Wamasai wanakwenda kuua misaada ya UN na EU kwa Tanzania; Ngorongoro imetugeuka vibaya

Wamasai wanakwenda kuua misaada ya UN na EU kwa Tanzania; Ngorongoro imetugeuka vibaya

Mbinyo (pressure) lazima uendelee hadi serikali ya CCM itapoacha hila zake zote ovu kwa raia kufurushwa pia kuburuza miguu kukataa katiba mpya ambayo hakika ndiyo msingi wa Uhuru, Haki na Maendeleo ya watu

Uhuru
wa kuipeleka mahakamani serikali, haki ya raia mmoja mmoja kumiliki ardhi bila kutwaliwa au kufurushwa na hapo ndipo maendeleo ya kweli kwa wananchi yatapatikana .
 
Its a multpolar world...Tanzania is a NAM Nation.
 
Correction....wazungu wanawapenda watanzania kuliko serikali iliyolaaniwa ya CCM na wafuasi wake wanavyowapenda watanzania....nje ya CCM tunapendana sana ndugu yangu
 
Tulikosa misaada wakati wa JPM na tuliishi acha roho ya kimaskini wewe misaada misaada mtaacha lini utegenezi? Tusihifadhi maliasili na uoto wetu eti kisa misaada? Amkeni Watanzania,hiyo misaada mpaka Leo imekusaidia nini?
 
Mkiendekeza misaada, mikopo na uwekezaji wa wazungu mtabaki watumwa siku zote.
Hawataki mjenge bwawa la ml Nyerere huku kwenu kuna shida kubwa ya umeme.
Hawataki mtoe gesi yenu mliogundua ambayo itanyanyua uchumi weni kwa sababu eti inachafua mazingira. Huku wao ndio wachafuaji wakubwa wa mazingira
Hawataki nyie kupinga mashoga, ni lazima muwe na muwasaidie mashoga kwenye jamii zenu. Museveni kisha wekewa vikwazo.
Hawataki nyie muamuae matumizi ya raslimali zenu kwa njia mnayo ona inafaa, ni lazima wao ndio wawape ruhusa.

Tanzania ni nchi tajiri, ina wasomi, ila inabidi kujiamini na kuwapiga chini wote wanaotuangusha kwenye uongozi
 
Maamuzi ya bunge la Ulaya kuhusu kuhamisha Wamasai Ngorongoro linakwenda kutaathiri kiuchumi. Tutaathirika kwa sababu tulitumia nguvu huku tukijua kabisa kwamba tunajipanga kuimarisha mahusiano na mataifa mengine.

Bunge la Ulaya kwa zaidi ya asilimia 90 limesema maamuzi ya Tanzania siyo sahihi. Means wazungu wanawapenda Watanzania kuliko sisi tunavyojipenda. Wazungu ni waasisi wa maliasili ,walitunga sheria na kanuni zote za kulinda rasilimali. Wamesema Wamasai ni ASILI na kwamba hakuna kinachoweza kufuta asili yao ngorongoro.

Tunatokaje hapa? Tunawezaje kukwepa athari za kiuchumi pale watakapoamua kulimalia hii hoja? Tujadiliane
Kama sisi wenyewe hatuna akili za kujiamria mambo kama nchi, unatarajia hao wengine huko nje watafanya nini? Watatuamria.

Bunge letu ndilo lililopashwa kufanya uamzi bila ya mizengwe, kama Bunge linabadilishwa na kuwa chombo cha kutumiwa tu na chama tutawalaumu vipi watu wa nje wakituamria yanayotufaa sisi.

Ni aibu, lakini inabidi tuivumilie hiyo aibu na tuwashukuru hao watu kuwakumbusha viongozi wetu kwa niaba yetu.

Sipendezwi kamwe na hali hii, lakini nafurahia hatua ya kuwaonyesha CCM kwamba ukichaa wao huko nje hawautambui.
 
Maamuzi ya bunge la Ulaya kuhusu kuhamisha Wamasai Ngorongoro linakwenda kutaathiri kiuchumi. Tutaathirika kwa sababu tulitumia nguvu huku tukijua kabisa kwamba tunajipanga kuimarisha mahusiano na mataifa mengine.

Bunge la Ulaya kwa zaidi ya asilimia 90 limesema maamuzi ya Tanzania siyo sahihi. Means wazungu wanawapenda Watanzania kuliko sisi tunavyojipenda. Wazungu ni waasisi wa maliasili ,walitunga sheria na kanuni zote za kulinda rasilimali. Wamesema Wamasai ni ASILI na kwamba hakuna kinachoweza kufuta asili yao ngorongoro.

Tunatokaje hapa? Tunawezaje kukwepa athari za kiuchumi pale watakapoamua kulimalia hii hoja? Tujadiliane
Unadhani wenzio wanajali basi?
 
Wazungu wana mchango mkubwa sisi kuwa kwenye huu umaskini. Sio watu wa kuwaamini hata kidogo. Kuhusu Ngorongoro ilikuwa suala la muda tu kuwaondoa. Kwa idadi ya watu waliopo na maendeleo ya binadamu ile Ngorongoro ingekuja kupotea ndani ya miaka michache. Sisi tunawaogopa wanyama ila wanyama wanatuogopa sisi kuliko tunavyodhani. Binadamu wakihamia sehemu ya wanyama automatically wanyama lazima wahame na kupotea kabisa. Shughuli za binadamu ni adui mkubwa wa maisha ya wanyama. Ngorongoro kulishaanza kujengwa nyumba za ghorofa kitu ambacho kinahatarisha mazingira ya hifadhi. Ikumbukwe serikali ilishahamisha wafanyakazi wote NCAA waliokuwa wanaishi ndani ya hifadhi kwa kuwajengea makazi Karatu. Zamani kama unaenda Ngorongoro ukishatoka kidogo tu nje ya Arusha kuanzia maeneo ya Kisongo utaanza kuona mbuni, swala, twiga, pundamilia na wanyama wengine mida ya mchana lakini kutokana na shughuli za binadamu kwa sasa ni ngumu kuwaona hasa mbuni.
 
