Wamiliki wa mabasi wapewa wiki moja kurejea stendi ya Magufuli

Kuna siku wiki mbili zilizopita, nilifanya kautafiti kadogo kwenye barabara ya Mandela na barabara ya Kilwa.

Kutoka Ubungo - Kijazi Interchange mpaka Tazara - Mfugale Flyover nimekutana na malori matatu yameharibikia na yameegeshwa barabarani, pamoja na daladala 2 zimeharibikia barabarani.

Wakati huo huo, kuna malori 11 yalikuwa yanahangaika kuingia barabara kuu kutoka kwenye ICDs, viwanda, vituo vya mafuta na parking za malori, vyote hivyo vilivyopo kando ya barabara hii kuu ya Mandela.

Nikaja kukutana na matukio hayo hayo kwenye barabara ya Kilwa kutoka daraja la juu la Uhasibu mpaka Kisemvule.

Ni kwa nini Kwala haitumiki ipasavyo!!??
 
isipokuwa kampuni 6 ambazo tayari zina vibali vya kushushia kati kati ya mji, ikiwa ni hatua ya Serikali kupunguza msongamano wa magari katikati ya Jiji la Dar es Salaam.
1. Ester luxury coach- Dr Mwigulu
2. ABOOD BUS- MBUNGE
3. SHABBY BUS - MBUNGE
4. BM COACH - Dr Kimei
 
Chanika,chamazi,kigamboni, na sehemu nyingine Kuna ofisi mabasi yanatokea huko kuwarahisishia walio nnje ya mji, hizo nazo zisifanye kazi?? Au sijaelewa, kama ni hivyo wasafiri tutalia sana
 
Leo ndio nimejua mmiliki wa BM
 
Ivii chalamila amewai kuishi mbande kisewe alafu saa 11 alfajir awe hapo magufuri bus stand kwa ajiri ya safari...

Kwa mtazamo wangu mabasi yalikua yanasaidia sana mfano unafika hapo magufuri then basi linakuleta mpaka shekilango then unaenda zako mabibo kwa miguu ama hapo sinza madukani

Unajua chalamila anatakiwa awe anafikilia mara mbili mbili kabla ya kukurupuka na kuja kuzungumza na umma bila taarifa za kitafiti
 
Asiingilie biashara za watu, weka siasa kando wafu wanatafuta pesa kwa jasho sio kama nyie mnaotuibia kodi zetu
 
Uhuni mtupu, aseme tu ana bajaji na daladala zake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…