Wamanyema ndio kabila pekee lenye watu majasiri, shupavu, na wajanja hapa nchini

Natoa salamu kwenu marafiki na ndugu zangu. Kwa wale wasiolifahamu hili kabila. Wamanyema ni kabila linalopatikana katika mkoa wa Kigoma, hasa hasa maeneo ya mjini kama vile Kigoma mjini, Ujiji, Mwanga, Gungu na baadhi ya maeneo ya Kasulu mjini.

Yani toka enzi za ukoloni mpaka leo hii, mtoto wa mjini pale Kigoma ni mmanyema, japo miaka hii kuna waha wachache waliojisogeza sogeza na kufoji uenyeji wa mjini kwa kuiga mienendo na tamaduni za kimanyema nk.

Pia kabila hili la Wamanyema linapatikana katika baadhi ya maeneo ya mkoa wa Tabora, na huko Ufipa mkoani Rukwa.

Wamanyema ni kabila la pili kwa ukubwa mkoani Kigoma, kabila la kwanza kwa ukubwa mkoani humo ni Waha ambao wengi wanaishi vijijini, pamoja na makabila mengine madogo madogo.

Wamanyema ni kati ya makabila ya mwanzo mwanzo kabisa kufika katika mkoa wa Dar es salaam enzi hizo ikiitwa mzizima, kabla hata Tanganyika haijawaza au hata kufikiria kuwa kuna siku itapata uhuru.

Pia Wamanyema ndio lilikuwa kabila la kwanza la wageni kumiliki maeneo yote muhimu ambayo sasa ndio mjini kama vile Kariakoo, Ilala na Tabata.

Kwa watu wanaoishi au waliowahi kufika Dar es salaam nafikiri mnaufahamu msikiti wa Manyema uliopo katika katika ya mjini yani kariakoo, ule msikiti ulijengwa kabla ya uhuru na hakuna mkoloni yeyote aliethubutu kuugusa kwa vile hata wakoloni walilifahamu vizuri hili kabila, kwamba sio la kulifanyia mzaha hata kidogo.

Kabla mambo ya utandawazi hayajaeneo na kupelekea waha kuvamia miji kwa fujo hasa kwa mkoa wa Dar es salaam, watu wengi walikuwa wanajua kuwa Wamanyema ndio kabila pekee katika mkoa wa Kigoma.

Ila miaka inavyokwenda ndo na mambo yanavyozidi kujiweka wazi yenyewe, na kupelekea watu kujua makabila mengine ya mkoa wa Kigoma.

Wamanyema ni kati ya Makabila yaliopigania uhuru kwa kupambana na wakoloni, huku wakishirikiana na wenyeji wao wa Dar es salaam kama vile Wazaramo, Wandengereko na makabila mengine ya mkoa wa Pwani.

Tabia za wamanyema wake kwa waume ni 1] usafi 2] umaridadi 3]unadhifu. Wamanyema wengi ni maridadi sana kuanzia kwenye swala la mavazi, usafi wa mwili ndani na nje, pia huwa hawajinyimi kula.

Ni vigumu sana kumkuta mmanyema anatembeza mayai, sijui vikapu vya mafuta uzuri na biashara nyingine ndogo ndogo za kuzurula juani, hizi biashara kwa watu wanaotokea Kigoma iwe kwa mkoa wa Kigoma wenyewe, Dar au kwengineko huwa zinafanywa na waha.

Kwa mtu ambae ashawahi kuishi na wamanyema iwe jirani au nyumba moja nafikiri atakuwa amenielewa. Kama una mkeo au mumeo akinaswa na mmanyema tu basi andaa talaka, au kama mwanamke andaa kutalikiwa kabisa, maana mkeo au mumeo ndo umeshamkosa tayari.

Sifa nyingine 4]ubishi 5]kujiamini kupita kiasi. Mmanyema anaweza kutoa hela yake mfukoni akaununua ugomvi wa rafiki yake, na kuanza kupambana kwa niaba yake.

Watu maarufu kutoka katika kabila la Wamanyema ni 1]Sheikh Yahya Husein (aliekuwa mtabiri afrika mashariki) 2] Iddi Faiz Mafongo (aliekuwa mwekahazina wa chama cha TANU) 3] Iddi Tosiri 4] Iddi Simba (huyu mama alikuwa mmanyema, huku baba ni mdengereko) 5] Amri Abedi Karuta (meya wa kwanza jijini Dar) 6] Amani Kabouru (aliekuwa mbunge wa kwanza Kigoma mjini CDM) 7] Diamond 8] Ally Kiba 9] Ommy Dimpoz 10] mh Zitto Kabwe kiongozi wa ACT wazalendo (mbunge mstaafu) 11] Katibu mkuu kiongozi mh balozi Huseein A.
Katanga na wengine wengi serikalini, siasani, kwenye michezo, mziki na fani mbali mbali.

