Elections 2010 Wameanza kuchakachua hapa

Elections 2010 Wameanza kuchakachua hapa

Nimewakilisha pale Mlimani-utawala. Kimkakati zaidi, japo diwani simjui bt nilipoona 'V' I knew what to do.
 
Jamani wameanza kuchakachua mapema majina yamechanganywa watu wanahangaika ovyo. Ila wanasema hawaondoki mpaka kieleweke. Mwamko upo wa hali ya juu. Mm nilikosa jina langu nimelia machozi. Kweli tunaonewa sana.

KWA NINI HUKUENDA KUHAKIKI JINA LAKO TANGU Juzi AU JANA.... WHY WAIT TILL LAST MINUTES..

ila na wewe usiondoke kituoni hadi upige kura!!!! mafanikio mema
 
Nimeisha piga kura yangu tayari, ila nimeshangazwa na mfumo wa karatasi za kupigia kura, kwani huo mtindo wa kuandika namba ya shahada kwenye karatasi unayo pigia, na kuibakiza kwenye kishina, mtu akiamua kufatilia ulimpigia nani anaweza, na hii binafsi naona inahujumu uhuru wa mtu kumchagua unaye mtaka, kwani mtu aweza kwenda trace back kujua nani ulimpigia kura!

Nadhani hii ni kuhujumu demokrasia, kwani kwa mtaji huu wengine waweza kupiga kura za woga, na sasa naelewa vitisho vya baadhi ya wagombea kwamba usipo nipigia kura utanitambua kumbe jeuri yao iko katika kipengele hiki! so sad!
Ila binafsi sijaogopa nimefanya kweli, na nawasihi wengine tugangamare hivo hivo.
 
Thx wakuu. Nipo home sasa. Nilipatwa kihoro maana tulizungushwa sana. Ila mpaka naondoka wenye majina yenye herufi s bado wanahangaika. Kinachotia moyo ni kuwa watu wana msmamo wamesema leo kazi ni moja tu kupiga kura hata kitabu kije saa nane ucku.
 
Ubungo nhc. Watu hawaoni majina yao ni kuhangaika tu.

Yaani wana JF tupo wote kituo kimoja hatufahamiani hahaha Brandon nimepiga kura yangu hapo hapo NHC Ubungo, wale wasimamizi ni bogus kabisa, wamebandika majina kwenye Milango ya vyumba lkn majina kwenye madaftari ndani hayapo, ule ni upuuzi mtupu, niliwahi saa kumi na mbili kamili tukaambiwa kupiga kura ni saa moja wanaanza ilipofika saa moja eti ndo wanasema kuanzia majina ya A mpaka c hayapo pale wakatafute kwenye vyumba vingine, wanampigia simu msimamizi wao eti simu kazima hapatikani daaaaah jamani saa ya Ukombozi ni sasa
 
Nimeisha piga kura yangu tayari, ila nimeshangazwa na mfumo wa karatasi za kupigia kura, kwani huo mtindo wa kuandika namba ya shahada kwenye karatasi unayo pigia, na kuibakiza kwenye kishina, mtu akiamua kufatilia ulimpigia nani anaweza, na hii binafsi naona inahujumu uhuru wa mtu kumchagua unaye mtaka, kwani mtu aweza kwenda trace back kujua nani ulimpigia kura!

Nadhani hii ni kuhujumu demokrasia, kwani kwa mtaji huu wengine waweza kupiga kura za woga, na sasa naelewa vitisho vya baadhi ya wagombea kwamba usipo nipigia kura utanitambua kumbe jeuri yao iko katika kipengele hiki! so sad!
Ila binafsi sijaogopa nimefanya kweli, na nawasihi wengine tugangamare hivo hivo.

Hii mpya sasa mbona hakukuwa na maelekezo kama haya pale UBUNGO NHC? kwa nini uandike namba yako ya shahada kwenye karatasi ya kura?
 
Nyamagana badoooooo na kuna rafiki ameniambia huenda wamefuta...kuna mwenye habari kamili kuhusu Nyamagana?
 
Jamani wameanza kuchakachua mapema majina yamechanganywa watu wanahangaika ovyo. Ila wanasema hawaondoki mpaka kieleweke. Mwamko upo wa hali ya juu. Mm nilikosa jina langu nimelia machozi. Kweli tunaonewa sana.

