Poleni. Kisheria, kama amejenga ukumbi bila kufuata utaratibu basi amefanya makosa.
Iko hivi, bilashaka maeneo hayo yatakuwa ni maeneo ya makazi; ambapo Sheria ina-suggest yanapaswa yawe na utulivu. Mtu akitaka kubadilisha matumizi (change of use) na kufanya biashara anapaswa aombe kibali cha kubadilisha matumizi kinachotanguliwa na tangazo litakalobandikwa ili kukaribisha maoni ya wakazi kuona kama wanaafiki au la.
Iwapo amejenga ukumbi kiholela mnaweza kufungua kesi Mahakamani. Cause of action itakuwa nuisance ambayo inaweza kuwafidia wakazi mlioathirika na kadhia hiyo.
Tafuteni Wakili awaongeze katika hili kwa kumuandikia demand notice ya kumtaka aweke vizuia sauti (sound proof); akishindwa mumpeleke Mahakamani akajibu tuhuma zinazomkabili.
Sijajua uko mkoa gani, lakini kama ungekuwa Dodoma bilashaka ningekuwa msaada. Nawatakia kila la kheri.