Jamani eh.
Hebu niambieni mtajisikiaje Wazanzibari kesho kuwa mwiko kupika au kula rojo....haijalishi
Wazaramo watajisikiaje kusikia kuwa kesho ni mwiko kucheza ngoma ya mdundiko na lazima waka surrender ngoma zao na zana zingine za jadi yao?
Narudi Zanzibar, mtajisikiaje kesho mkiambiwa muache kuvaa kanzu, makobazi na kula supu la pweza, ati, vinahatarisha usalama wa wengine?
Utajisikia vipi ukiambiwa uache utambulisho wako, urithi wako, mtindo wako wa maisha? Waweza kuacha kula rojo? Waweza kuacha mdundiko, waweza kuacha kuvaa makobazi na kanzu.
Sasa, hayo ndiyo yanayowakumba Wamaasai leo.
Wanalazimishwa kuacha Utamaduni wao wa muda mrefu, desturi ya kubeba rungu na sime, vitu ambavyo vimekuwa ndio utambulisho wao. Utambulisho unaoonyesha ujasiri wao na ujuzi wa vita..
Zana hizi zimekuwa muhimu maishani mwao, kama wafugaji na Warriors kwa karne na karne.
Wamelinda ardhi yao, bahati mbaya wameshindwa safari hii, lakini wamekuwa wakijilinda na kulinda mifugo yao na heshima(dignity) yao for S.A.W sake! for centuries.
Wamerithishana kwa vizazi na vizazi kama tambiko na heshima kwa vijana baada ya kubalehe, sasa wanaambiwa wakavisalimishe! wawe kama Wazungu, wapoteze utambulisho(uniqueness) wao/yao.
Suala hili haliko sawa kabisaaa, na Sikubaliani nalo, huu sio Ubinadamu sio Uislamu, sio Ukristo, sio Ushetani, sio uwekezaji- its GENOCIDE
Namalizia
NB:Sasa unaweza kufikiri haya yanasikitisha, la hasha.
Yanayosikitisha zaidi, mbali na CCM ambaye ndie muuaji, ni CHADEMA, chama ambacho kinajinadi, kinadai haki. Wako kimya sana? Unayoyasikia ni haki yao ya kuja kuendesha ma V8 na kurusha helikopta.
Sera zenu zinasema nini kuhusu hawa ndugu zetu Wamaasai?
Mtawarudisha Loliondo au na nyie ndio mje muwamalize muwavue na nguo zao za jadi?
STOP THE GENOCIDE