Wamasai wanakwenda kuua misaada ya UN na EU kwa Tanzania; Ngorongoro imetugeuka vibaya

Wamasai wanakwenda kuua misaada ya UN na EU kwa Tanzania; Ngorongoro imetugeuka vibaya

Maamuzi ya bunge la Ulaya kuhusu kuhamisha Wamasai Ngorongoro linakwenda kutaathiri kiuchumi. Tutaathirika kwa sababu tulitumia nguvu huku tukijua kabisa kwamba tunajipanga kuimarisha mahusiano na mataifa mengine.

Bunge la Ulaya kwa zaidi ya asilimia 90 limesema maamuzi ya Tanzania siyo sahihi. Means wazungu wanawapenda Watanzania kuliko sisi tunavyojipenda. Wazungu ni waasisi wa maliasili ,walitunga sheria na kanuni zote za kulinda rasilimali. Wamesema Wamasai ni ASILI na kwamba hakuna kinachoweza kufuta asili yao ngorongoro.

Tunatokaje hapa? Tunawezaje kukwepa athari za kiuchumi pale watakapoamua kulimalia hii hoja? Tujadiliane
Wamasai wana kosa gani? Ma CCM ndo yamefukuza wamasai Sasa ulitaka wakatae kuhama wauawe?
Laumu serikali kwa kuuza ngorongoro.
 
Mungu wabariki Wazungu
Ndiyo shida yenu hii, mmekuwa makuwadi wa wazungu. Siku mkichukua nchi sisi sijui tutakuwa wageni wa nani...HamqeI kusimama kama ninyi bila.mzunhu nyuma yenu?
 
Maamuzi ya bunge la Ulaya kuhusu kuhamisha Wamasai Ngorongoro linakwenda kutaathiri kiuchumi. Tutaathirika kwa sababu tulitumia nguvu huku tukijua kabisa kwamba tunajipanga kuimarisha mahusiano na mataifa mengine.

Bunge la Ulaya kwa zaidi ya asilimia 90 limesema maamuzi ya Tanzania siyo sahihi. Means wazungu wanawapenda Watanzania kuliko sisi tunavyojipenda. Wazungu ni waasisi wa maliasili ,walitunga sheria na kanuni zote za kulinda rasilimali. Wamesema Wamasai ni ASILI na kwamba hakuna kinachoweza kufuta asili yao ngorongoro.

Tunatokaje hapa? Tunawezaje kukwepa athari za kiuchumi pale watakapoamua kulimalia hii hoja? Tujadiliane
Sasa kama washauri wa siasa wa Mama Kizimkazi ni akina Petro Magoti unategemea nini?
Samia ameanza kuharibu Uchumi wa raia mmojammoja na akiachwa ataharibu sana mbele ya safari!
Mara ooh,anafungua nchi,kwani ni lini Tanzania ilifungwa kwa Wageni kuja!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Huu ulikuwa unyanyasaji mkubwa sana. Watu wameishi hapo miaka yote, unakuja kuwatoa ghafla na kutaka waanze maisha mengine ambayo sio asili yao.

Ngoja tuone, ila naunga mkono uamuzi huo.
Bado kuna sekeseke la kule Ruaha National Park Wananchi wamefanyiwa vitendo vya kikatili kuhamishwa na kubakwa juu.World Bank wamemng'ang'ania Mama Kizimkazi na serikali yake!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Jamaa unapenda sana ligi..umeamua kutoka hadi nje ya mada..
Kupenda au kutopenda ligi si issue. Hata baadhi ya maendeleo makubwa ya kisayansi yameletwa kwa mashindano.

Issue ni, kilichoandikwa ni kweli au si kweli?

Kiukweli, Tanzania kupenda ligi si tatizo, tatizo watu wengi hawapendi kujadiliana kwa ligi iliyo fact based na yenye research iliyo na attention to detail.

Hujaweza kukanusha kilichoandikwa. Umefanya logical fallacy moja inaitwa ad hominem attack.

Ad Hominem attack ni kuacha kujadili hoja iliyotolewa na mtu, na kumshambulia mtu mwenyewe.

Ni shambulio linalotumiwa na watu wasio na hoja kuondoka kwenye mazungumzo ya hoja na kwenda kwenye mazungumzo ya kumshambulia mtu binafsi, kwa sababu ya chuki, ujinga, kukosa hoja etc.

