Wamarekani weusi waathirika zaidi na virusi vya Covid19 tofauti na wenye rangi nyeupe

Wamarekani weusi waathirika zaidi na virusi vya Covid19 tofauti na wenye rangi nyeupe

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Raia weusi wa mji wa Chicago ni nusu ya visa vyote vya ugonjwa wa virusi vya corona katika mji huo

Raia weusi wa mji wa Chicago ni nusu ya visa vyote vya ugonjwa wa virusi vya corona katika mji huo
Takwimu kutoka maafisa wa afya mjini Chicago zimeonesha athari kubwa ya virusi vya corona katika Wamarekani weusi.

Raia weusi wa mji wa Chicago ni nusu ya visa vyote vya ugonjwa wa virusi vya corona katika mji huo na zaidi ya asilimia 70 ya vifo vyote , licha ya kwamba idadi yao ni asilimia 30 ya watu wote katika mji huo.

Miji mingine yenye idadi kubwa ya watu weusi ikiwemo Dteroit, Milwaukee , New Orleans na New York pia imetajwa kuwa maeneo yalio hatari.

Marekani imerekodi wagonjwa 370,000 wa virusi hivyo na takriban vifo 11,000. Kote duniani kumekuwa na vifo 75,000 na visa milioni 1.3 kwa jumla.

Je takwimu hizo za Chicago zinaonesha nini?

Kufikia tarehe 5 mwezi Aprili , visa 1,824 vya ugonjwa wa corona kati ya 4,680 vilivyothibitishwa vilihusisha wakaazi weusi, walisema maafisa wa mji huo siku ya Jumatatu.

Hiyo ni tofauti na visa 847 vya weupe, 478 vya Hispanic na 126 vya Wa - Asia wa Chicago. Chicago iliripoti vifo 78 siku ya Jumapili huku asilimia 72 ya vifo hivyo vikihusisha watu weusi.

Utofauti huo unaonekana katika jimbo zima, ambapo watu weusi ni asilimia 41 ya vifo vilivyotokana na Covid-19, licha ya kuwa ni asilimia 14 ya watu wote wa jimbo la Illinois.

Kamishna wa Afya ya Umma wa jiji la Chicago Dkt Allison Arwady amewaambia wanahabari kuwa wakaazi weusi wa jiji hilo tayari wana wastani wa maisha mafupi kwa miaka 8.8 kulinganisha na wazungu.

Meya Lori Lightfoot amesaema kuwa virusi vya corona "vitateketeza Chicago ya watu weusi".

Amesema kuwa wakaguzi wa jiji hilo watatumwa madukani kuhakikisha kila mtu anatekeleza maelekezo ya kujitenga kwa umbali na wengine.

Meya Lightfoot pia ameelezea juu ya uwezekano wa kuwekwa marufuku ya kutoka nje kwa baadhi ya saa katika maeneo ambayo watu hukusanyika kwenye maduka ya pombe, linaripoti gazeti la Chicago Sun-Times.

Taswira ipoje nchi nzima?
Japo virusi vya corona vimepewa jina la "msawazo mkuu ", takwimu zinaonesha kuwa madhara ya maambukizi yanaweza kutofautiana kwa sehemu.

Katika jimbo la Michigan, Wamarekani Weusi ni asilimia 14 ya watu wote, lakini wao ni asilimia 33 ya wagonjwa wa corona na asilimia 41 ya vifo kutokana na ugonjwa huo, zinaonesha takwimu kutoka idara ya afya ya jimbo hilo kufikia jana Jumatatu.

Wazungu katika jimbo hilo ni asilimia 23 ya wagonjwa na vifo vyao ni asilimia 28, kwa mujibu wa takwimu hizo.

d980490dccfe9a47c92fb4b426d33c5f-1

Rais Donald Trump wa Marekani
Jiji la Detroit

katika jimbo la Michigan, lina wakazi weusi takribani asilimia 80, na jiji hilo pekee pamoja na viunga vya karibu yake vina asilimia 80 ya wagonjwa wote wa corona katika jimbo hilo.

