Wamarekani weusi waathirika zaidi na virusi vya Covid19 tofauti na wenye rangi nyeupe

Wamarekani weusi waathirika zaidi na virusi vya Covid19 tofauti na wenye rangi nyeupe

'Ulizia Russia, saudia, Iran, nk mweusi hata uenyekiti wa mtaa Urusi au Saudia hawezi kupata. '

Hio sentensi hapo juu si ya kweli, kuna jamaa anaitwa Jean Gregoire Sagbo, ni mzaliwa za Benin na ni councilor of Novozavidovo huko Urussi.
Ni mmoja tu siyo? Taja mwengine
 
Wamarekani weusi wengi ni masikini ndio maana wengi wameathirika na Corona
Raia weusi wa mji wa Chicago ni nusu ya visa vyote vya ugonjwa wa virusi vya corona katika mji huo

Raia weusi wa mji wa Chicago ni nusu ya visa vyote vya ugonjwa wa virusi vya corona katika mji huo
Takwimu kutoka maafisa wa afya mjini Chicago zimeonesha athari kubwa ya virusi vya corona katika Wamarekani weusi.

Raia weusi wa mji wa Chicago ni nusu ya visa vyote vya ugonjwa wa virusi vya corona katika mji huo na zaidi ya asilimia 70 ya vifo vyote , licha ya kwamba idadi yao ni asilimia 30 ya watu wote katika mji huo.





Miji mingine yenye idadi kubwa ya watu weusi ikiwemo Dteroit, Milwaukee , New Orleans na New York pia imetajwa kuwa maeneo yalio hatari.

Marekani imerekodi wagonjwa 370,000 wa virusi hivyo na takriban vifo 11,000. Kote duniani kumekuwa na vifo 75,000 na visa milioni 1.3 kwa jumla.

Je takwimu hizo za Chicago zinaonesha nini?

Kufikia tarehe 5 mwezi Aprili , visa 1,824 vya ugonjwa wa corona kati ya 4,680 vilivyothibitishwa vilihusisha wakaazi weusi, walisema maafisa wa mji huo siku ya Jumatatu.

Hiyo ni tofauti na visa 847 vya weupe, 478 vya Hispanic na 126 vya Wa - Asia wa Chicago. Chicago iliripoti vifo 78 siku ya Jumapili huku asilimia 72 ya vifo hivyo vikihusisha watu weusi.

Utofauti huo unaonekana katika jimbo zima, ambapo watu weusi ni asilimia 41 ya vifo vilivyotokana na Covid-19, licha ya kuwa ni asilimia 14 ya watu wote wa jimbo la Illinois.

Kamishna wa Afya ya Umma wa jiji la Chicago Dkt Allison Arwady amewaambia wanahabari kuwa wakaazi weusi wa jiji hilo tayari wana wastani wa maisha mafupi kwa miaka 8.8 kulinganisha na wazungu.

Meya Lori Lightfoot amesaema kuwa virusi vya corona "vitateketeza Chicago ya watu weusi".

Amesema kuwa wakaguzi wa jiji hilo watatumwa madukani kuhakikisha kila mtu anatekeleza maelekezo ya kujitenga kwa umbali na wengine.

Meya Lightfoot pia ameelezea juu ya uwezekano wa kuwekwa marufuku ya kutoka nje kwa baadhi ya saa katika maeneo ambayo watu hukusanyika kwenye maduka ya pombe, linaripoti gazeti la Chicago Sun-Times.

Taswira ipoje nchi nzima?
Japo virusi vya corona vimepewa jina la "msawazo mkuu ", takwimu zinaonesha kuwa madhara ya maambukizi yanaweza kutofautiana kwa sehemu.

Katika jimbo la Michigan, Wamarekani Weusi ni asilimia 14 ya watu wote, lakini wao ni asilimia 33 ya wagonjwa wa corona na asilimia 41 ya vifo kutokana na ugonjwa huo, zinaonesha takwimu kutoka idara ya afya ya jimbo hilo kufikia jana Jumatatu.