Kati ya maamuzi ya kifedhuli yaliyowahi kufanyika na awamu ya sita ni haya.

Huyo wanayemuita mama hana moyo wa huruma hata kidogo.

Ngoja wanyooshwe kwanza na hao wanaojaribu kila siku kujipendekeza kwao.
 
Pamoja na mimi kutounga mkono yaliyofanyika Loliondo Lakini Sio kila maamuzi ya nchi za kiafrika kwamba lazima yawafurahishe wazungu.Hao ni wanafiki watupu.
Sababu rasmi sio kuwapenda Wamasai bali ni kwa sababu kule anapewa hasimu wao mkuu ambaye ni Mwarabu.

Lakini pia wengi wetu humu mnachangia kishabiki zaidi ya uhalisia.
Tena wengi wenu mnatumia taarifa za wanaharakati kuliko uhalisia ulivyo.Ili kuulinda utalii na kipato chake nchini.Ilikuwa ni lazima wamasai wapunguzwe pamoja na mifugo yao inayoongezeka kuliko eneo husika.

Na kingine ni siasa uchwara za upinzani wa kitanzania.
Hiyo ndio kazi ya Tundu Lissu anayoifanya kila anapokwenda huko kwa wafadhili wake wakuu.
Umeelewa ulichoandika hapa mkuu? UNAUNGA MKONO WAMASAI KUHAMISHWA AU HUUNGI MKONO?

Nyie CCM mna taabu Sana. Unaunga mkono hoja alafu unaichambua weeeeee kwa kui dis!
 

MRG welcomes outcomes of the recent African Commission mission to Tanzania​

STATEMENTS | 2023

Minority Rights Group International (MRG) welcomes recent recommendations from the African Commission on Human and Peoples’ Rights (ACHPR), concerning the government of Tanzania’s systematic use of multi-pronged approaches to deny Maasai their rights to their ancestral land in the name of conservation. Years of forced evictions and the destruction of property have recently evolved into a direct attack on the livelihoods of the indigenous Maasai community that amounts to forced displacement.
Following its Promotion Mission, the ACHPR recommends that Tanzania implements several international and regional human rights instruments that would protect Maasai rights; protect human rights defenders; ensure that conservation efforts are conducted with the participation of Maasai; and address the depreciation of essential amenities in the area.
MRG shares the concerns raised by the Mission concerning the eviction of the Maasai community from the Ngorongoro Conservation Area. MRG calls upon the government of Tanzania to cease all measures undertaken to render Maasai ancestral lands uninhabitable by restricting and, in some cases, totally withholding, social and economic amenities key to the very survival of the community, such as emergency medical care.
The government of Tanzania must fully implement the Mission’s recommendations and take urgent steps to ensure that Maasai rights over their ancestrally owned land are enforced. MRG also urges Tanzania to uphold the internationally recognized right of indigenous peoples to free, prior and informed consent, and to allow Maasai to participate fully and equally in government meetings and decisions concerning their ancestral lands.
MRG reiterates that the safeguarding of indigenous peoples’ rights, including their land tenure rights, remains the cornerstone of any sustainable conservation ventures.
Further, MRG is deeply disappointed by the ruling delivered by the East African Court of Justice in September 2022, that Maasai appellants had not been evicted from their ancestral land. This ruling goes against the precedence set by the African Court on Human and Peoples’ Rights in the historic Ogiek ruling of 2017 and its subsequent reparations decision of June 2022. It similarly goes against the recommendation of the ACHPR in the Endorois case.
Both these rulings have set precedence at a regional level on the recognition and protection of the rights of indigenous communities to their ancestral lands, as well as their rights to religious practice, property, culture and the free disposition of natural resources and development. Tanzania should pay attention to this precedence.
The ruling delivered by the East African Court of Justice has been a setback for Maasai and all indigenous peoples across Africa, whose rights are increasingly violated in the name of conservation. More detrimentally still, it has in fact legitimized the human rights violations to which the government of Tanzania continues to subject the Maasai community.
The rights of ethnic minorities and indigenous peoples in Tanzania are continuously undermined because of both weak domestic legislation and the failure of domestic legal mechanisms to protect such rights. Currently, owing to a lack of constitutional protection of land rights, Tanzania does not have the legislative framework needed to meet its obligations under Articles 21 and 22 of the African Charter on Human and Peoples’ Rights, which safeguard the land rights and rights to economic, social and cultural development of all peoples
 
Watunyime kila kitu mpaka tukome.
Mtetezi wa agenda za kifaragha naona atakuwa ameenda kuichomea nchi utambi, unajua ushoga unaharibu sana akili, ukishatumbukia humo na akili huwa zinahama mazima! Hafahamu kuwa kuzaliana kwa wingi kwa masai mbugani na ujenzi kulikuwa ni tishio kwa wanyamapori!
 
Back
Top Bottom