Wamasai wanakwenda kuua misaada ya UN na EU kwa Tanzania; Ngorongoro imetugeuka vibaya

Wamasai wana kosa gani? Ma CCM ndo yamefukuza wamasai Sasa ulitaka wakatae kuhama wauawe?
Laumu serikali kwa kuuza ngorongoro.
 
Mungu wabariki Wazungu
Ndiyo shida yenu hii, mmekuwa makuwadi wa wazungu. Siku mkichukua nchi sisi sijui tutakuwa wageni wa nani...HamqeI kusimama kama ninyi bila.mzunhu nyuma yenu?
 
Sasa kama washauri wa siasa wa Mama Kizimkazi ni akina Petro Magoti unategemea nini?
Samia ameanza kuharibu Uchumi wa raia mmojammoja na akiachwa ataharibu sana mbele ya safari!
Mara ooh,anafungua nchi,kwani ni lini Tanzania ilifungwa kwa Wageni kuja!


Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Huu ulikuwa unyanyasaji mkubwa sana. Watu wameishi hapo miaka yote, unakuja kuwatoa ghafla na kutaka waanze maisha mengine ambayo sio asili yao.

Ngoja tuone, ila naunga mkono uamuzi huo.
Bado kuna sekeseke la kule Ruaha National Park Wananchi wamefanyiwa vitendo vya kikatili kuhamishwa na kubakwa juu.World Bank wamemng'ang'ania Mama Kizimkazi na serikali yake!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Jamaa unapenda sana ligi..umeamua kutoka hadi nje ya mada..
Kupenda au kutopenda ligi si issue. Hata baadhi ya maendeleo makubwa ya kisayansi yameletwa kwa mashindano.

Issue ni, kilichoandikwa ni kweli au si kweli?

Kiukweli, Tanzania kupenda ligi si tatizo, tatizo watu wengi hawapendi kujadiliana kwa ligi iliyo fact based na yenye research iliyo na attention to detail.

Hujaweza kukanusha kilichoandikwa. Umefanya logical fallacy moja inaitwa ad hominem attack.

Ad Hominem attack ni kuacha kujadili hoja iliyotolewa na mtu, na kumshambulia mtu mwenyewe.

Ni shambulio linalotumiwa na watu wasio na hoja kuondoka kwenye mazungumzo ya hoja na kwenda kwenye mazungumzo ya kumshambulia mtu binafsi, kwa sababu ya chuki, ujinga, kukosa hoja etc.

Kuhusu kutoka nje ya mada, ni wazi ukioneshwa mada hii hapa huwezi kuichambua, pengine huwezi hata kuitambua, na huelewi maana ya open forum kama JF. Huelewi maana ya kaulimbiu ya "Where We Dare To Talk Openly".

Ukitaja chochote JF, unaruhusu watu kukihoji.

Tunaweza kuendelea kujadiliana mada ya msingi, na hapo hapo tukasahihishana kwenye mada nyingine zinazojitokeza. Si lazima tukubaliane kwenye kila kitu.

We can chew gum and walk. We can reject premises. We do not have to agree on everything for fear of being labelled "wapenda ligi".

Ndiyo maana, jibu langu kwa mtoa mada limeanza kwa kusema kuwa nakubaliana naye kwa mambo mengi aliyoandika. Maana yake, kimsingi simpingi, nimeona kuna hii habari moja tu haijakaa sawa, natoa habari ambayo nafikiri itaiweka hii habari ya wazungu kuwa waasisi wa kutetea maliasili, rasilimali, mazingira vizuri zaidi.

Mtoa mada alitaja hiyo hoja niliyoihoji na kuipinga, sikuileta hapa out of thin air.

Kuna watu wanaamini kuwa wazungu ndio walioanzisha uanamazingira, wakati Afrika tulikuwa na tuna mpaka dini za kuheshimu mazingira, na Wazungu ndio watu walioharibu mazingira kwa kiasi kikubwa sana, ndiyo kwanza wanaamka kwenye mambo ya kutunza mazingira.