Wazungu katika jimbo hilo ni asilimia 23 ya wagonjwa na vifo vyao ni asilimia 28, kwa mujibu wa takwimu hizo.

d980490dccfe9a47c92fb4b426d33c5f-1

Rais Donald Trump wa Marekani
Jiji la Detroit

katika jimbo la Michigan, lina wakazi weusi takribani asilimia 80, na jiji hilo pekee pamoja na viunga vya karibu yake vina asilimia 80 ya wagonjwa wote wa corona katika jimbo hilo.

Utofauti kama huo pia unaonekana jiji la Milwaukee, jimboni Wisconsin, moja ya maeneo yaliyoathirika zaidi na ubaguzi wa rangi nchini Marekani.

Watu weusi kufikia Ijumaa ya wiki iliyopita wanafikia nusu ya wagonjwa 1,000 na asilimia 81 ya vifo, japo watu weusi ni asilimia 26 tu ya wakaazi wa jiji hilo.

Takribani asilimia 40 ya vifo vitokanavyo na virusi vya corona katika jimbo la Louisiana katika jiji la New Orleans ambako watu weusi ni wengi zaidi.

Maafisa wa Afya hapo awali walieleza kuwa wakaazi wengi wa New Orleans wanakabiliwa na matatizo ya unene wa kupitiliza, kisukari na presha ya kupanda kwa kiwango cha juu zaidi nchini Marekani hali inayowafanya kuwa rahisi kudhurika zaidi na Covid-19.

d980490dccfe9a47c92fb4b426d33c5f-2

Utofauti wa Chicago unachochewa na nini?
Meya Lightfoot anasema kisukari, magonjwa ya moyo na magonjwa ya mfumo wa hewa yapo "kwa kiwango kikubwa" kwenye jamii za weusi.

Dkt Arwady amewaambia waandishi kuwa hata kama kila mtu katika jiji hilo angekuwa na uwezekano wa kumuona daktari, "bado tungeendelea kuona utofauti mkubwa kutokana na upatikanaji haba wa chakula bora na mitaa ya kutembea ".

Dkt Cameron Webb, ambaye ni tabibu mweusi anayewania ubunge katika jimbo la Virginia, ameiambia BBC kuwa tofauti za rangi na kiuchumi zinaoneshwa wazi na janga hili.

"(Janga la corona) linaonesha nyufa za jamii yetu," amesema.

Alderman Jason Ervin, ambaye ni mwenyekiti wa umoja wa wawakilishi weusi katika baraza la jiji la Chicago ameliambia gazeti la Chicago Tribune kuwa "wingi wa watu wasiofuata maagizo ya kujitenga nyumbani katika baadhi ya sehemu za jiji hilo" inawezekana pia ikawa inachangia takwimu hizo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
$60m, vipande vya dhahabu, nk
Hahah balozi mstaafu wa TZ wa nchini Russia alisema Wkt inshu ya dr.Shika inatokea Russia yeye alikua ni balozi kule,kilichotokea Shika alienda kusoma kule then akawa anaji-bragg ana mabilioni,ma-viwanda warussi wakamteka wakamkata kidole alivyofanikiwa kutoroka ndipo ubalozi ukamsaidia huyo shika kumlipia tiketi kurudi bongo.

Kwa hio alibebaje hizo $60mil kuwapelekea hao mafiasi?mnaijua lkn $60mil?

Mmiliki wa $60mil yuko sa hivi analala chini hapa bongo.
 
Hata ujumbe wa chama cha ushirika hawapati[emoji14][emoji14]
Ulizia Russia, saudia, Iran, nk mweusi hata uenyekiti wa mtaa Urusi au Saudia hawezi kupata. '

Hahah
 
Maafisa wa Afya hapo awali walieleza kuwa wakaazi wengi wa New Orleans wanakabiliwa na matatizo ya unene wa kupitiliza, kisukari na presha ya kupanda kwa kiwango cha juu zaidi nchini Marekani hali inayowafanya kuwa rahisi kudhurika zaidi na Covid-19.

