Wamachinga waliosalia katikati ya Mji Iringa wasakwa

Wamachinga waliosalia katikati ya Mji Iringa wasakwa

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Meya wa Manispaa ya Iringa, Ibrahim Ngwada amesema Wafanyabiashara wanaofanya shughuli zao wakati wa usiku ni changamoto na hawatakiwi kuwepo maeneo hayo, hivyo watakamatwa na kushitakiwa.

Meya Ngwada ameyasema hay oleo Aprili 12 alipokuwa akizungumza na Mwananchi mjini hapa, akisema licha ya baadhi ya wafanyabiashara kuruhusiwa kufanya kazi zao usiku katikati ya mji huo, baadhi yao wameingia kwenye maeneoi yasiyoruhusiwa.

Kauli ya Meya Ngwada imekuja kufuatia kuhamishwa kwa Wamachinga kutoka katikati ya mji na kupelekwa eneo la Mlandege mwezi uliopita.

"Maeneo rasmi yametengwa sasa ijulikane wazi hawaruhusiwi watu hao kufanya biashara katikati ya mji kwa maeneo yasiyo rasmi na sahihi kwa upande wao Wamachinga," amesema Ngwada

Kwa upande wake Mwenyekiti wa umoja wa Wamachinga Mkoa wa Iringa, Yahaya Mpelembwa amekiri kuwepo kwa changamoto japo ni kundi dogo la wafanyabiashara hao, kwani Wamachinga wengi wamehamia eneo la Mlandege na wanaendelea na biashara kama ilivyokuwa awali katikati ya mji.

Mpelembwa ameendelea kusema kwa uongozi wa umoja wa Wamachinga bado unaendelea kutoa elimu kwa wale wachache ambao wanaendelea kufanya biashara zao sehemu zilizopigwa marufuku.

"Wamachinga waliobakia katika maeneo marufuku wafanye jitihada na kukubali kuhama Kama wengi wa umoja wa Wafanyabiashara walishahama wanafanya biashara zao , Kila mmoja afahamu Kila kitu kinamuanzilishi ndipo kinakuwa kizuri hata miyomboni au mashine tatu inayongangania Leo hii ina watu walioanza biashara pale kwa mazingira mapya mpka kufikia pale"alisema Mpelembwa

Mwananchi imeshuhudia wafanyabiashara hao wakifanya biashara zao wakati wa usiku katika maeneo yaliyopigwa marufuku bayo ni tembo baa na mashine tatu.

Wamachinga hao wamesema ni ngumu kwao kufanya biashara zao katika soko la Mlandege wakati wote hivyo inawalazimu kuja usiku maeneo yasiyo rasmi kutafuta wateja ikiwa ni rahisi kwao na wamepazoea.

"Unakuta inafika jioni hujauza kwa uhakika hivyo inabidi tujitose ili tupate ridhiki kidogo," amesema Hamish Bakari.

MWANANCHI
 
Back
Top Bottom