Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Mapenzi huwa hayachagui, unakuta kijana amefika amekwisha kwa dada wa kazi. Mara nyingi mama akisikia habari hii huwa anaona kama inamshushia heshima katika jamii inayomzunguka.
Wengi wanapenda mtoto wake amuoe mtoto wa rafiki au watu wa kaliba yake. Wamama wenye busara hushukuru kuwa mtoto wake amempata mtu ambae na yeye ana mfahamu na hasa kama ameridhika na tabia za binti.
Wamama wengine huwapa dada wa kazi hela na kuwatisha waondoke haraka na wapotee kwenye maisha ya vijana wao. Huu ni ukatili unaosababisha msongo wa mawazo kwa vijana wao baada ya penzi changa kukatishwa ghafla.
Wa mama ndoa ni jambo la kheri, kama kijana amependa, kazi ya mtu si kasoro.