Wameru ni wakimbizi wa Kichaga

Wameru lugha yao ni kama kisiha na kimachame, utamaduni wao ni mchanganyiko wa kimasai na kichaga, mf; jando kama wamasai, ngoma kama wamasai, mahari kama wachaga urithi kama wachaga na mwanamke akijifungua lazima achinjiwe mbuzi au kondoo. Vyakula loshoro, ndizi, mtori, ngararum au ngararim za naasha.
 
Wameru n Wacha Mungu sana Alafu wana sheria Kali km Wamasai uwez kuta kijana wa kimeru Analewa lewa ovyo ovyo km vijana wa kichaga. Alafu dizain km wana ushirikiano sanaa Arusi za kimeru Watu wanatoa zawad hadi ratiba ya Shugul inaribika.
Sawa muwamba ngoma tumekusikia
 
Hapana, wachaga hawaelekei huko acha propaganda.
 
Na wahaya wana matabaka mengi mhaya wa Muleba lafudhi ya kihaya chake ni tofauti mhaya wa Misenyi
.... kwa kawaida jamii ambazo zimekuwa na permanent settlement kwa muda mrefu uwezakano wa lafudhi kubadilika ndani ya umbali mfupi ni kawaida kwa sababu muingiliano (social interaction) ni mdogo kuliko jamii ambazo zinahamahama.

Kwa mfano, mmasai aliyeko Mbarali si ajabu miaka miwili iliyopita alianzia Loitoktok (Kenya), kaingia Longido, Kibaya, all the way to Mbarali pori kwa pori; wanapiga kambi baada ya muda safari inaendelea. No wonder Kimasai cha Loitoktok ni kile kile kinachoongelewa Kibaya, Kiteto. The same applies to Wasukuma na jamii nyingine za maporini unlike jamii kama Wachaga, Wanyakyusa, Wahaya, Wabena, Tarime kule, n.k. ambao wamekuwa na makazi ya kudumu miaka na miaka kabla hata ya Vijiji vya Ujamaa vya Nyerere.
 
Wameru ni mchanganyiko wa Waarusha na Wamachame. Wamechukua sehemu zote mbili.
Halafu uchawi meru ni kitu kipya, sanasana wameleta wanyaturu ambao ni wafanyakazi wa kukata majani na kazi nyingine za shambani.
hao ndio wameleta magari ya "Jaguar' a.k.a Fisi.
 
Wanawake wa kimeru Wana tabia kama wale wa Machame a.k.a wapelestina?? Maana hapa ninakaribia kujicommit kwa mmeru
 
Wanawake wa kimeru Wana tabia kama wale wa Machame a.k.a wapelestina?? Maana hapa ninakaribia kujicommit kwa mmeru
Nasikia wanawake wa kimachame wana tabia ya kuua waume zao wakipata mali kuna ukweli gani kuhusu hilo
 
Hii taarifa pamoja na kwamba inaweza kuwa na jambo la kuchochea uchunguzi zaidi juu ya makabila yetu, ila inaacha ombwe kubwa juu ya asili ya varwa. Wameru sio jina lao, kwa asili wameru wanaitwa varwa-wingi, nrwa-umoja. Hili la wameru, ni jina la Kimasai lenye kumaanisha jua linakozama. Ukiwa Arusha ama Kilimanjaro, jua huchomoza mlimani Kilimanjaro na kuzama mlima Meru. Hivyo kutokana na hili, Wamasai wakawaita wakaaji wa eneo hili wameru, yaani watu wanaoishi kwenye mlima jua linakozama. Wazungu walipokuja wakaendeleza jadi hii ya kupotosha jina halisi la wakaazi wa ardhi hii ambao huitwa varwa.
Historia ya wameru inaelezwa kwa namna nyingi na waandishi tofauti tofauti kwa namna tofauti. Wako wanaoamini kuwa asili ya wameru ni milima ya Usambara na wanajenga hoja yao kwa kuangalia hulka, tabia na mwendo wa maisha ya varwa wa leo na kule usambaani. Wako ambao wanaamini varwa ni dialect ya kichanga, na hawa walikuwa ndugu ila baadaye ukazuka ugomvi wa kikoo na hivyo wakatawanyika. Kwenye vita hii zilizaliwa dialects nyingi, ikiwa ni pamoja na wapare ambapo maana yake ni waliopigwa na kupasuliwa, wakibosho, wa Machame na nk. Hoja ya pili ina nguvu zaidi kutokana ufanano uliopo kati ya dialects nyingi zilizo katika ukanda huu. Hivyo ni sahihi kusema varwa sio wachanga kwa sababu kwa asili hakuna kabila la kichanga. Kuna uwezekano mkubwa, hawa wanaojiita Wachaga leo ambao kwa hakika hawapo, wote shina lao ni milima ya Usambara. Na kwa hivyo, varwa ni kati ya vikabila vidogo vilivyozaliwa toka kabila kubwa la Usambaa kama matokeo ya vita miongoni mwa jamii hii.
 
Mimi nipo kwa wameru nimewauliza kuhusu hii kadhia wanabisha sana.Ila kwa jinsi Wameru walivyokuwa na ubinafsi pamoja na wivu hizi ni tabia za kichawi kabisa.Naunga mkono hoja!
Kabisa asee, kuna namna wapo
 
Mkuu asante kwa kujazia hii. Nimeipenda
 
Mkuu upo sawa, lakini hapo varwa nafikiri sahihi ni WARWA wengi, NRWA mmoja.
 
Wanyambo na wanyankole wa Uganda hawana tofauti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…