Wamegeuka timu za Shirikisho ni nyepesi

Wamegeuka timu za Shirikisho ni nyepesi

Kwamba far rabat, monastir, malumo, pyramids wamezidiwa na vipers?
Sio hao tu vilaza wote wanaoshiriki kombe la LOOSERS wakikutana na VIPERS wanabondwa bila wasiwasi.

Mfano nzuri waangalie vilaza TP MAZEMBE na WALAMBA VINYEO walipokutana na wababe VIPERS.
 
Hili unatakiwa umwambie mwanachama na msemaji wa Yanga, Haji Manara.
Kwani Yanga imefika semi final? 😁. Kumbuka Simba ilishafika fainali ya Kombe la CAF
Hao wanaopost thread kila siku kuzungumzia ilo ni hakina manara hao?
 
Hao wanaopost thread kila siku kuzungumzia ilo ni hakina manara hao?
Sio akina Manara, ila wanamnukuu Manara. Tatizo mnamlinda, mwambieni ajitokeze atengue kauli yake. Sasa hapa unataka kuhamishia mzigo wa misumari kwa waanzisha nyuzi wakati ipo wazi kabisa aliyetamka hivyo ni Haji!
 
Ifikie wakati tukubali tu ukweli; mashabiki wengi wa simba ni mbumbumbu.
 
Kama wamegeuka basi hilo ni kosa, lakini bado haiondoi ukweli kwamba timu zinazocheza Kombe la Shirikisho huwa zinapatikana kwa utaratibu mmoja kati ya huu kutoka katika nchi shiriki.
1. Huwa sio mabingwa wa nchi bali wa kikombe cha shirikisho la nchi husika au kikombe maalum au washindi wanaofuata wa kikombe hicho iwapo bingwa wa ligi alitwaa pia kiombe hicho maalum
AU
2. ni washiriki wa michuano ya Klabu Bingwa walioondolewa katika raundi ya pili, au kwa ufupi walioshindwa kuingia katika hatua ya makundi ya CAF Champions League

Huo ndio uhalisia, sasa kama ni wabovu au wazuri walioondolewa kwa bahati mbaya, hilo ni suala lingine la kupima
Mkuu mbona Simba sio mabingwa wa nchi? Au nao ndio miongoni mwa timu izo timu zilizoko klabu bingwa kwa bahati mbaya?
 
Uto wana team nzuri kwa confed kwao imekua rahisi kidogo atakutana na level zake kuanzia robo

Simba tuna team ina quality ila kwa CCL haitoshi kwenda toe to toe na hao so called giants
Kwa msimu huu ingependeza Yanga ndo awe CCL alafu sisi tuwe confed tuone
 
Sio akina Manara, ila wanamnukuu Manara. Tatizo mnamlinda, mwambieni ajitokeze atengue kauli yake. Sasa hapa unataka kuhamishia mzigo wa misumari kwa waanzisha nyuzi wakati ipo wazi kabisa aliyetamka hivyo ni Haji!
Rage ajengewe sanamu
 
Mkuu mbona Simba sio mabingwa wa nchi? Au nao ndio miongoni mwa timu izo timu zilizoko klabu bingwa kwa bahati mbaya?
Kwa mtazamo wa CAF, Simba inastahili kushiriki michuano ya Klabu bingwa ya Afrika. Ni mtazamo huo huo ndio uliotumika kuichagua Simba kushiriki michuano ijayo ya kwanza ya Super League, tena uchaguzi umefanyika bila kujali Simba itashika nafasi ya ngapi katika ligi ya mwaka huu, maana yake hata kama itashuka daraja. Sio mimi, ni CAF.

Na Simba haikuiangusha CAF, maana ndio timu pekee nchini inayoshiriki hatua ya makundi ya Klabu Bingwa za Afrika, na hapo haikuwekwa, imefika kwa kufuzu, na mabingwa wengine wa nchi wamekosa nafasi wakapelekwa huko unakolalamikia (naogopa kupataja nisije nikaonekana mimi ndio muasisi, kumbe ni Manara)
 
Rage ajengewe sanamu
Tena kumbuka, Manara akiwa katika jezi na nembo za Yanga, alisema huku Yanga wenye akili ni wawili tu. Bahati mbaya alipotaja majina hayo mawili, la kwako halikuwepo. Manara ajengewe sanamu
 
Wewe kolo niambie lini ulinifunga kwenye ligi..
This is Yanga Mzee, Hamtuwezi nyie Wachawi
 
Wewe kolo niambie lini ulinifunga kwenye ligi..
This is Yanga Mzee, Hamtuwezi nyie Wachawi
Nakwambia hivi, kwenye ligi tangu aje Nabi timu zimetoa sare zote. Simba na Yanga zikitoka sare unasema Simba imeshindwa kumfunga Yanga, ila cha ajabu hausemi Yanga imeshindwa kumfunga Simba
 
Nakwambia hivi, kwenye ligi tangu aje Nabi timu zimetoa sare zote. Simba na Yanga zikitoka sare unasema Simba imeshindwa kumfunga Yanga, ila cha ajabu hausemi Yanga imeshindwa kumfunga Simba
Labda ni Msimu wa mwaka Jana, mechi zote zimetoka share.. na hii ya kwanza Msimu huu.. licha ya hvyo Kuna hizi za FA na Ngao ya jamii, Makolo mmepasuliwa sana na Yanga, nn unataka kukataa
 
arsenal anaongoza lig ila hayupo UEFA , je anaeza mmudu nani pale UEFA ? kuongoza lig ni kuokota points nying kwa vibonde
Kwenye UEFA unataka nikutajie timu ambayo inaweza kufungwa na Arsenal.
1) Ac Milan
2)Dortumond
3)Club bruge
4) Tottenham
5) Chelesea
6) Benfica
 
Bado haibadilishi ukweli kuwa shirikisho ni kombe la vilaza walioshindwa CHAMPIONS LEAGUE.
Kama mpira unaujua na mifumo ya mashindano unayaelewa, basi ungekuwa na uwezo wa kutofautisha kati ya kufeli klabu bingwa na kuwa timu mbovu. Hakuna uhusiano kati ya kufeli kufuzu klabu bingwa na kuwa timu mbovu. Kuna timu zimepitia njia nyepesi na kuna timu zimepitia njia ngumu.
Na ndio maana nikakupa tu uhalisia kuwa kwenye kombe la shirikisho kuna timu ngumu na ndio maana bingwa wa klabu bingwa akakalishwa na bingwa wa shirikisho kwenye super cup.
 
Ifikie wakati tukubali tu ukweli; mashabiki wengi wa simba ni mbumbumbu.
Sasa unalia nn wee, si alisema Sope, shirikisho ni kombe la losers. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Labda ni Msimu wa mwaka Jana, mechi zote zimetoka share.. na hii ya kwanza Msimu huu.. licha ya hvyo Kuna hizi za FA na Ngao ya jamii, Makolo mmepasuliwa sana na Yanga, nn unataka kukataa
Unaposema sana utaje na idadi kama mimi nilivyotaja, usiseme kwa imagination. Mara ya kwanza ulisema Simba imefungwa na Nabi kwenye ligi, nikasema onyesha ushahidi. Sasa hivi umehamia kwingine kabla haujaleta ushahidi
 
Back
Top Bottom