Tatizo kubwa la Wamanyema wa enzi hizo (yani mababu) ilikuwa ni ushirikina. Jambo lililosababisha wamanyema wengi kusambaa katika mikoa mingine hasa Dar es salaam na kujenga huko ili kuwaepuka vigagula hao.

Pia wamanyema hawana ushirikiano kivile katika mambo yanayohusu maisha. Iwe kazini, katika biashara na mambo mengi ya kimaendeleo huwa hawabebani kama yanavyobebana makabila mengine, yani kwa wamanyema kila mtu hubeba msalaba wake mwenyewe.

Kwa kukosa kushirikiano huo ndio maana mababu ambao ndio waliwahi kuwa wamiliki wa maeneo ya Kariakoo, Ilala, Tabata nk walipofariki, wale waliorithishwa maeneo hayo waliyauza yote kwa wahindi (K'koo) waarabu (Ilala) pia maeneo mengi ya Tabata waliorithishwa waliyauza kwa watu mbali mbali.
Umesahau kua wadada wa kimanyema sio wachoyo...nimeruka nao sana enzi nasoma tabora mitaa ya kanyenye,mwz road,rufita,isevya wamejaa huko
 
Yaani list yako imejaa waganga na wasanii et wajanja .wamanyema ndo watumwa waliobebeshwa ndovu na wazungu .
Karne ya 20 bado unawaza habari za uganga, kweli wewe ni mwanakijiji. Sisi watoto wa mjini tunawaza hela na sio uganga.

Usanii ni moja ya njia ya kijanja ya kumsaidia mtu kuishi vizuri mjini.

Leo hii Davido anaonekana bora na mjanja kuliko wanasiasa wengi kule Nigeria.
Kuna mtu anawaza waganga ka mmaanyema. Hapo si umemtaja sheikh yaya yule tapeli kwamba yule mtoto wa mjini.mi toka kigoma naowakubali waha
Wanapiga kazi na wanasafiri kujifunza kwenu ujiji hadi leo ukiwa na mil 5 unapata nyumba kabisa
 
Swala la ndoa ni la mtu binafsi, karibu mikoa yote Tz watu wanauwana kwa sababu za wivu wa kimapenzi. Hivyo hii ni sifa ya taifa sio kabila.
Pana makabila waliozidi kwa usumbufu labda awe amesoma na anayo dini.
Mfano wajita,wadigo
 
Yaani list yako imejaa waganga na wasanii et wajanja .wamanyema ndo watumwa waliobebeshwa ndovu na wazungu .
Kuna mtu anawaza waganga ka mmaanyema. Hapo si umemtaja sheikh yaya yule tapeli kwamba yule mtoto wa mjini.mi toka kigoma naowakubali waha
Wanapiga kazi na wanasafiri kujifunza kwenu ujiji hadi leo ukiwa na mil 5 unapata nyumba kabisa
Sheikh Yahaya!!

Kwahiyo mtu akiwa mwizi, basi kabila lake lote linakuwa la wezi?
 
Natoa salamu kwenu marafiki na ndugu zangu. Kwa wale wasiolifahamu hili kabila. Wamanyema ni kabila linalopatikana katika mkoa wa Kigoma, hasa hasa maeneo ya mjini kama vile Kigoma mjini, Ujiji, Mwanga, Gungu na baadhi ya maeneo ya Kasulu mjini.

Yani toka enzi za ukoloni mpaka leo hii, mtoto wa mjini pale Kigoma ni mmanyema, japo miaka hii kuna waha wachache waliojisogeza sogeza na kufoji uenyeji wa mjini kwa kuiga mienendo na tamaduni za kimanyema nk.

Pia kabila hili la Wamanyema linapatikana katika baadhi ya maeneo ya mkoa wa Tabora, na huko Ufipa mkoani Rukwa.

Wamanyema ni kabila la pili kwa ukubwa mkoani Kigoma, kabila la kwanza kwa ukubwa mkoani humo ni Waha ambao wengi wanaishi vijijini, pamoja na makabila mengine madogo madogo.

Wamanyema ni kati ya makabila ya mwanzo mwanzo kabisa kufika katika mkoa wa Dar es salaam enzi hizo ikiitwa mzizima, kabla hata Tanganyika haijawaza au hata kufikiria kuwa kuna siku itapata uhuru.

Pia Wamanyema ndio lilikuwa kabila la kwanza la wageni kumiliki maeneo yote muhimu ambayo sasa ndio mjini kama vile Kariakoo, Ilala na Tabata.

