Yeah, Wambura yuko sahihi,
Wao TFF wnamtuhumu kua alighushi nyaraka akachukua fedha za Jecks, sasa ilifaa hao Jecks waje wathibitishe kua hawakupewa fedha zao. Lakini TFF imedai haikukaa kikao ili kusikiliza mashahidi, bali kuthibitisha tuhuma.
Pili kawaida summons ya kumuita mtu inatakiwa kutolewa kwa siku zisizopungua tatu ili mtuhumiwa apate kujipanga kwa utetezi, hapa wambura kapewa siku 2 tu.
Tatu kabla ya kikao/kesi kuanza inabidi kila upande kuelezea mashahidi na vielelezo watakavyotumia ili upande mwengine ujipange kwa utetezi against vielelezo hivyo lakini pia hili halikufanyika.
Nne tuhuma anazotuhumiwa nazo Wambura ni za toka enzi ambazo Karia kwa cheo chake ndie aliekua mlipaji Mkuu wa hizo fedha, anaachwaje kuhusishwa nazo??
Tano Tuhuma hizo zinahusisha kufoji nyaraka, why isiwe ni jukumu la Polisi kuthibitisha kua kuna forgery iliyofanyika?? TFF wana utaalamu wa kuchunguza forgery??
Sita tuhuma hizi ni za muda mrefu, kabla hata ya uchaguzi. Kwanini zimekuja kuibuliwa muda huu?? Kwanini pamoja na tuhuma hizi bado aliruhusiwa kugombea lakini sasa anaondolewa??
Kwa kumalizia inaonekana Makamu wa Rais wa TFF ndio wanaokuja kua Rais ajae wa TFF. Tukianaza na kina Nassibu Ramadhan, Athuman Nyamlani, Walace Karia katika hawa angalao wapo waliokuja kua either Rais au Kaimu rais wa TFF. Inawezekana kwa Wambura ni hofu tu ya watawala walioko TFF now kumuogopa.
-Ra