Wameru ni wakimbizi wa Kichaga

Wameru ni wakimbizi wa Kichaga

Hata uchagani ipo hiyo. Wauru hasa wanaotoka Kishumundu wanaonekana duni sana. Ndio maana ukimkuta mchaga yeyote akimwita mkishumundu hata kama ni kweli atakataa kabisa. Ntaielezea kwa kirefu siku zijazo
utanitag kaka
 
Wameru n Wacha Mungu sana Alafu wana sheria Kali km Wamasai uwez kuta kijana wa kimeru Analewa lewa ovyo ovyo km vijana wa kichaga. Alafu dizain km wana ushirikiano sanaa Arusi za kimeru Watu wanatoa zawad hadi ratiba ya Shugul inaribik

Wameru lugha yao ni kama kisiha na kimachame, utamaduni wao ni mchanganyiko wa kimasai na kichaga, mf; jando kama wamasai, ngoma kama wamasai, mahari kama wachaga urithi kama wachaga na mwanamke akijifungua lazima achinjiwe mbuzi au kondoo. Vyakula loshoro, ndizi, mtori, ngararum au ngararim za naasha.
Hapo umenena mkuu vyakula ni kwel huwa tunakula hivyo kuhusu mjamzito ni kwel pia big up
 
Wamashami mmbatana kasi ya hoteli fo...

Kwi kulemenlolya mmashami akumba subu neekumba wari efo murin?

Kazi eto gheiya Wakibosho ...

Eli nkindo mmiku akwa aleshiwia kyeri Alesha nla kindo shiketana kumi murin .

😂😂😂😂
Kwani wamashami wawee wandu wa kwi nuuri imanya kitaare waari ikumba subu murin(kimeru)
 
Hii taarifa pamoja na kwamba inaweza kuwa na jambo la kuchochea uchunguzi zaidi juu ya makabila yetu, ila inaacha ombwe kubwa juu ya asili ya varwa. Wameru sio jina lao, kwa asili wameru wanaitwa varwa-wingi, nrwa-umoja. Hili la wameru, ni jina la Kimasai lenye kumaanisha jua linakozama. Ukiwa Arusha ama Kilimanjaro, jua huchomoza mlimani Kilimanjaro na kuzama mlima Meru. Hivyo kutokana na hili, Wamasai wakawaita wakaaji wa eneo hili wameru, yaani watu wanaoishi kwenye mlima jua linakozama. Wazungu walipokuja wakaendeleza jadi hii ya kupotosha jina halisi la wakaazi wa ardhi hii ambao huitwa varwa.
Historia ya wameru inaelezwa kwa namna nyingi na waandishi tofauti tofauti kwa namna tofauti. Wako wanaoamini kuwa asili ya wameru ni milima ya Usambara na wanajenga hoja yao kwa kuangalia hulka, tabia na mwendo wa maisha ya varwa wa leo na kule usambaani. Wako ambao wanaamini varwa ni dialect ya kichanga, na hawa walikuwa ndugu ila baadaye ukazuka ugomvi wa kikoo na hivyo wakatawanyika. Kwenye vita hii zilizaliwa dialects nyingi, ikiwa ni pamoja na wapare ambapo maana yake ni waliopigwa na kupasuliwa, wakibosho, wa Machame na nk. Hoja ya pili ina nguvu zaidi kutokana ufanano uliopo kati ya dialects nyingi zilizo katika ukanda huu. Hivyo ni sahihi kusema varwa sio wachanga kwa sababu kwa asili hakuna kabila la kichanga. Kuna uwezekano mkubwa, hawa wanaojiita Wachaga leo ambao kwa hakika hawapo, wote shina lao ni milima ya Usambara. Na kwa hivyo, varwa ni kati ya vikabila vidogo vilivyozaliwa toka kabila kubwa la Usambaa kama matokeo ya vita miongoni mwa jamii hii.
Kikawaida hakuna wameru Tanzania, Meru ipo kenya ila baada ya ya WARWA kukimbia kutoka uchagani walienda chini ya mlima Meru hapo ndipo waliishi mda mrefu ndio wakaamua kujiita Wameru kwasababu wapo chini ya mlima Meru ila sio kwamba wao ni Wameru asili (my opinion)
 
Wameru ni mchanganyiko wa Waarusha na Wamachame. Wamechukua sehemu zote mbili.
Halafu uchawi meru ni kitu kipya, sanasana wameleta wanyaturu ambao ni wafanyakazi wa kukata majani na kazi nyingine za shambani.
hao ndio wameleta magari ya "Jaguar' a.k.a Fisi.
Wameru ni kabila kutoka kenya
 
So Wahaya ni kama Wachagga tuu.
Wote hawa wanashabihiana mazingira na chakula na wote mazingira yao nature yake ni bonde LA UFA. Wachaga mlima Kilimanjaro ni features za bonde LA UFA.Wahaya nao wanaishi jirani na bonde LA UFA.Msosi ni ndizi wote.Kupenda masifa wote Wahaya na Wachaga ni hivo hivo.
 
