Wamasai wavamia Kata ya Kimnyaki - Arumeru wakidai ng'ombe wao walioibiwa, Polisi wapiga mabomu ya machozi

Wamasai wavamia Kata ya Kimnyaki - Arumeru wakidai ng'ombe wao walioibiwa, Polisi wapiga mabomu ya machozi

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
706
Reaction score
1,716

Na Joseph Ngilisho | Arumeru
TAHARUKI imetanda katika Kata ya Kimnyaki, Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, baada ya kundi la watu zaidi ya 700 wanaodaiwa kutoka Kata ya Lengijave kuvamia maboma ya wakazi wa eneo hilo na kupora ng’ombe 26 kwa nguvu, hali iliyolazimu polisi kuingilia kati na kutumia mabomu ya machozi kuzuia mapigano.
880582264_2489411781584790_525378634328391324_n.jpg
Tukio hilo lililotokea majira ya saa 9 usiku, linadaiwa kuchochewa na mgogoro wa wizi wa mifugo, baada ya wakazi wa Lengijave kuwatuhumu wenzao wa Kimnyaki kuhusika na kupotea kwa ng’ombe wao.

Hata hivyo, licha ya pande hizo kuwa na mazungumzo ya awali na wakazi wa Kimnyaki kukubali kulipa fidia ya ng’ombe 12, kundi hilo lilivamia tena usiku na kuchukua mifugo iliyokuwa katika maboma ya wananchi.

Akisimulia mkasa huo, mkazi wa Kimnyaki, Yohana Lekamoi, alisema wavamizi hao walifika usiku na kuanza kuvamia nyumba na maboma mbalimbali, wakichukua ng’ombe waliowakuta hadi idadi yao kufikia 26.

Alisema walishangazwa na uvamizi huo kwa kuwa tayari walikuwa wamefanya mazungumzo na wakazi wa Lengijave kuhusu madai ya kupotea kwa mifugo, hatua iliyofikia makubaliano ya kulipa fidia ya ng’ombe 12.

Alisema kitendo cha kundi hilo kurudi kwa nguvu na kuvamia makazi yao kiliibua hofu kubwa miongoni mwa wananchi.

"Tunawashukuru sana polisi waliofika na kuingilia kati. Walitumia mabomu ya machozi kuwatawanya na kufanikiwa kurejesha baadhi ya mifugo iliyokuwa imeporwa," alisema Lekamoi.
WhatsApp Image 2026-11-03 at 16.58.57.jpeg
Hali ilikuwa tete zaidi baada ya wakazi wa Kimnyaki, kwa mujibu wa mashuhuda, kuanza kukusanyika wakiwa na silaha za jadi zikiwemo sime na mikuki kwa lengo la kufuatilia na kukomboa mifugo yao.

Baadhi ya wananchi walisema hatua ya polisi kuingilia kati iliokoa hali isigeuke kuwa mapigano makubwa ambayo yangeweza kusababisha vifo na majeruhi.

Walisema mgogoro huo wa mifugo unahitaji kushughulikiwa haraka na viongozi wa serikali za vijiji, kata na vyombo vya usalama ili kuzuia kulipizana kisasi na kurejea kwa vurugu.

Hata hivyo, bado haijafahamika iwapo watu waliotuhumiwa kuhusika na uvamizi huo wamekamatwa, huku wananchi wakitaka hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya wote waliohusika.

Pia soma ~ Polisi: Tunachunguza Vijana Jamii ya Kimasai kuvamia wenzao wa Jamii ya Kimasai eneo la Kimnyaki - Arumeru
 
Wamasai wanapaswa madhibitiwe mapema sana , hata moro wamekua na kiburi mno, wanachungia mazao kwa kiburi, kwa madai ya kuwa hakuna wakuwafanya kitu kwa sababu ng'ombe ni wa wakubwa , wao ni wachungaji tu
 
Mambo ya kishamba na kijinga sana
 
Wamasai wanapaswa madhibitiwe mapema sana , hata moro wamekua na kiburi mno, wanachungia mazao kwa kiburi, kwa madai ya kuwa hakuna wakuwafanya kitu kwa sababu ng'ombe ni wa wakubwa , wao ni wachungaji tu
Wekeni asali katika mahindi wakila ng'ombe wanadedi na wanahama eneo hilo,wana hela hao bila ya hivyo hamuwawezi.
 
Back
Top Bottom