Wamiliki wa mabasi wapewa wiki moja kurejea stendi ya Magufuli

PM alisema sio lazima na ni kweli sio lazima.

Kama shida yenu ni Mapato wapeni control number wakalipe.

Mnajenga mamiradi ya kijinga na ya kukurupuka harafu mnalazimisha watu walale? Sio kazi ya serikali kufanya biashara

Halafu umejisahau ni wewe chawa humu ndio huwa unasifia hayo mamiradi ukisema kajenga Samuya..

Mfano kuna stendi humo katika huo uzi uliopandisha wanaokaa huko wanashangaa stendi kubwa inajengwa kwenye eneo lenye watu wachache mwisho wake imegeuka kituko.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amewapa wamiliki na waendeshaji wa Kampuni za Mabasi makubwa ya Mikoani wiki moja kuhakikisha wanaanza kurejesha huduma zao katika Stendi ya Magufuli, isipokuwa kampuni 6 ambazo tayari zina vibali vya kushushia kati kati ya mji, ikiwa ni hatua ya Serikali kupunguza msongamano wa magari katikati ya Jiji la Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Chalamila amesema mabasi hayo yanapaswa kuanzia na kumalizia safari katika Kituo cha Magufuli, badala ya kuingia katikati ya jiji kwa ajili ya kupakia na kushusha abiria.

Amesema wamiliki na waendeshaji wa mabasi hayo wanapaswa kutumia muda kuanzia sasa hadi Agosti 17, 2026 kuhakikisha magari yao yanaanza kutumia Stendi ya Magufuli, huku utekelezaji wa utaratibu huo ukianza rasmi baada ya tarehe hiyo.

Kwa mujibu wa Chalamila, abiria wanaofikishwa Stendi ya Magufuli wataendelea na safari zao kuelekea maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam kwa kutumia usafiri wa ndani, ikiwemo mabasi ya mwendokasi, daladala, bajaji na pikipiki au 'shuttle' ambazo zitatolewa na kampuni za mabasi husika

Chalamila amesema hatua hiyo pia inalenga kulinda fursa za ajira na biashara kwa waendeshaji wa usafiri wa ndani, akisema mabasi makubwa yanapoingia katikati ya jiji yanaingilia shughuli zinazoweza kufanywa na wadau wengine katika mnyororo wa usafirishaji.

Samia ndiyo umeamua kuja kwa ID hii, ile ya zamani hautaitumia tena?
 
isipokuwa kampuni 6 ambazo tayari zina vibali vya kushushia kati kati ya mji, ikiwa ni hatua ya Serikali kupunguza msongamano wa magari katikati ya Jiji la Dar es Salaam.
1. Ester luxury coach- Dr Mwigulu
2. ABOOD BUS- MBUNGE
3. SHABBY BUS - MBUNGE
4. BM COACH - Dr Kimei
Bm sio wa DR kimei, umeingia chaka
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amewapa wamiliki na waendeshaji wa Kampuni za Mabasi makubwa ya Mikoani wiki moja kuhakikisha wanaanza kurejesha huduma zao katika Stendi ya Magufuli, isipokuwa kampuni 6 ambazo tayari zina vibali vya kushushia kati kati ya mji, ikiwa ni hatua ya Serikali kupunguza msongamano wa magari katikati ya Jiji la Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Chalamila amesema mabasi hayo yanapaswa kuanzia na kumalizia safari katika Kituo cha Magufuli, badala ya kuingia katikati ya jiji kwa ajili ya kupakia na kushusha abiria.

Amesema wamiliki na waendeshaji wa mabasi hayo wanapaswa kutumia muda kuanzia sasa hadi Agosti 17, 2026 kuhakikisha magari yao yanaanza kutumia Stendi ya Magufuli, huku utekelezaji wa utaratibu huo ukianza rasmi baada ya tarehe hiyo.

Kwa mujibu wa Chalamila, abiria wanaofikishwa Stendi ya Magufuli wataendelea na safari zao kuelekea maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam kwa kutumia usafiri wa ndani, ikiwemo mabasi ya mwendokasi, daladala, bajaji na pikipiki au 'shuttle' ambazo zitatolewa na kampuni za mabasi husika

Chalamila amesema hatua hiyo pia inalenga kulinda fursa za ajira na biashara kwa waendeshaji wa usafiri wa ndani, akisema mabasi makubwa yanapoingia katikati ya jiji yanaingilia shughuli zinazoweza kufanywa na wadau wengine katika mnyororo wa usafirishaji.

Mabasi si ya Chalamila, wakati umefika wamuachie huyo Chalamila aweke mabasi yake.
 
Nadhani kwa dar es laam kungekuwa na standi ya mabasi kila kanda

Mabasi ya kusini yaanze na kuishia kongowe huko.
Mabasi yanayopita Morogoro yaishie na kuanzia kibaha.

Mabasi ya kaskazini yaanzie na kuishi mapinga
We jamaa. Nikiwa naenda Arusha nikapande basi mapinga na hizi hela hela za dar? Upo serious
 
Hizo stendi mpya bila serikali kukomalia matumizi yake,hakuna angeenda huko kwa hiari hivyo zote tu zingekuwa magofu.

Nyegezi nayo ilianza kwa mbinde sana mwaka 2005 ikisemwa ni nje ya mji.
 
Tuanze na Malori, yaishie Pwani kwenye Dry port , badala ya kupambana na wenye mabasi, kwenda Mbezi!​

Back
Top Bottom