Wamebadili Mbinu Wametaka Kumwibia Mzee Wangu Usiku Huu

Wamebadili Mbinu Wametaka Kumwibia Mzee Wangu Usiku Huu

Faana

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2011
Posts
38,657
Reaction score
44,759
Picha inajieleza, wametaka kumwibia mzee wangu kwenye kiswaswadu chake usiku huu, akanikimbilia nimsaidie kutuma fedha kwa mjukuu ndipo nikamshitua akazinduka.

Hivi sasa hawasemi "ile fedha tuma kwa namba hii", wanatuma ujumbe wa namna hii
20230306_224701.jpg
 
Utapeli utaisha siku Serikali ikiamua hivi

Kila NIN isajili namba 1 tu ya mtandao 1

Ikitokea namba yake imehusika kutapeli, namba zote za mhusika zifungwe hadi aende kituo cha polisi kutoa maelezo.

Namba isibadilishwe iwe kama TIN hata mtu akifa namba ibakie kwenye jina lake na ikithibitishwa amekufa basi namba husika ifungwe kwa miaka 10 kabla ya kutolewa kwa mtu mwingine.

Huruma na siasa ndo sababu watu wanaendelea tapeli

Kuhusu namba zaidi, kama ni mfanyabiashara apeleke Leseni, TIN ili asajili kama namba ya biashara, akifanya kosa ifungiwe hadi aende Polisi
 
Tapeli mwingine mwenye namba +255 0689 460 513 juzi kaniharibia siku baada ya kumshtukia kanitukania marehemu mama yangu (RIP) tusi kubwa sana mpaka nikajuta kujibishana naye. Najiuliza si hivi karibuni tu simu zimehahakiwa inawezekana vipi tena hawa matapeli bado wanakuwepo mitandaoni?
 
Pole Sana halafu namba nyingi za matapeli huwa ni za Airtel

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Picha inajieleza, wametaka kumwibia mzee wangu kwenye kiswaswadu chake usiku huu, akanikimbilia nimsaidie kutuma fedha kwa mjukuu ndipo nikamshitua akazinduka.

Hivi sasa hawasemi "ile fedha tuma kwa namba hii", wanatuma ujumbe wa namna hiiView attachment 2539861
Hata mimi nilitumiwa huu ujumbe siku ya jana. Nikauangalia, halafu nikabakia tu kucheka. Maana ni mwezi uliopita tu, line za simu zilihakikiwa na mamlaka husika.

Ila cha kushangaza matapeli bado wanaendelea tu kutamalaki. Hivi ni kwa nini kusiwepo na sheria kali kwenye usajili wa laini ili kuwabaini hawa matapeli kwa urahisi?
 
Hivi wale matapeli wa mtindo huu waliokamatwaga, waliishia wapi?
 
Picha inajieleza, wametaka kumwibia mzee wangu kwenye kiswaswadu chake usiku huu, akanikimbilia nimsaidie kutuma fedha kwa mjukuu ndipo nikamshitua akazinduka.

Hivi sasa hawasemi "ile fedha tuma kwa namba hii", wanatuma ujumbe wa namna hiiView attachment 2539861
Kitambo sana labda ulikuwa hujakutana nayo hio
 
Back
Top Bottom