Trump Hana options zaidi ya hiyo Tu basi, kutuma vikosi kwenye ardhi ya Iran tena Kwa muda mfupi sana na kufanya kazi Yao na kuondoka then ajitangazie ushindi wa kuondoa kitisho kikuu...
Trump kajiingiza kwenye mtego waliojiingiza wenzake kwenye vita ya Vietnam, unataka kutoka kwenye vita lakini huwezi, Kipindi hichi ni tofauti kidogo maana wenzake waliweza kukaa muda mrefu Vietnam ila yeye hataweza kukaa muda mrefu Iran.
Trump akisema akubaliane na Yale makubaliano yaani points za Iran itakuwa ni ushindi mkubwa Kwa Iran, strategically na kumfanya Iran super power ajaye, kumbuka US anasimamisha vita kwasababu ya joto la mafuta na kuishiwa interceptors then kuna uchaguzi pia...
Trump akisema atoke vitani hivi hivi basi watu hawatamuelewa Kwani Vifo na harakati za hii vita itakuwa ni kazi bure walifanya Hili ni bonge la aibu na anguko, akisema aingie Iran na kukaa muda mrefu watu wengi Sana watafariki ikiwemo US soldiers wa kutosha na Wairani wengi ambapo ndio itazidi kuleta sababu ya Iran kuungana hata kama wengi hawaupendi utawala....
Mwisho kuna Mid-term election ambayo ni ya kuangalia Kwa makini maana wale Democrat hii ni karata Yao kubwa Sana, Aidha waichukue na senate au Congress au Vyote Kwa pamoja itategemea na maamuzi ya Trump.
Netanyahu safari Yake ya US ni kwenda kumfanyia manipulation Trump ili Moto uwake, kumbuka Israel hataki superpower mwingine middle east zaidi Yake, US akicheza vibaya anakwenda kuzalisha superpower middle east then Magiants watakuwa wawili (Iran & Israel) kitu ambacho Israel hataki kitokee maana Kuwa na taifa jingine lenye nguvu ni kutishia au kufuta kabisa ukuu wa Israel middle east...Kumbuka Israel Hana rafiki middle east.