Utofauti kama huo pia unaonekana jiji la Milwaukee, jimboni Wisconsin, moja ya maeneo yaliyoathirika zaidi na ubaguzi wa rangi nchini Marekani.

Watu weusi kufikia Ijumaa ya wiki iliyopita wanafikia nusu ya wagonjwa 1,000 na asilimia 81 ya vifo, japo watu weusi ni asilimia 26 tu ya wakaazi wa jiji hilo.

Takribani asilimia 40 ya vifo vitokanavyo na virusi vya corona katika jimbo la Louisiana katika jiji la New Orleans ambako watu weusi ni wengi zaidi.

Maafisa wa Afya hapo awali walieleza kuwa wakaazi wengi wa New Orleans wanakabiliwa na matatizo ya unene wa kupitiliza, kisukari na presha ya kupanda kwa kiwango cha juu zaidi nchini Marekani hali inayowafanya kuwa rahisi kudhurika zaidi na Covid-19.

d980490dccfe9a47c92fb4b426d33c5f-2

Utofauti wa Chicago unachochewa na nini?
Meya Lightfoot anasema kisukari, magonjwa ya moyo na magonjwa ya mfumo wa hewa yapo "kwa kiwango kikubwa" kwenye jamii za weusi.

Dkt Arwady amewaambia waandishi kuwa hata kama kila mtu katika jiji hilo angekuwa na uwezekano wa kumuona daktari, "bado tungeendelea kuona utofauti mkubwa kutokana na upatikanaji haba wa chakula bora na mitaa ya kutembea ".

Dkt Cameron Webb, ambaye ni tabibu mweusi anayewania ubunge katika jimbo la Virginia, ameiambia BBC kuwa tofauti za rangi na kiuchumi zinaoneshwa wazi na janga hili.

"(Janga la corona) linaonesha nyufa za jamii yetu," amesema.

Alderman Jason Ervin, ambaye ni mwenyekiti wa umoja wa wawakilishi weusi katika baraza la jiji la Chicago ameliambia gazeti la Chicago Tribune kuwa "wingi wa watu wasiofuata maagizo ya kujitenga nyumbani katika baadhi ya sehemu za jiji hilo" inawezekana pia ikawa inachangia takwimu hizo.
 
Maafisa wa Afya hapo awali walieleza kuwa wakaazi wengi wa New Orleans wanakabiliwa na matatizo ya unene wa kupitiliza, kisukari na presha ya kupanda kwa kiwango cha juu zaidi nchini Marekani hali inayowafanya kuwa rahisi kudhurika zaidi na Covid-19.

Hiki kipande nilicho bold ni nukuu niliyoitoa hapo kwenye hiyo post yako, ilitakiwa kiwe kichwa cha habari. Vinginevyo unaweza kuwachanganya wadau wakajua kua mwafrika anakufa kwa corona

Mtu kama chris brown, rihana, willsmith nk hao wengi wao wana genes za uzungu na ndo kinacho wakostisha
 
No one is Immune to corona

Sent using Jamii Forums mobile app
Lakini hili limeelezwa kwanini wa Marikani weusi wanakufa zaidi na hili gonjwa uko Chicago kuliko weupe ni sababu ya umasikini..... wanashi wengi sehemu moja pia wanatokatoka nje sana, kwahiyo ni rahisi kusambaza hu ungojwa kwa weusi wenzao pia hawana routine medical check up kwa hiyo miili yao imesha kua dhaifu na maradhi mengine mengi..........tuombe Mungu hili gonjwa lisisambae hapa kwetu natabia zetu hizi za kiswahili, Mungu atakua ametusaliti tu....

Bado logic inakukatalia. Kama weusi ni imara zaidi ya wazungu, kwanini mchanganyiko wa mzungu na mweusi uwe weak kuliko mzungu mwenyewe.
Hapo ilitakiwa mweusi awe strong, afate chotara wa kizungu na kiafrika then afate mzungu au jamii za Asia.
Sasa kwa kesi hii ni kinyume, yani ni sawa na kusema wazungu ni weupe, waafrika ni weusi lakini chotara ni weusi zaidi ya wote hao.

