Haipaswi kuwa hivyo, Sasa wananchi wanasimamiwa na nani? Wawakilishi wao bungeni wanawasaliti, wasimamia haki, nao wanawaruka. Mustakabali wa mwananchi uko wapi?
Tz haina 'Utawala Bora', na utawala bora ni pale mahakama inapokubaliana na waleta shitaka, iwe na uwezo wa kusema hilo suala ni batili, sio kukubaliana nao halafu inadai si hoja ya kubatilisha.
Utawala bora ni pale bunge linapoiuliza maswali serikali kwa niaba ya wananchi, na sio kukubali kila kinachofanywa na Serikali hata inapoonekana dhahiri, Serikali inaliburuta bunge, na mbaya zaidi, wabunge wanauonga mkono Serikali kwa manufaa yao binafsi sio ya uwakilishi wa wananchi.
Utawala bora, ni pale Serikali kabla ya kufanya lolote, kupata ridhaa ya wananchi, iwe moja kwa moja au kwa wawakilishi wao, na iwe kabla hata ya mazingumzo yoyote na wadau wowote wale. Sio iingie mpaka mkataba, halafu ndio inalazimisha wananchi wakubaliane nayo.
Utawala bora ni kwa bunge, mahakama n, Serikali na wananchi kuhakikisha hawafanyi lolote linaloenda kinyume na Katiba!