Kuhusu kutoka nje ya mada, ni wazi ukioneshwa mada hii hapa huwezi kuichambua, pengine huwezi hata kuitambua, na huelewi maana ya open forum kama JF. Huelewi maana ya kaulimbiu ya "Where We Dare To Talk Openly".

Ukitaja chochote JF, unaruhusu watu kukihoji.

Tunaweza kuendelea kujadiliana mada ya msingi, na hapo hapo tukasahihishana kwenye mada nyingine zinazojitokeza. Si lazima tukubaliane kwenye kila kitu.

We can chew gum and walk. We can reject premises. We do not have to agree on everything for fear of being labelled "wapenda ligi".

Ndiyo maana, jibu langu kwa mtoa mada limeanza kwa kusema kuwa nakubaliana naye kwa mambo mengi aliyoandika. Maana yake, kimsingi simpingi, nimeona kuna hii habari moja tu haijakaa sawa, natoa habari ambayo nafikiri itaiweka hii habari ya wazungu kuwa waasisi wa kutetea maliasili, rasilimali, mazingira vizuri zaidi.

Mtoa mada alitaja hiyo hoja niliyoihoji na kuipinga, sikuileta hapa out of thin air.

Kuna watu wanaamini kuwa wazungu ndio walioanzisha uanamazingira, wakati Afrika tulikuwa na tuna mpaka dini za kuheshimu mazingira, na Wazungu ndio watu walioharibu mazingira kwa kiasi kikubwa sana, ndiyo kwanza wanaamka kwenye mambo ya kutunza mazingira.

Kuna jamaa alikuwa anasimulia alikuwa katika team ya kupanua bandari ya Dar miaka ya 1970s, akaingia kwenye shamba la mzee mmoja akimuelezea mpango wa serikali wa kupanua bandari. Yule mzee mwenye shamba akamwambia jamaa kuwa hawezi kuruhusu upanuzi wa bandari kwa sababu hii miti ni mungu kwake, anafanya ibada za asili hapo, haruhusu miti ikatwe.

Muandishi nguli aliyeshinda nishani ya Pulitzer, Jared Diamond, ameandika kitabu kizima kinachoangazia mambo haya, kinaitwa "The World Until Yesterday: What Can We Learn From Traditional Societies?".

Ubaya ni kwamba na sisi siku hizi tumeambukizwa systems za wazungu, mtu akiangalia historia fupi anaona wao ndio wanatufundisha sisi kutunza mazingira, kitu ambacho ukiangalia historia vizuri utaona si kweli. Muafrika akikataza kukata miti anaitwa mpagani mshenzi, Mzungu akikataza kukata miti anaitwa mwanamazingira.

Hujaigusia kabisa hii hoja, na pengine hujaweza hata kuitambua na kuielewa hii hoja.

Umerukia kumshambulia mtoa hoja, ad hominem attack.

Sasa, kwa tabia yako ya kuacha kujadili hoja na kumshambulia mtoa hoja, ad hominem attack yako, wewe ndiye umekuwa mpenda ligi, bila hata kutetea ukweli, na kwa kutoka nje ya hoja.

Umefanya kitu kinachoitwa "psychological projection". Mashuzi ya kuendekeza ligi za kutoka nje ya hoja kwa logical fallacy ya ad hominem attack umejamba wewe, lawama unanipa mimi.

Waswahili walisema, "Nyani haoni kundule".
 
Kwa hiyo kwako ni sawa tu Mmasai mwenye sime na mkuki akiondolewa kwenye ardhi yake kisha kupewa Mwarabu mwenye bunduki na risasi???

Kwako nyumnbu ana dhamani kubwa kuliko Binadamu mwenzako??

Tuachane na hayo, Mtu ana wake zake 5 na kila mwanamke ana nyumba yake pamoja na watoto wake. Unamhamisha na kwenda kumpa nyumba moja yenye vyumba viwili eti akaishi yeye na wake zake pamoja na watoto wake wasiopungua 20. Hapo utu wake utakuwa wapi?? Wazungu wameliona hilo na wakalifanyia kazi wewe unaleta mambo yako ya Uzungu na Uarabu.
Hakuna mtu anapenda kuhamishwa makazi yake aliyozoea. Wamasai lazima wapambanie kubaki.
Je nini kifanyike? Wamasai waachwe waendelee kuishi hifadhi ya Ngorongoro?
Kwa takwimu za kuongezeka kwa watu na kuongezeka kwa mifugo baada ya miaka 10 ngorongoro itabaki? Kumbuka wanaoongoza kwa uharibifu wa mazingira ni wafugaji.
Harafu tusiwe na perspective ya kirofa kuwa kuwaondoa wamasai Ngorongoro ni kujali nyati kuliko watu.
Serikali makini haiwezi kufanya maamuzi kwa kuangalia masilahi ya kundi moja la watu tu, yanaangaliwa pia maslahi mapana na nchi.
Ukisema uangalie kila mtu anataka nini huwezi fanya kitu, sisi wanadamu ni wabinafsi sana.
Njia ya kuwaondoa wamasai pale labda inaweza ikawa sio njia nzuri ila wamasai lazima wangehamishwa tu kuokoa hifadhi ya Ngorongoro.
 