Unalo sema nikweli nimetoka kituoni kama dakika kumi zilizopita na nilikwenda saa moja kasorobo majina yanao anzia na herufi hayajaandikwa mpaka watu kuanza kubwabwaja ndio waka weka herufi vyema nandipo watu wakawanaja ni foleni gani anatakiwa ajipange ili apige kura kwa kweli bado utaratibu ni mbovu sana NEC hawajajipanga kabisa na tatizo jingine kubwa ni wale walio jiandikisha majuzi hapa majina yao hayapo kabisa na wasimamizi wanawambia eti pigeni simu mtajibiwa ili mjue kama majina yenu yapo wakati huo huo mtendaji wa kata ni mmoja vibanda vya kupigia kura ni vinne ataweza kuhakikije hawa watu kama huyu jina lake lipo na hana ile orodha mpya ya watu wapya waliojiandikisha na kumbukeni huyu mtu hapo alipo ana kitamburisho kipya na kituo alicho jiandikisha ndio hicho alipo kuja kupiga kura na jina ndilo hakuna.

Mama mmoja aliamua kusepa baada ya kupata maelekezo mabovu anambiwa hapa jina lako halipo labda nenda upande wa pili akaenda napo ati hakuna kweli alikutana na maelekezo mabaya na akarudi home. Hii inamaanisha NEC haikutoa semina ya kutosha kwa wasimamiaji wa hilo zoezi la kupiga kura na sidhani kama idadi ya wapiga kura maeneo mengine ita kuwa ni wengi safari hii
 
MLIMANI PRIMARY HAKUNA WAKALA WA CCM!!! SIJUI TUIBE, sema tu hatuna tabia ya wizi kama wao, nimetoka hapo naelekea kituo cha MLIMANI-NKRUMAH HALL
 
Thx wakuu. Nipo home sasa. Nilipatwa kihoro maana tulizungushwa sana. Ila mpaka naondoka wenye majina yenye herufi s bado wanahangaika. Kinachotia moyo ni kuwa watu wana msmamo wamesema leo kazi ni moja tu kupiga kura hata kitabu kije saa nane ucku.
 
Majina nje yapo ila wanasema kitabu hakijafika eti wasubiri. Wengine wanaanza kukata tamaa.

Watulize hao wanaoanza kukata tamaa waambie uchaguzi huu ni muhimu sana kwa Taifa letu. Waambie wasubiri na wawe wavumilivu mpaka kieleweke na nawaomba sana msifanye fujo ya aina yoyote ile.
 
Thx wakuu. Nipo home sasa. Nilipatwa kihoro maana tulizungushwa sana. Ila mpaka naondoka wenye majina yenye herufi s bado wanahangaika. Kinachotia moyo ni kuwa watu wana msmamo wamesema leo kazi ni moja tu kupiga kura hata kitabu kije saa nane ucku.

Hongera kwa uvumilivu wako hatimaye kuweza kuitumia haki yako ya kikatiba
 
Ndo nafika, napiga kituo namba mbili UTAWALA MLIMANI, Habari njema sana kwangu ni kwamba wadau wanakumbushana jinsi ya kuandika na ku-stress pale kwa SLAA ili kura isihamie kwa JK
 
Azania seconndary chumba nilichopigia kura wakala ni mmoja tu wa Chadema naona kuna mgomo mawakala wa CCM labda kuna mtu kala hela yao.Wanafunzi wengi wamekuja kupiga kura,vijana wengi ina maana nzuri.Jana usiku nimetumiwa SMS yenye jina langu Kikwete akiomba kura yangu jamani kuandikisha simu kumbe haya ndio matumizi yake? watu wenye akili ndogo akitumiwa SMS yenye jina lake si atajiona ni mtu muhimu sana na kumpa kura yake kwakuwa kathaminiwa.
 
teheteeh Mkapa aliniboa sana kwenye mkutano wao, nimeamka na hasira za FULL suit, yaani kuanzia Rais, Mbunge na diwani woote Chademaaaaaaaaaa
 
Hii mpya sasa mbona hakukuwa na maelekezo kama haya pale UBUNGO NHC? kwa nini uandike namba yako ya shahada kwenye karatasi ya kura?

Wakuu hakuna sababu ya kuogopa hata wakijua kuna tatizo gani au nyie ni wanachama wa CCM so mnaogopwa kufukuzwa uanachama?, kama mmechagua chadema ni kwasababu mlikuwa na sababu za msingi hakuna ubaya hapo
 
Mbatia ameshindwa kupiga kura. Yani leo mpaka ieleweke...
 
Huwezi amini mpaka sasa ninaemjua ni Mbunge wangu na Rais wangu ila diwani mpaka sasa simjui. Ila sina shaka nijuacho ni kuwa kwa ngazi zote nawapa CHADEMA.

Safari za hapa na pale zimenifanya nisijue diwani halafu sikubadili kituo changu cha kupigia kura
hata mimi mkuu, nilikuwa namjua dr an mpendazoe tu. huyo diwan niliangalia tu kwenye vidole viwili nikajua hapa ndo nyumbani nikaweka vema
 
Back
Top Bottom