehemu haya maneno yasingewezwa kuzungumzwa.

Kauli za nitaamuru polisi wapige push up juu ya migongo yenu zilikuwa ni fedheha, ni udhalilishaji na ni kutweza utu wa mtu.

Tunaomba kutumia fursa hii kumuomba mkuu wa mkoa kwamba hizi kauli asizitumie tena mahala popote ndani ya nchi yetu kwasababu pia zinaifanya Serikali ipate taswira mbaya kwa wananchi wake na kauli zile zinaweza zikajenga chuki baina ya Serikali na viongozi.

View: https://www.youtube.com/live/naKo4HNboMs

Hivi huyu Chalamila na Nape si huenda biological father wao akawa ni mtu mmoja!
 
Wafanyabiashara wanaofanya shughuli zao kwenye soko lililopo stendi ya mabasi Simu 2000 wamelaani vikali baadhi ya kauli zilizotolewa na Mkuu wa mkoa Dar es salaam, Bw Albert Chalamila baada ya mgomo uliofanywa na wafanyabiashara hao hivi karibuni.

Akizungumza na wanahabari, Mwenyekiti wa wafanyabiashara hao bw Mussa Ndile amelaani kauli hizo na kumtaka mkuu wa mkoa kushughukia swala lao badala ya kuwabeza na kuona madai yao si ya msingi.

"Kweli mtu analia kwa uchungu, unasema anajiliza vimachozi kwasababu amefinywa na mumewe nyumbani! Na kwamba anajiliza kwa unafiki! Hizi kauli si nzuri na tunaomba zisijirudie tena. Sisi hatuna ubaya na Mkuu wa mkoa na ndio maana alipokuja mara ya kwanza tuliosha gari lake na tulimtunza mia mbili mbili zetu lakini alipokuja mara ya pili kwa kweli kauli zake zilituvunja moyo na tunaomba kauli kama hizi asizitumie tena" Alisisitiza bw. Ndile.

Mnamo Julai 8, wafanyabiashara wa soko lililopo ndani ya stendi ya mabasi ya simu 2000 waligoma na kufunga barabara wakipinga mpango wa kugawa sehemu ya eneo la soko hilo kwa ajili ya ujenzi wa karakana ya mabasi ya Mwendokasi (Dart)
 
Hapo ndio mlianza kukosea
 
dah hii nchi mbna usegeju umezidi sana watu wanaona kama ni ya kwao
 
Back
Top Bottom