Kwani wote si wanaishi mazingira yanayofanana?je wanatofautiana tamaduni na maendeleo?
Wahaya walipata maendeleo hasa ya kielimu kabla ya wanyambo

Kama uwajuavyo Wahaya dharau zilikuwa ni nyingi dhidi ya wanyambo

Ikawepo kama chuki baina yao mpaka na wa leo

Na lafudhi zao ni tofauti sana lazima mnyambo umjue japo tamaduni wanafanana kwa asilimia kubwa

Na wilaya zinazobeba wahaya ni Muleba Misenyi na Bukoba wakati wanyambo wapo Karagwe na Kyerwa ila wakiongea wote wanaelewana tofauti ni lafudhi tu
 
Katika kabila lenye matabaka mengi Tanzania ni la Kichagga.

Na lugha zinabadilika kulingana na eneo ndio mana unakuta ukianza Rombo mpaka Siha lafudhi ni tofauti japo tunasikilizana vizuri lakini huwezi kujibu kama ulivyosemeshwa.

Katika kutaka kujua historia kidogo kwanini Wameru wanaongea lafudhi ya kufanana kabisa na Kichaga cha Machame?

HISTORIA YENYEWE

Wameru ni Wachagga wa Machame lakini walikuwa wachawi sana hapo zamani. Kipindi cha utawala wa Mangi ikafanyika opereseheni ya kuondoa na kuuwa wachawi wote. Ili kusafisha jamii dhidi ya ushirikina ile operation ilia wachawi wengi baadhi yao wakakimbilia milima ya Meru kutafuta makaazi huko.


Baada kukaa huko na kuongezeka na kuwa wengi na kwa sababu walikua kando kando ya mlima Meru wakaanza kujulikana kama Wameru.

Hadi leo ni kabila linalojulikana Tanzania kama Wameru. Ongea yao lafudhi yao maneno mengi, baadhi ya tamaduni zao haitofautiani na Kichaga.

Mwenye kutaka kujua zaidi afuatilie kuuliza,ila asiwaulize Wameru waulie wazee wa Kichaga. Ruksa kujazia.
Kipindi cha Mangi yupi sasa??
 
Wahaya walipata maendeleo hasa ya kielimu kabla ya wanyambo

Kama uwajuavyo Wahaya dharau zilikuwa ni nyingi dhidi ya wanyambo

Ikawepo kama chuki baina yao mpaka na wa leo

Na lafudhi zao ni tofauti sana lazima mnyambo umjue japo tamaduni wanafanana kwa asilimia kubwa

Na wilaya zinazobeba wahaya ni Muleba Misenyi na Bukoba wakati wanyambo wapo Karagwe na Kyerwa ila wakiongea wote wanaelewana tofauti ni lafudhi tu
Hao ni Wahaya tu! Lafudhi haibadilishi sana maana ktk Lugha.
Wachaga kwa mfano wapo ambao hawaelewani mfano wanaotoka Wilaya ya Rombo hawaelewani na wale wa machame kutoka Wilaya ya Hai!
 
Wote hawa wanashabihiana mazingira na chakula na wote mazingira yao nature yake ni bonde LA UFA. Wachaga mlima Kilimanjaro ni features za bonde LA UFA.Wahaya nao wanaishi jirani na bonde LA UFA.Msosi ni ndizi wote.Kupenda masifa wote Wahaya na Wachaga ni hivo hivo.
Sio kweli Wachagga na Wahaya ni makabila mawili tofauti izo ndizi na Bonde la ufa sio kigezo cha kuwafanya wawe sawa. Zingatia Bonde la ufa halijapita kwao tu lina coverage kubwa so usitudanganye.
 
Hao ni Wahaya tu! Lafudhi haibadilishi sana maana ktk Lugha.
Wachaga kwa mfano wapo ambao hawaelewani mfano wanaotoka Wilaya ya Rombo hawaelewani na wale wa machame kutoka Wilaya ya Hai!
Sio kwamba hawaelewani kuna baadhi ya maneno ndio hutofautiana itoshe kusema Wachagga pamoja na utofauti wa lugha huwezi msema mwingine kilugha na asielewe
 
Back
Top Bottom