Hii ndo sehemu mama natakiwa kusimama na kuwaonesha hawa mabeberu kuwa tunaweza kusonga mbele bila utegemezi kwao,mimi binafsi naunga mkono wamasai kuondolewa kwenye maeneo ya hifadhi ya ngorongoro kwa hoja ya uhifadhi wa mazingira .

Ikumbukwe kuwa jamii nyingi za wafugaji wakiwemo wasukuma na maasai wanaongoza kwa kuharibu mazingira,ikiwa wataachwa waendelee na shughuli zao bila kuingiliwa na serikali nadhani baada ya 20 yrs to come ngorongoro itakuwa jangwa.

Serikali imechelewa kuchukua hatua,na tutaendelea na mifumo hii huku tukiharibu mazingira yetu tusipochukua hatua sitahiki,nashauri serikali kutunga sheria kali ili kuwabana wafugaji kupunguza idadi ya mifugo yao kwa hoja ya utuzaji mazingira,moja ya njia sahihi ni kuwatoza kodi wafugaji,haiwzekani mimi mwalimu mwenye mshahara wa basic ya 700K nalipa 50K kama kodi huku mfugaji mwenye ngombe 200 halipi chochote,no

Pili serikali ije na sheria ya kuwabana wafugaji kuchungia kwenye maoneo yale tu wanayomiliki hii itasaidi kuondoa migogoro ya wakulima na wafugaji
Huna lolote..we unakili kuliko watangulizi wako wote..seriakli msitumie hoja za kisiasa kuharibu maisha na kupora haki ya wamaasai kwa maslahi binafsi ..swali la msingi kama wameweza kuishi zaidi ya miaka 2000 huko na hakujawahi kutokea tatizo la kuuwa wanyama na kuharibu mazingira..maana yake ni ni hoja na kigandamizaji kwa haki..hivi utamtoa mmasai mwenye ng'ombe 1000 alafu unampeleka tanga kwenye eka moja na kinyumba hicho..utakuwa umemsadia kuimprove maisha yake au umemsababishia umadikini?unajua thamani ya ng'ombe 200 ni shilingi ngapi?serikali mmefail kabisa..kama kuna changamoto wamasai wapewe alimu dhidi ya hiyo changamoto au taizo...hiyo plan ni yakumsababishia mmasai umaskini..kuna dhana pana ya kutafsiri utajiri au maisha bora katika jamii...mambo ya kitenge kusema wamasai wanaishi maisha duni ngorongoro ni hoja za kisiasa na za aibu
 
Maamuzi ya bunge la Ulaya kuhusu kuhamisha Wamasai Ngorongoro linakwenda kutaathiri kiuchumi. Tutaathirika kwa sababu tulitumia nguvu huku tukijua kabisa kwamba tunajipanga kuimarisha mahusiano na mataifa mengine.

Bunge la Ulaya kwa zaidi ya asilimia 90 limesema maamuzi ya Tanzania siyo sahihi. Means wazungu wanawapenda Watanzania kuliko sisi tunavyojipenda. Wazungu ni waasisi wa maliasili ,walitunga sheria na kanuni zote za kulinda rasilimali. Wamesema Wamasai ni ASILI na kwamba hakuna kinachoweza kufuta asili yao ngorongoro.

Tunatokaje hapa? Tunawezaje kukwepa athari za kiuchumi pale watakapoamua kulimalia hii hoja? Tujadiliane
Wamasai walinyimwa haki zao sababu ya kuhitaji misaada, sasa UK nao wanastisha misaada, ajabu kuna watu wanaonyesha kuhuzunika sababu ya kukosa misaada

Swali: je Mungu aliiumba Tanzania ili ije kuwa nchi iishiyo kwa kutegemea misaada?