Kuna jamaa alikuwa anasimulia alikuwa katika team ya kupanua bandari ya Dar miaka ya 1970s, akaingia kwenye shamba la mzee mmoja akimuelezea mpango wa serikali wa kupanua bandari. Yule mzee mwenye shamba akamwambia jamaa kuwa hawezi kuruhusu upanuzi wa bandari kwa sababu hii miti ni mungu kwake, anafanya ibada za asili hapo, haruhusu miti ikatwe.

Muandishi nguli aliyeshinda nishani ya Pulitzer, Jared Diamond, ameandika kitabu kizima kinachoangazia mambo haya, kinaitwa "The World Until Yesterday: What Can We Learn From Traditional Societies?".

Ubaya ni kwamba na sisi siku hizi tumeambukizwa systems za wazungu, mtu akiangalia historia fupi anaona wao ndio wanatufundisha sisi kutunza mazingira, kitu ambacho ukiangalia historia vizuri utaona si kweli. Muafrika akikataza kukata miti anaitwa mpagani mshenzi, Mzungu akikataza kukata miti anaitwa mwanamazingira.

Hujaigusia kabisa hii hoja, na pengine hujaweza hata kuitambua na kuielewa hii hoja.

Umerukia kumshambulia mtoa hoja, ad hominem attack.

Sasa, kwa tabia yako ya kuacha kujadili hoja na kumshambulia mtoa hoja, ad hominem attack yako, wewe ndiye umekuwa mpenda ligi, bila hata kutetea ukweli, na kwa kutoka nje ya hoja.

Umefanya kitu kinachoitwa "psychological projection". Mashuzi ya kuendekeza ligi za kutoka nje ya hoja kwa logical fallacy ya ad hominem attack umejamba wewe, lawama unanipa mimi.

Waswahili walisema, "Nyani haoni kundule".
 
Hakuna mtu anapenda kuhamishwa makazi yake aliyozoea. Wamasai lazima wapambanie kubaki.
Je nini kifanyike? Wamasai waachwe waendelee kuishi hifadhi ya Ngorongoro?
Kwa takwimu za kuongezeka kwa watu na kuongezeka kwa mifugo baada ya miaka 10 ngorongoro itabaki? Kumbuka wanaoongoza kwa uharibifu wa mazingira ni wafugaji.
Harafu tusiwe na perspective ya kirofa kuwa kuwaondoa wamasai Ngorongoro ni kujali nyati kuliko watu.
Serikali makini haiwezi kufanya maamuzi kwa kuangalia masilahi ya kundi moja la watu tu, yanaangaliwa pia maslahi mapana na nchi.
Ukisema uangalie kila mtu anataka nini huwezi fanya kitu, sisi wanadamu ni wabinafsi sana.
Njia ya kuwaondoa wamasai pale labda inaweza ikawa sio njia nzuri ila wamasai lazima wangehamishwa tu kuokoa hifadhi ya Ngorongoro.
 
Huna lolote..we unakili kuliko watangulizi wako wote..seriakli msitumie hoja za kisiasa kuharibu maisha na kupora haki ya wamaasai kwa maslahi binafsi ..swali la msingi kama wameweza kuishi zaidi ya miaka 2000 huko na hakujawahi kutokea tatizo la kuuwa wanyama na kuharibu mazingira..maana yake ni ni hoja na kigandamizaji kwa haki..hivi utamtoa mmasai mwenye ng'ombe 1000 alafu unampeleka tanga kwenye eka moja na kinyumba hicho..utakuwa umemsadia kuimprove maisha yake au umemsababishia umadikini?unajua thamani ya ng'ombe 200 ni shilingi ngapi?serikali mmefail kabisa..kama kuna changamoto wamasai wapewe alimu dhidi ya hiyo changamoto au taizo...hiyo plan ni yakumsababishia mmasai umaskini..kuna dhana pana ya kutafsiri utajiri au maisha bora katika jamii...mambo ya kitenge kusema wamasai wanaishi maisha duni ngorongoro ni hoja za kisiasa na za aibu
 
Wamasai walinyimwa haki zao sababu ya kuhitaji misaada, sasa UK nao wanastisha misaada, ajabu kuna watu wanaonyesha kuhuzunika sababu ya kukosa misaada

Swali: je Mungu aliiumba Tanzania ili ije kuwa nchi iishiyo kwa kutegemea misaada?