Kwa watu wanaoishi au waliowahi kufika Dar es salaam nafikiri mnaufahamu msikiti wa Manyema uliopo katika katika ya mjini yani kariakoo, ule msikiti ulijengwa kabla ya uhuru na hakuna mkoloni yeyote aliethubutu kuugusa kwa vile hata wakoloni walilifahamu vizuri hili kabila, kwamba sio la kulifanyia mzaha hata kidogo.

Kabla mambo ya utandawazi hayajaeneo na kupelekea waha kuvamia miji kwa fujo hasa kwa mkoa wa Dar es salaam, watu wengi walikuwa wanajua kuwa Wamanyema ndio kabila pekee katika mkoa wa Kigoma.

Ila miaka inavyokwenda ndo na mambo yanavyozidi kujiweka wazi yenyewe, na kupelekea watu kujua makabila mengine ya mkoa wa Kigoma.

Wamanyema ni kati ya Makabila yaliopigania uhuru kwa kupambana na wakoloni, huku wakishirikiana na wenyeji wao wa Dar es salaam kama vile Wazaramo, Wandengereko na makabila mengine ya mkoa wa Pwani.

Tabia za wamanyema wake kwa waume ni 1] usafi 2] umaridadi 3]unadhifu. Wamanyema wengi ni maridadi sana kuanzia kwenye swala la mavazi, usafi wa mwili ndani na nje, pia huwa hawajinyimi kula.

Ni vigumu sana kumkuta mmanyema anatembeza mayai, sijui vikapu vya mafuta uzuri na biashara nyingine ndogo ndogo za kuzurula juani, hizi biashara kwa watu wanaotokea Kigoma iwe kwa mkoa wa Kigoma wenyewe, Dar au kwengineko huwa zinafanywa na waha.

Kwa mtu ambae ashawahi kuishi na wamanyema iwe jirani au nyumba moja nafikiri atakuwa amenielewa. Kama una mkeo au mumeo akinaswa na mmanyema tu basi andaa talaka, au kama mwanamke andaa kutalikiwa kabisa, maana mkeo au mumeo ndo umeshamkosa tayari.

Sifa nyingine 4]ubishi 5]kujiamini kupita kiasi. Mmanyema anaweza kutoa hela yake mfukoni akaununua ugomvi wa rafiki yake, na kuanza kupambana kwa niaba yake.

Watu maarufu kutoka katika kabila la Wamanyema ni 1]Sheikh Yahya Husein (aliekuwa mtabiri afrika mashariki) 2] Iddi Faiz Mafongo (aliekuwa mwekahazina wa chama cha TANU) 3] Iddi Tosiri 4] Iddi Simba (huyu mama alikuwa mmanyema, huku baba ni mdengereko) 5] Amri Abedi Karuta (meya wa kwanza jijini Dar) 6] Amani Kabouru (aliekuwa mbunge wa kwanza Kigoma mjini CDM) 7] Diamond 8] Ally Kiba 9] Ommy Dimpoz 10] mh Zitto Kabwe kiongozi wa ACT wazalendo (mbunge mstaafu) 11] Katibu mkuu kiongozi mh balozi Huseein A.
Katanga na wengine wengi serikalini, siasani, kwenye michezo, mziki na fani mbali mbali.

Tatizo kubwa la Wamanyema wa enzi hizo (yani mababu) ilikuwa ni ushirikina. Jambo lililosababisha wamanyema wengi kusambaa katika mikoa mingine hasa Dar es salaam na kujenga huko ili kuwaepuka vigagula hao.

Pia wamanyema hawana ushirikiano kivile katika mambo yanayohusu maisha. Iwe kazini, katika biashara na mambo mengi ya kimaendeleo huwa hawabebani kama yanavyobebana makabila mengine, yani kwa wamanyema kila mtu hubeba msalaba wake mwenyewe.

Kwa kukosa kushirikiano huo ndio maana mababu ambao ndio waliwahi kuwa wamiliki wa maeneo ya Kariakoo, Ilala, Tabata nk walipofariki, wale waliorithishwa maeneo hayo waliyauza yote kwa wahindi (K'koo) waarabu (Ilala) pia maeneo mengi ya Tabata waliorithishwa waliyauza kwa watu mbali mbali.
UZI WA HOVYO KABISA!!!
 
Mlianza wachaga..mkaja wahaya..mkaja wasukuma..juzi mlikua kwa wakinga jana kwa wabena leo wamanyema...sawa ngoja tuone kesho mtahamia wapi.

Sisi wahadzabe tupo zetu maporini huku tunakula matunda na kuwinda digidigi.

#MaendeleoHayanaChama
Ila umesahau kuwaambia kuwa nyani walioko katika mapori yetu ni watamu sana. Ukiwa na asali na matunda mwitu huna hata hamu ya kula hizo kokoto zao.
 
Wamanyema nawaona mamwinyi sana
Waha ndiyo wapambanaji

Ova
 
Back
Top Bottom