Hatuna mawazo mbadala wa kuendeleza taifa letu mbali na kuitegemea misaada?

Kama jibu ni ndio, bado tunayo haki ya kujiona bora kuliko viumbe wengine kama paka , panya , na mende waishio majumbani mwetu?
 
Nchi za Ulaya zinaongozwa na ma-Rais ambao ni mashoga na zimebariki ndoa za jinsia moja. Hazina audacity ya kutuamulia Waafrika hususan Watanzania tunaojitambua. Ya kwao yanawashinda mpaka wanaume kwa wanaume wanaoana, sembuse watuamulie ya kwetu!! No way

Hatuwezi kuamuliwa na Bunge la wase_nge
hapo Zanzibar kuna mashoga kama woteeee Acha kulalamika
 
Maamuzi ya bunge la Ulaya kuhusu kuhamisha Wamasai Ngorongoro linakwenda kutaathiri kiuchumi. Tutaathirika kwa sababu tulitumia nguvu huku tukijua kabisa kwamba tunajipanga kuimarisha mahusiano na mataifa mengine.

Bunge la Ulaya kwa zaidi ya asilimia 90 limesema maamuzi ya Tanzania siyo sahihi. Means wazungu wanawapenda Watanzania kuliko sisi tunavyojipenda. Wazungu ni waasisi wa maliasili ,walitunga sheria na kanuni zote za kulinda rasilimali. Wamesema Wamasai ni ASILI na kwamba hakuna kinachoweza kufuta asili yao ngorongoro.

Tunatokaje hapa? Tunawezaje kukwepa athari za kiuchumi pale watakapoamua kulimalia hii hoja? Tujadiliane
Si wamasai watakaoikosesha nchi yetu misaada. Ni seeikali inayoendeshwa kihuni ndiyo itasababisha madhilq hayo kwa nchi yetu.

Hata hivyo, sisi waTZ ni lazima tuondokane na fikra za utegemezi kwa wahisani. Tutafanya hivyo kwa kupigania rasli mali zatu na kuendelea kuwaunga mkono wamasai katika harakati zao zao.
 
Hadi leo sijawahi kuelewa sababu ya maana ya kuwatoa wamasai Ngorongoro wakati miaka naenda rudi wameishi na wanyama pori bila shida
Aliuza ili apate hela!!kifupi ipo hivyo!!

Hivi deep state mmelala usingizi wa pono!!?

Tumia akili huko mlipo mnafanya Nini!!?au mmepata na nyie mgao!!?

Nikisoma nyuzi zako huwa napata matumaini mbona sasa mpo kimya!!?hebu angalia:-

1.Rais ambaye hajawahi kugombea ilitokea marekani itatokea na huku!

2.operation imesitishwa the state amesema apewe muda!

3.franklin delano Roosevelt na utawala wa miaka 12 ndani ya Tanzania.

4.mstaafu aliekwisha kustaafu lakini hataki kustaafu kustaafishwa!

5.kitabu kilichoanzwa kuandikwa Kisha kikaachwa kitamalizika Kwa hesabu hii!

6.usaliti wa jemedari wa marekani!!

7.kitambaa cheusi katika Bunge la marekani!!

TIMIZENI MAANDIKO YENU MUOKOE NCHI!!
 
Maazimio ya pamoja

13.12.2023 JOINT MOTION FOR A RESOLUTION on the Maasai Communities in Tanzania​

Motion for a European Parliament resolution on the Maasai Communities in Tanzania

(2023/3024(RSP))

The European Parliament,

– having regard to Rules 144(5) and 132(4) of its Rules of Procedure,

A. whereas the Maasai communities are facing evictions from their land in the Ngorongoro District, which includes the Ngorongoro Conservation Area and the Loliondo Area;

B. whereas in June 2022, the Tanzanian authorities began converting 1 500 km2 of land in Loliondo into a game reserve, leading to widespread evictions and depriving over 70 000 people of access to grazing land critical for their livestock’s health and their livelihoods; whereas this was not the first attempt to block the Maasai in Loliondo from accessing grazing village land with little or no consultation;

C. whereas since June 2022 in the Ngorongoro Conservation Area, the government has restricted access to vital services such as food, education, water and healthcare, forcing the departure of many Maasai communities;