Hatuna mawazo mbadala wa kuendeleza taifa letu mbali na kuitegemea misaada?

Kama jibu ni ndio, bado tunayo haki ya kujiona bora kuliko viumbe wengine kama paka , panya , na mende waishio majumbani mwetu?
 
hapo Zanzibar kuna mashoga kama woteeee Acha kulalamika
 
Si wamasai watakaoikosesha nchi yetu misaada. Ni seeikali inayoendeshwa kihuni ndiyo itasababisha madhilq hayo kwa nchi yetu.

Hata hivyo, sisi waTZ ni lazima tuondokane na fikra za utegemezi kwa wahisani. Tutafanya hivyo kwa kupigania rasli mali zatu na kuendelea kuwaunga mkono wamasai katika harakati zao zao.
 
Hadi leo sijawahi kuelewa sababu ya maana ya kuwatoa wamasai Ngorongoro wakati miaka naenda rudi wameishi na wanyama pori bila shida
Aliuza ili apate hela!!kifupi ipo hivyo!!

Hivi deep state mmelala usingizi wa pono!!?


Tumia akili huko mlipo mnafanya Nini!!?au mmepata na nyie mgao!!?

Nikisoma nyuzi zako huwa napata matumaini mbona sasa mpo kimya!!?hebu angalia:-

1.Rais ambaye hajawahi kugombea ilitokea marekani itatokea na huku!

2.operation imesitishwa the state amesema apewe muda!

3.franklin delano Roosevelt na utawala wa miaka 12 ndani ya Tanzania.

4.mstaafu aliekwisha kustaafu lakini hataki kustaafu kustaafishwa!

5.kitabu kilichoanzwa kuandikwa Kisha kikaachwa kitamalizika Kwa hesabu hii!

6.usaliti wa jemedari wa marekani!!

7.kitambaa cheusi katika Bunge la marekani!!


TIMIZENI MAANDIKO YENU MUOKOE NCHI!!
 

Msemaji mkuu wa serikali azungumza kuhusu azimio la wabunge wa Bunge la Ulaya


View: https://m.youtube.com/watch?v=FH4XWztAiqsMr. Mobhare Matinyi, Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania ~ the Chief Spokesman of the Government of Tanzania // Habari MAELEZO

N.B
European Parliament urges authorities to stop forced evictions of Maasai communities

Brussels, 14/12/2023 (Agence Europe)
In a resolution adopted (493 votes in favour, 29 against, and 17 abstentions) on Thursday, 14 December, the European Parliament has sided with the Maasai communities who have been expelled from their land in the Ngorongoro District of Tanzania notably due to a vast section of land in the Loliondo area being converted into a game reserve.
 
Ukiona mwanamke anawafukuza watu waliokuwa katika asili yao kwa miaka na miaka, huyu ni mtu hatari na hatasita kugeuza kura zote za 2025 kama ilivyokuwa 2020.
 
Hadi leo sijawahi kuelewa sababu ya maana ya kuwatoa wamasai Ngorongoro wakati miaka naenda rudi wameishi na wanyama pori bila shida
Naskia wanyama wameandamana Jana

Haiwezekani ndugu zao wanaondoka

Hali ni tete mbugani

Serikali inajaribu kuongea na kiongozi wa wanyama mbugani

Jamaa haelewi kabisa hataki hata Mia
 
Siungi mkono Wamasai kuhamishwa toka Ngorongoro kwa mabavu; lakini hao wakoloni wakituzingua tuhamie BRICS haraka sana. BRICS ni alternative nzuri ya nchi kulinda uhuru wake dhidi ya ukandamizaji na ukoloni mamboleo wa nchi za ulaya na marekani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…