Uchaguzi 2020 Wamasai wamemuelewa Tundu Lissu

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
15,101
Reaction score
56,054
Kama ilivyo ada, mheshimiwa Lissu ameamua kuwafuata wananchi kule waliko na kusemezana nao.

Jana alipita katika eneo la Ngorongoro na kuongea na wamasai, Mheshimiwa Lissu akazungumza nao kuhusu madhila wanayoyapata katika hifadhi hiyo na namna atakavyoyashughulikia pindi akiwa Rais. Akawakumbusha historia ya hifadhi hiyo na sacrifice ambayo wamasai walifanya ili kufanikisha uanzishwaji wa hifadhi hiyo.

Kwa mujibu wa lugha ya Kimwili na muitikio chanya wa Wakazi hao ni dhahiri Lissu amepata uungwaji mkono wa Wamasai.

Wakati huohuo akipita njiani Lissu amepokea baraka za wazee wa kimasai.

Tazama video hii:

Your browser is not able to display this video.


Lissu akipokea baraka



Lissu akicheka na kufurahi na wananchi


 
Hongera sana Lisu. Pita kila mahali utakapoweza na muda ukaruhusu. Hata penye watu 100, usipadharau. Maneno mawili, dakika 2 zinatosha.

Watanzania baada ya kuongozwa kikatili, wanahitaji faraja. Watu wapewe matumaini, waambiwe na wathibitishiwe kuwa hii ni nchi yao ambayo wana mamlaka nayo. Hata tukitofautiana vipi, haki ya umiliki wa Taifa letu, kwa kila mmoja, ni sawa.

Tofautiana na wale wapu.mbavu ambao ukitofautiana tu kifikra, utawasikia, Magufuli ndiyo Rais, kama hutaki, hama nchi! Mtu ahame nchi kwa sababu tu umetofautiana naye kifikra? Pumbaf kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kujitekenya
Kucheka
Kula
Kuingia mitandaoni kudanganyaaaaa kisha
Kujipa matumaini
Kulala
October 28 kwani mbalii!!
Tukutane sanduku la kura

Mnafungua thread nyingi za kujipa moyo huku mkisahau waTZ si wajinga kiasi hicho hasa kipindi hichi Cha kampeni.

Yake mlotuaminisha miaka nenda Rudi kwa Sasa mnakana Kila Kona.
Sijui ilani yenu imeandikwa nn Sasa kama yote mazuri mnayakataaa.
 

Ebu tazama hapo umati ambao Lissu akiona njiani anapunguza speed wamshangilie na vipicha vitaletwa JF Lissu sijui keshashinda; upande wa pili awasimami kama wanataka kumsikiliza Magufuli waende uwanjani.

Magufuli kusubiriwa njiani ni kawaida sana tena na watu wengi kushinda wanaoudhuria mikutano ya Lissu kwenye viwanja vyake.
 
Hakika.
 
Daah huyu mwamba anaijua hii nchi vizuri aisee dah.historia yote iko kichwani nimemkubali,vichwa adhimu hapa Tanzania kuwahi kutokea..
,[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]eti anajua nchi ,kama anaijua nchi asingepotea katavi.
 
,[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]eti anajua nchi ,kama anaijua nchi asingepotea katavi.
Kwa akili yako ukisikia mtu anaijua Nchi unadhani kuwa anafahamu njia,mitaa na vitongoji vyote vya kila sehemu? Kweli Pole Pole Chakubanga sijui kawatoa wapi nyie zero.
 
Huyu jamaa anafuja hela za walipa kodi. Msafara mkubwa sana huu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…