D. whereas respect of Indigenous Peoples and Local Communities (IPLC) rights is a prerequisite for effective biodiversity conservation; whereas UN independent experts and the African Commission on Human and Peoples’ Rights have urged Tanzania to stop all forced evictions in Ngorongoro and have raised concerns about the government’s inadequate consultation with the affected Maasai communities and the lack of transparency;

1. Urges the Tanzanian Government to immediately halt the forcible evictions of Maasai communities, to avoid any measures that will negatively impact the lives, livelihoods and cultures of these communities, to guarantee their safe return and uphold their right of access to justice and effective remedies for victims;

2. Calls on the Tanzanian Government to recognise and protect the rights of IPLCs and to recognise the lands and resources that the Maasai communities have managed for generations and their role in maintaining wildlife and biodiversity;

3. Reaffirms that all measures relating to Maasai communities must respect the rule of law and human rights, with particular regard to the rights of IPLCs;

4. Calls on the authorities to work with affected communities to design a permanent and acceptable solution for the Maasai in the Ngorongoro District that respects their rights;

5. Calls on the European External Action Service and the Commission in their political dialogue with the Tanzanian Government to insist on the importance of upholding human rights;

6. Urges the Tanzanian Government to allow UN and EU institutions observation visits;

7. Calls on the Commission to increase its development cooperation and humanitarian aid allocations for Tanzania, given that no aid had initially been planned in support of the Maasai;

8. Calls on the Commission to report to Parliament on EU budget support programmes and other initiatives in Tanzania, with particular attention to projects dealing with biodiversity loss and climate change and to the built-in human rights safeguards;

9. Instructs its President to forward this resolution to the EU institutions, the Member States, the Government and Parliament of Tanzania, and the UN.

Source : JOINT MOTION FOR A RESOLUTION on the Maasai Communities in Tanzania | RC-B9-0511/2023 | European Parliament

Msemaji mkuu wa serikali azungumza kuhusu azimio la wabunge wa Bunge la Ulaya

View: https://m.youtube.com/watch?v=FH4XWztAiqs
Mr. Mobhare Matinyi, Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania ~ the Chief Spokesman of the Government of Tanzania // Habari MAELEZO

N.B
European Parliament urges authorities to stop forced evictions of Maasai communities

Brussels, 14/12/2023 (Agence Europe)
In a resolution adopted (493 votes in favour, 29 against, and 17 abstentions) on Thursday, 14 December, the European Parliament has sided with the Maasai communities who have been expelled from their land in the Ngorongoro District of Tanzania notably due to a vast section of land in the Loliondo area being converted into a game reserve.
 
Maamuzi ya bunge la Ulaya kuhusu kuhamisha Wamasai Ngorongoro linakwenda kutaathiri kiuchumi. Tutaathirika kwa sababu tulitumia nguvu huku tukijua kabisa kwamba tunajipanga kuimarisha mahusiano na mataifa mengine.

Bunge la Ulaya kwa zaidi ya asilimia 90 limesema maamuzi ya Tanzania siyo sahihi. Means wazungu wanawapenda Watanzania kuliko sisi tunavyojipenda. Wazungu ni waasisi wa maliasili ,walitunga sheria na kanuni zote za kulinda rasilimali. Wamesema Wamasai ni ASILI na kwamba hakuna kinachoweza kufuta asili yao ngorongoro.

Tunatokaje hapa? Tunawezaje kukwepa athari za kiuchumi pale watakapoamua kulimalia hii hoja? Tujadiliane
Ukiona mwanamke anawafukuza watu waliokuwa katika asili yao kwa miaka na miaka, huyu ni mtu hatari na hatasita kugeuza kura zote za 2025 kama ilivyokuwa 2020.
 
Hadi leo sijawahi kuelewa sababu ya maana ya kuwatoa wamasai Ngorongoro wakati miaka naenda rudi wameishi na wanyama pori bila shida
Naskia wanyama wameandamana Jana

Haiwezekani ndugu zao wanaondoka

Hali ni tete mbugani

Serikali inajaribu kuongea na kiongozi wa wanyama mbugani

Jamaa haelewi kabisa hataki hata Mia
 
Siungi mkono Wamasai kuhamishwa toka Ngorongoro kwa mabavu; lakini hao wakoloni wakituzingua tuhamie BRICS haraka sana. BRICS ni alternative nzuri ya nchi kulinda uhuru wake dhidi ya ukandamizaji na ukoloni mamboleo wa nchi za ulaya na marekani.
 
Back
Top Bottom