Jamaa unapenda sana ligi..umeamua kutoka hadi nje ya mada..
Kupenda au kutopenda ligi si issue. Hata baadhi ya maendeleo makubwa ya kisayansi yameletwa kwa mashindano.
Issue ni, kilichoandikwa ni kweli au si kweli?
Kiukweli, Tanzania kupenda ligi si tatizo, tatizo watu wengi hawapendi kujadiliana kwa ligi iliyo fact based na yenye research iliyo na attention to detail.
Hujaweza kukanusha kilichoandikwa. Umefanya logical fallacy moja inaitwa
ad hominem attack.
Ad Hominem attack ni kuacha kujadili hoja iliyotolewa na mtu, na kumshambulia mtu mwenyewe.
Ni shambulio linalotumiwa na watu wasio na hoja kuondoka kwenye mazungumzo ya hoja na kwenda kwenye mazungumzo ya kumshambulia mtu binafsi, kwa sababu ya chuki, ujinga, kukosa hoja etc.
Kuhusu kutoka nje ya mada, ni wazi ukioneshwa mada hii hapa huwezi kuichambua, pengine huwezi hata kuitambua, na huelewi maana ya open forum kama JF. Huelewi maana ya kaulimbiu ya "Where We Dare To Talk Openly".
Ukitaja chochote JF, unaruhusu watu kukihoji.
Tunaweza kuendelea kujadiliana mada ya msingi, na hapo hapo tukasahihishana kwenye mada nyingine zinazojitokeza. Si lazima tukubaliane kwenye kila kitu.
We can chew gum and walk. We can reject premises. We do not have to agree on everything for fear of being labelled "wapenda ligi".
Ndiyo maana, jibu langu kwa mtoa mada limeanza kwa kusema kuwa nakubaliana naye kwa mambo mengi aliyoandika. Maana yake, kimsingi simpingi, nimeona kuna hii habari moja tu haijakaa sawa, natoa habari ambayo nafikiri itaiweka hii habari ya wazungu kuwa waasisi wa kutetea maliasili, rasilimali, mazingira vizuri zaidi.
Mtoa mada alitaja hiyo hoja niliyoihoji na kuipinga, sikuileta hapa out of thin air.
Kuna watu wanaamini kuwa wazungu ndio walioanzisha uanamazingira, wakati Afrika tulikuwa na tuna mpaka dini za kuheshimu mazingira, na Wazungu ndio watu walioharibu mazingira kwa kiasi kikubwa sana, ndiyo kwanza wanaamka kwenye mambo ya kutunza mazingira.
Kuna jamaa alikuwa anasimulia alikuwa katika team ya kupanua bandari ya Dar miaka ya 1970s, akaingia kwenye shamba la mzee mmoja akimuelezea mpango wa serikali wa kupanua bandari. Yule mzee mwenye shamba akamwambia jamaa kuwa hawezi kuruhusu upanuzi wa bandari kwa sababu hii miti ni mungu kwake, anafanya ibada za asili hapo, haruhusu miti ikatwe.
Muandishi nguli aliyeshinda nishani ya Pulitzer, Jared Diamond, ameandika kitabu kizima kinachoangazia mambo haya, kinaitwa "
The World Until Yesterday: What Can We Learn From Traditional Societies?".
Ubaya ni kwamba na sisi siku hizi tumeambukizwa systems za wazungu, mtu akiangalia historia fupi anaona wao ndio wanatufundisha sisi kutunza mazingira, kitu ambacho ukiangalia historia vizuri utaona si kweli. Muafrika akikataza kukata miti anaitwa mpagani mshenzi, Mzungu akikataza kukata miti anaitwa mwanamazingira.
Hujaigusia kabisa hii hoja, na pengine hujaweza hata kuitambua na kuielewa hii hoja.
Umerukia kumshambulia mtoa hoja, ad hominem attack.
Sasa, kwa tabia yako ya kuacha kujadili hoja na kumshambulia mtoa hoja, ad hominem attack yako, wewe ndiye umekuwa mpenda ligi, bila hata kutetea ukweli, na kwa kutoka nje ya hoja.
Umefanya kitu kinachoitwa "psychological projection". Mashuzi ya kuendekeza ligi za kutoka nje ya hoja kwa logical fallacy ya ad hominem attack umejamba wewe, lawama unanipa mimi.
Waswahili walisema, "Nyani haoni kundule".