Wamiliki wa mabasi wapewa wiki moja kurejea stendi ya Magufuli

Jannatul Firdaus

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
446
Reaction score
1,113
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amewapa wamiliki na waendeshaji wa Kampuni za Mabasi makubwa ya Mikoani wiki moja kuhakikisha wanaanza kurejesha huduma zao katika Stendi ya Magufuli, isipokuwa kampuni 6 ambazo tayari zina vibali vya kushushia kati kati ya mji, ikiwa ni hatua ya Serikali kupunguza msongamano wa magari katikati ya Jiji la Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Chalamila amesema mabasi hayo yanapaswa kuanzia na kumalizia safari katika Kituo cha Magufuli, badala ya kuingia katikati ya jiji kwa ajili ya kupakia na kushusha abiria.

Amesema wamiliki na waendeshaji wa mabasi hayo wanapaswa kutumia muda kuanzia sasa hadi Agosti 17, 2026 kuhakikisha magari yao yanaanza kutumia Stendi ya Magufuli, huku utekelezaji wa utaratibu huo ukianza rasmi baada ya tarehe hiyo.

Kwa mujibu wa Chalamila, abiria wanaofikishwa Stendi ya Magufuli wataendelea na safari zao kuelekea maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam kwa kutumia usafiri wa ndani, ikiwemo mabasi ya mwendokasi, daladala, bajaji na pikipiki au 'shuttle' ambazo zitatolewa na kampuni za mabasi husika

Chalamila amesema hatua hiyo pia inalenga kulinda fursa za ajira na biashara kwa waendeshaji wa usafiri wa ndani, akisema mabasi makubwa yanapoingia katikati ya jiji yanaingilia shughuli zinazoweza kufanywa na wadau wengine katika mnyororo wa usafirishaji.

Your browser is not able to display this video.
Pia soma ~ Ushauri wangu: Mabasi ya abiria ya mikoani yaishie Mbezi Magufuli
 
PM alisema sio lazima na ni kweli sio lazima.

Kama shida yenu ni Mapato wapeni control number wakalipe.

Mnajenga mamiradi ya kijinga na ya kukurupuka harafu mnalazimisha watu walale? Sio kazi ya serikali kufanya biashara
 
Chalamila amevimbiwa na mshahara wa kodi za wananchi ambao ni abiria.

Chalamila hafahamu adha inayowapata wananchi wenye mizigo waliyokuja nayo kupunguza ukali wa maisha. Anataka wapate usumbufu na gharama zingine kufikisha mikungu ya ndizi, viazi, vitunguu walivyonunua kupunguza gharama za maisha

Chalamila yeye akitoka kwao kijijini akutumia basi, atapokewa na dereva wake ambaye anaendesha V8 gari, mafuta, mshahara na kiyoyozj walichomlipia wananchi kupitia kodi

Chalamila anaumia sana basi toka mikoani likichukua abiria au kushusha abiria katika vitongoji vyao wanavyokaa ktk jiji pana, kubwa lililotapakaa kwa kilometa kibao.

Chalamila anataka wananchi hao wapate adha ndiyo furaha kuwa yeye ni kiongozi wa matamko na bila kujali kama matamko hayo yana athari kwa furaha na maisha ya watu walipa kodi

Chalamila kuna shida gani magari kuingia na kutoka kituo cha Magufuli baada ya kupakia na kuteremsha watu kituo cha Magufuli?

CHALAMILA AKICHEZA SINGELI


View: https://m.youtube.com/watch?v=7LXGiCdkI2w
 
Sisi wa Mbagala Rangi tatu tunapenda Arusha mmetufikiria itakuwaje na Hali hatuna magari?
 
Mate so mnayoendelea kuwatafutia Watanzania na kuuwa biashara zao sijui mnataka magari yenu ndiyo ya single stendi ya Magu ili mnufaike ama ni baada ya kuona Watanzania wananufaika na ubunifu ulioondoa mate so kwao ?
 
Solution ni kuwa na Zonal Bus Stands. Magufuli terminal tu haitoshi japo imejengwa kwa standard kubwa.

Ia hii ya Shekilango hadi Kagera ni kukosa mipango tu, kila mahali ni private stands, mmbo ya hovyo haya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…