Tokea siku nyingi inajulikana kuwa black Americans wana life expectancy ndogo, wanapata magonjwa ya moyo kuliko wazungu na matatizo kibao. Nilisoma kutoka kitabu cha 'Comparatible worth of Different races'.

Hii inaakisi maisha yetu yalivyo huku, watu ambao waliwahi kuwa na viribatumbo, matege, malnutrition, kwashiorkor na magonjwa ya utotoni kibao siamini kama wanaweza kuwa na kinga za maana. Tuna asili ya kuwa na kinga lakini maisha yetu yanatufanya tuwe very weak.

Lets wait.
 
Stark statistics from Chicago health officials have underscored the heavy toll of coronavirus on black Americans.

Black Chicagoans account for half of all coronavirus cases in the city and more than 70% of deaths, despite making up 30% of the population.

Other cities with large black populations, including Detroit, Milwaukee, New Orleans and New York, have become coronavirus hotspots.

The US has recorded nearly 370,000 virus cases and almost 11,000 deaths.

Globally there have been nearly 75,000 deaths and more than 1.3m cases total.

What do Chicago's statistics show?
As of 5 April, 1,824 out of Chicago's 4,680 confirmed Covid-19 cases were black residents, said city officials on Monday.

That compared with 847 white, 478 Hispanic and 126 Asian Chicagoans.

Chicago has seen a total of 98 deaths as of Sunday, with 72% of them black residents.

The disparity is reflected across the state, where black people account for 41% of Covid-19 deaths, despite making up 14% of the population of Illinois.

Chicago public health commissioner Dr Allison Arwady told reporters that black city residents already lived on average about 8.8 years less than their white counterparts.

Mayor Lori Lightfoot said the coronavirus was "devastating black Chicago".

She said city inspectors would be sent into shops to ensure everyone was adhering to social distancing guidelines.

Mayor Lightfoot also raised the possibility of curfews in areas where people gathered outside liquor stores, reports the Chicago Sun-Times.

Banner image reading 'more about coronavirus'

Banner
What's the picture nationally?
Though the coronavirus has been called the "great equalizer", data suggests that vulnerability to the infection may vary by neighbourhood.

In Michigan, African Americans make up 14% of the population, but they account for 33% of the coronavirus cases and 41% of deaths, figures from the state health department showed on Monday.

White residents account for about 23% of recorded cases in Michigan and 28% of deaths, according to the data.

p088tycz.jpg

Media captionTrump says call with Biden was "really wonderful"
Detroit, Michigan, is about 80% black, and the city together with its surrounding suburbs accounts for around 80% of confirmed coronavirus cases.

A similar disparity has emerged in Milwaukee, Wisconsin, one of the most segregated cities in the US.

African Americans made up almost half of Milwaukee Country's nearly 1,000 cases as of last Friday and 81% of its 27 deaths, despite black people accounting for 26% of the population there, according to a study by ProPublica.

Some 40% of Louisiana's coronavirus deaths have occurred in the New Orleans area, where the majority of residents are black.

Health officials have previously said the Big Easy's residents suffer from rates of obesity, diabetes and hypertension that are higher than the national average, making them more vulnerable to Covid-19.

A woman outside a hospital
Image copyrightREUTERSWhat's behind the disparity in Chicago?
Mayor Lightfoot said diabetes, heart disease and respiratory illness were "really prevalent" in black communities.

Dr Arwady told reporters that even if everyone in the city did have access to a doctor, "we would still see significant health disparities because of food deserts and lack of walkable streets".

p088mh9x.jpg

Media captionCoronavirus: "Pregnancy during a pandemic is terrifying"
Dr Cameron Webb, an African-American physician who is running for Congress in the US state of Virginia, told BBC News that US racial and economic disparities were being amplified by the pandemic.

"It really exposes our society's fault lines," he said.

Alderman Jason Ervin, who chairs Chicago council's black caucus, told the Chicago Tribune that "rates of non-compliance in some parts of the city with the stay-at-home orders" might also be contributing to the statistics.
 