Hiki kipande nilicho bold ni nukuu niliyoitoa hapo kwenye hiyo post yako, ilitakiwa kiwe kichwa cha habari. Vinginevyo unaweza kuwachanganya wadau wakajua kua mwafrika anakufa kwa corona

Mtu kama chris brown, rihana, willsmith nk hao wengi wao wana genes za uzungu na ndo kinacho wakostisha
Waafrika tunajibagua wenyewe...


Kinachofanya waafrika tusife kwa wingi ni muingiliano mdogo baina yetu... Fikiria ni watu wangapi unawajua huwa ni wasafiri wa kwenda nje ya nchi hapo utapata jibu, ili maradhi yasambae kwa nchi za Afrika yanahitaji muda mrefu kutokana na muingiliano mdogo tofauti na nchi zilizo endelea...

Tusijipe moyo kwamba muafrika haumwi... Binadamu wote ni sawa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Trevor Noah kaeleza viruzi kwanini wanugu wamepigwa zaidi na hili janga.

 
Lakini hili limeelezwa kwanini wa Marikani weusi wanakufa zaidi na hili gonjwa uko Chicago kuliko weupe ni sababu ya umasikini..... wanashi wengi sehemu moja pia wanatokatoka nje sana, kwahiyo ni rahisi kusambaza hu ungojwa kwa weusi wenzao pia hawana routine medical check up kwa hiyo miili yao imesha kua dhaifu na maradhi mengine mengi..........tuombe Mungu hili gonjwa lisisambae hapa kwetu natabia zetu hizi za kiswahili, Mungu atakua ametusaliti tu....

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa si wanakufa kwa Corona sababu ya umasikini, kuna uwezo wa mwafrika masikini aliyepo Africa kupona kweli?
 
Watu weusi waliamini kuwa huyu corona anaua wazungu zaidi,,, nadhani sasa hawakuwa makini kuchukua tahadhari kama tu ambavyo waafrika wengi hivi sasa bado wanapuuzia kuhusu kufuata njia za kujikinga.

Lakini najaribu kufikiria kuwa huu ugonjwa unawapa support ma'racist kufanya vitu vyao.

TUFANYE BIDII KUJIKINGA

Sent using Jamii Forums mobile app
 


Coronavirus Killing A Lot Of Blacks In The U.S
 
Hahah balozi mstaafu wa TZ wa nchini Russia alisema Wkt inshu ya dr.Shika inatokea Russia yeye alikua ni balozi kule,kilichotokea Shika alienda kusoma kule then akawa anaji-bragg ana mabilioni,ma-viwanda warussi wakamteka wakamkata kidole alivyofanikiwa kutoroka ndipo ubalozi ukamsaidia huyo shika kumlipia tiketi kurudi bongo.

Kwa hio alibebaje hizo $60mil kuwapelekea hao mafiasi?mnaijua lkn $60mil?

Mmiliki wa $60mil yuko sa hivi analala chini hapa bongo.
Warusi walimtapeli ndo maana analala chini
 
Marekani ni nchi ambayo kuna rangi 2 tu za binadamu..white & black...hakuna coloured, half-caste anayetambulika kama sijui mixed race, sijui nini...Arabs ni black...Indians ni black...Asians siyo white..
Sasa kundi hili la blacks nalo linajibagua ipasavyo, hispanics, Mexicans, Carribeans, African-American, Arabs, mvurugano mtupu..

Everyday is Saturday.................... 😎
 
Uimara unafifia pale ambapo genes za uzungu zinakua zipo kwa kiasi kikubwa kuliko genes za u-nigga

Lakini licha hata ya hivyo lakini bado victim waliokufa ni wale wale ambao wanamagonjwa ya ziada

Ifahamike kwamba huu ugonjwa bila kupata assist kutoka kwa ugonjwa mwingine ni ngumu sana kumuua kijana wa kiafrika (sio black america)
Nachukia sana ninapomuona mtu anaongea kwa hisia zake kama wewe na kutaka kuwaaminisha watu. Huu ni uongo uliokomaa na umejikita katika hisia zako binafsi. Tupe vyanzo vya kitafiti vinavyothibitisha haya unayoyasema, vinginevyo ni uongo na kujijazia matumaini hewa.
 
Back
Top Bottom