Wamiliki wa lodge kuweni serious

Kaka naona unaijua sana na hii sekta. Mungu akijalia mwisho wa mwaka huu nitaingia huko naomba nikutafute nipate madini.
Tiles za bafuni kuteleza na kuweka tiles za room unapachika washroom ni kosa kiufundi, halafu mopa ni 2500 hadi 3000 walau ukikaweka bafuni mteja akioga atajiongeza asukume hata maji lakini mtihani sana
 
Wamiliki wawe wanawapa short training wafanyakazi wao wajue hawapo hapo ku-facilitate fumanizi na umbeya.

Kuna jamaa amepata usumbufu toka kwa mtu asomjua akimtuhumu kutembea na mumewe baada ya kupewa namba toka Kwa wafanyakazi wa hiyo hotel .
Eti alienda na picha kwenye Simu akiuliza Huyu anakujaga hotel hii na Mwanamke, wafanyakazi wakajichanganya wakasema ndiyo,
Akawaambia nipeni namba ya huyo mwanamke wakatoa, Dada wa watu hana analojua anashangaa anatumiwa sms kwa mtu ambae hamjui kabisa.

Wapeni elimu ya usiri na privacy ya wateja.

Na itawasaidia kuepukana na unnecessary cases za kuitwa polisi na mahakamani Kama mashahidi.

Avoid giving information voluntarily because it can cost you much.
 
Pesa zangu nyingi zinaishia kwenye kulala, kama nalipa mwenyewe something decent…. From 50k na kuendelea. Kama wanalipa kazini wana rate zao i’ll get something better.

Japo ni kweli vikero kero vipo here and there. Kama kuna kitu siwezi kumsikiliza mtu hata awe nani ni anipe ushauri wa kucut cost kwenye malazi. Mi nateseka kutafuta pesa nilale kama mkimbizi! Na kwasisi wanawake usalama ni kipaumbele, bora miamba wanaweza pambana.

Unless kusiwe na a decent place, kuna wilaya nilienda…. Hizo lodge 🙆🏼‍♀️ nzuri kuliko zote ni elfu 20, ikabidi niende kugonga hodi kanisani, wana hostel walinihifadhi nikamaliza mambo yangu nikaondoka.
 
Taulo je???
 
Kigoma nililala ka lodge kapya, kagorofa hivi… kako barabara kama unaenda lake Tangayika hotel, Kasafiiii, very decent kwa 40 au 45k sikumbuki vizuri.

Mmiliki apewe maua yake, sijui sa hivi ina hali gani maana imepita karibu miaka 2.
 
😂😂😂😂 haaaaa!
 
Ahahaha Kidume unabebeshwa ndoo unaenda kuchota maji kisimani daah!! hao jamaa hawako serious
 
Nimechek mpaka watoto wakaniuliz unachek nn baba, imebidi nizuge nisema picha zinu hizi kwenye simu zinanichekesha.!!!!!
Dah.! 3 hrs ndani ya chooo.! Umenifurahisha as if comedy clip kumbe ndo maisha yanaendelea.
Tena choo chenyewe kidunchuuu 😂😂😂😂 nimecheka hadi nimelia, ila nimemuonea huruma sana.
 
Unambishia tu bure, nyingi hapo ulizotaja ni
🗑️🚮

Sasa kama NAM jamani? Dodoma hotel? Dear mama???? Golden crown??????? Hata nashera na morena ni nzuri ila sio kwa thamani ya pesa wanayochaji, tena kama Morena kuna baadhi ya vyumba ukioga maji hayasogei/hayaendi yanajaa!!!!! Nashera vyumba ni vingi sana na havijai…. So unaweza pewa chumba hakijatumika wiki, na hawapiti kuangalia usafi, ukikipewa jiandae na chafya.

Maramia ungemtajia Rafiki na yule jirani yake… Opposite na shoppers. Nisiyoijua ni hiyo Bestern ninini sijui, ndio hiyo mpya ya area D???

Hatukosoi biashara za watu kwa ubaya wamiliki wafuatilie, wateja hatulimi pesa!
 
Wadanganye washamba wenzio labda.....Hoteli zenye hadhi ya nyota nne kama St Gaspar(yenye presidential suite ndani),Morena,Dodoma Hotel,Royal Village,Best Western City Hotel unasema takataka 😀😀😀
Huyo alienda kwenye guest houses ndio akakutana na hizo changamoto sio Hoteli. Tofautisha hadhi ya guest house,lodge na Hotel
 
Best Western City Hotel ipo katikati ya mji pembeni ya TRA.

 
Hapo kwenye kitanda kupiga kelele kwangu ndo kero namba moja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…