Bado logic inakukatalia. Kama weusi ni imara zaidi ya wazungu, kwanini mchanganyiko wa mzungu na mweusi uwe weak kuliko mzungu mwenyewe.
Hapo ilitakiwa mweusi awe strong, afate chotara wa kizungu na kiafrika then afate mzungu au jamii za Asia.
Sasa kwa kesi hii ni kinyume, yani ni sawa na kusema wazungu ni weupe, waafrika ni weusi lakini chotara ni weusi zaidi ya wote hao.

Tokea siku nyingi inajulikana kuwa black Americans wana life expectancy ndogo, wanapata magonjwa ya moyo kuliko wazungu na matatizo kibao. Nilisoma kutoka kitabu cha 'Comparatible worth of Different races'.

Hii inaakisi maisha yetu yalivyo huku, watu ambao waliwahi kuwa na viribatumbo, matege, malnutrition, kwashiorkor na magonjwa ya utotoni kibao siamini kama wanaweza kuwa na kinga za maana. Tuna asili ya kuwa na kinga lakini maisha yetu yanatufanya tuwe very weak.

Lets wait.
Uimara unafifia pale ambapo genes za uzungu zinakua zipo kwa kiasi kikubwa kuliko genes za u-nigga

Lakini licha hata ya hivyo lakini bado victim waliokufa ni wale wale ambao wanamagonjwa ya ziada

Ifahamike kwamba huu ugonjwa bila kupata assist kutoka kwa ugonjwa mwingine ni ngumu sana kumuua kijana wa kiafrika (sio black america)
 
Lakini hili limeelezwa kwanini wa Marikani weusi wanakufa zaidi na hili gonjwa uko Chicago kuliko weupe ni sababu ya umasikini..... wanashi wengi sehemu moja pia wanatokatoka nje sana, kwahiyo ni rahisi kusambaza hu ungojwa kwa weusi wenzao pia hawana routine medical check up kwa hiyo miili yao imesha kua dhaifu na maradhi mengine mengi..........tuombe Mungu hili gonjwa lisisambae hapa kwetu natabia zetu hizi za kiswahili, Mungu atakua ametusaliti tu....

Sent using Jamii Forums mobile app
Maafisa wa Afya hapo awali walieleza kuwa wakaazi wengi wa New Orleans wanakabiliwa na matatizo ya unene wa kupitiliza, kisukari na presha ya kupanda kwa kiwango cha juu zaidi nchini Marekani hali inayowafanya kuwa rahisi kudhurika zaidi na Covid-19.

hiki kipande ukikielew haiwezi kukupa shida sana kufikiri kua waafrika nao ni wahanga kama wazungu
 
Nafikiri issue sio weusi. Issue ni namna gani una interact na mazingira ili kujenga kinga yako ya mwili.

Black Americans huko Europe na America are of no different to the whites ukiangalia lifestyle zao. Huku Africa mtoto anacheza na vimelea vya magonjwa tangu anatambaa
 
Sure, hii ndio point kubwa, mweusi wa london, newyok, milan, madrid au brussels ambako hata mafua wanayasikia ktk redio tu, malaria haipo kabisa kwan hakunaga mbu uko hawawezi kuwa sawa na sisi.

mimi nina malaria wiki sasa nadunda nayo tu nikiisubiri ihibuke ndo nianze dawa kwan mara nyingi nikinywa sana maji huwa inapotea yenyewe.

Muda mwingi nakua na mafua yakizidi natafuna tangawizi yanasepa tutakuwa nao sawa.

Nakupa mfano tu, aliwai kuja mke wa ashley cole hapa bongo aliugua malaria nusu afe baada ya kuwekwa mpaka ICU pale muhimbili.

Nadhan point yako mkuu ni ya kweli sana
Nafikiri issue sio weusi. Issue ni namna gani una interact na mazingira ili kujenga kinga yako ya mwili. Black Americans huko Europe na America are of no different to the whites ukiangalia lifestyle zao. Huku Africa mtoto anacheza na vimelea vya magonjwa tangu anatambaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nafikiri issue sio weusi. Issue ni namna gani una interact na mazingira ili kujenga kinga yako ya mwili. Black Americans huko Europe na America are of no different to the whites ukiangalia lifestyle zao. Huku Africa mtoto anacheza na vimelea vya magonjwa tangu anatambaa
Seconded.
 
Back
Top Bottom