Uchaguzi 2020 Wana ACT-Wazalendo wamuandikia Barua Msajili wa Vyama vya Siasa kumwambia Maalim na Zitto wamepoteza sifa za kuwa wanachama wa ACT-Wazalendo

Uchaguzi 2020 Wana ACT-Wazalendo wamuandikia Barua Msajili wa Vyama vya Siasa kumwambia Maalim na Zitto wamepoteza sifa za kuwa wanachama wa ACT-Wazalendo

Kipi kinamzuia Membe kufanya kampeni hadi sasa, kama sio anatumika na ccm kuchelewesha upinzani?
Kumbe jibu unalo hafanyi kampeni hana mvuto [emoji116] [emoji116] [emoji116]
Membe atagawa kura za upinzani kwa mvuto gani alionao?
Sasa Kama hana mvuto anatumika Vipi kuchelewesha upinzani
Kama Hana mvuto ana haja gani kufanya kampeni
 
Sio kutengenezewa Bali viongozi wenyewe mwenyekiti na kiongozi wa chama
Walitunga Katiba wenyewe na waliweka vipengele kadhaa wakiamini watavifuata wao na wanachama wao.
Sasa kwa maslahi yao Binafsi wanapindua pindua Katiba.

Halafu Maalim huu upuuzi wakujiamulia mambo ya ovyo inaonekana ni utamaduni wake
2015 kweli alishinda kwa mujibu wake Ila papara zake zikampeleka kujitangaza Mshindi kakosa vyote
Kazunguka ulaya Huko kaishia kupiga picha ukumbi mtupu kule UN
Akaja na story kibao

Kwani hapakuwahi kuwepo Serikali ya maridhiano/mseto huko Zanzibar na Maalimu Seif kupewa Cheo sikumbuki vizuri kama ni cha umakamu au nini sijui? Je, wewe hilo umelisahau ndio maana unamchukulia Maalimu Seif as if ni mkurupukaji!!
 
These n!99as are outright NUTS.

Nikukaribishe ndani kwangu halaf uje kusema mimi si baba mwenye nyumba?..nakuhakikishia hio ndo siku ungekifunza kutofautisha ncha ya kisu na ncha ya mkuki

Huyu waziri wa zamani anajishusha sana. Hivi ni hela ya kampeni alikosa au ni kibaraka wa mabepari wa kiafrika?
 
Kumbe jibu unalo hafanyi kampeni hana mvuto [emoji116] [emoji116] [emoji116] Sasa Kama hana mvuto anatumika Vipi kuchelewesha upinzani
Kama Hana mvuto ana haja gani kufanya kampeni

Ccm walitegemea cdm watampokea Membe, au kuungana na ACT yake ili wamtumie. Ila sasa hivi wanamtumia kutaka kumtoa Seif kwenye reli.
 
21/10/2020

Msajili wa Vyama vya Siasa Tanzania,
Kivukoni, Ilala CBD, 1 Shabaani Robert Str.,
11101 Dar Es Salaam, S. L. P 63010, Tanzania.
info@orpp.go.tz


Mheshimiwa Msajili,

YAH: UKIUKWAJI WA KATIBA YA CHAMA CHA ALLIANCE FOR CHANGE AND TRANSPARENCY (ACT WAZALENDO), 2015 TOLEO LA 2020.

UKIUKWAJI WA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, 1977.

UKIUKWAJI WA KATIBA YA ZANZIBAR, 1984.

UKOSEFU WA SIFA ZA UANACHAMA KWA NDUGU MAALIM SEIF HAMAD NA NDUGU ZITTO ZUBERI KABWE.


Sisi, Crytus Adrian Kabete (Kadi Na. 1010540) na Nasma Ramadhan Assedy (Kadi Na. 1008440) ni wanachama hai wa Chama cha ACT Wazalendo. Ndugu Msajili, tunapenda kuchukua nafasi kuleta kwako taarifa rasmi kama wanachama na wapiga kura walioandikishwa kuhusu masuala ambayo kwa kiasi kikubwa ni uvunjaji na ukiukwaji wa Katiba ya Chama chetu, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Katiba ya Zanzibar, Sheria ya Vyama vya Siasa, 1992 na Sheria za Uchaguzi. tunaomba kuwasilisha taarifa hiyo kama ifuatavyo;

1.0 IBARA YA KATIBA YA ACT WAZALENDO ILIYOVUNJWA

1.1 Ibara ya 13(4)
ya Katiba ya Alliance for Change and Transparency (ACT Wazalendo) ya 2015, Toleo la 2020 inaeleza kwamba, “pamoja na sababu nyingine kama zilivyoelezwa katika katiba hii na kanuni zitakazotungwa na Halmashauri Kuu, mwanachama yeyote ambaye atasaidia, kushawishi, kujiunga, kutoa tamko la kuunga mkono chama kingine au mgombea wakati Chama kimeweka mgombea kwenye uchaguzi wowote kwa mujibu wa Sheria ya Nchi atakuwa amepoteza uanachama wa ACT”.

1.2 Kwa mujibu wa Katiba ya Alliance for Change and Transparency (ACT Wazalendo) ya 2015, Toleo la 2020 Ibara ya 13(1)(iv) mwanachama atakoma kuwa mwanachama ikiwa atapoteza sifa za uanachama kama zilivyoainishwa kwenye Katiba hiyo.

2.0 VITENDO/KAULI ZA UVUNJIFU WA KATIBA YA ACT WAZALENDO

2.1 Ndugu Msajili
, Chama cha ACT Wazalendo kupitia Mkutano Mkuu wa Taifa kilimpendekeza na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilimteua Ndugu Bernard Membe kuwa Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa sababu uamuzi wa kusimamisha mgombea wa nafasi ya Urais ni uamuzi wa msingi (core function) ya Mkutano Mkuu wa Taifa hakuna kikao au chombo kingine chochote chenye mamlaka ya KUTENGUA au KWENDA KINYUME na maamuzi hayo isipokuwa Mkutano Mkuu wa Taifa wenyewe. Mkutano Mkuu wa Taifa haukutoa azimio maalum kwamba endapo Mgombea wetu hatafanya kampeni basi viongozi wa kitaifa wamuunge mkono Mgombea wa Chama kingine.

2.2 Ndugu Msajili, kwa mujibu wa kifungu cha 6A(3) na (4) cha Sheria ya Vyama vya Siasa, 1992 kama ilivyorekebishwa na Sheria ya Marekebisho, G.N. 1 ya 2019 Mkutano Mkuu na Kamati Kuu wa/ya Chama cha siasa HAZIRUHUSIWI kukasimisha madaraka yake ya msingi (core functions) kwa chombo kingine chochote. Kifungu hicho kinasomeka hivi;

A political party general meeting and national executive committee or any similar organ shall not delegate their core functions prescribed in the party constitution

For the purpose of subsection (3), core functions means-

(a) in the case of the party national general meeting, be enactment and amendment of party constitution, election of party national chairman, deputy national chairman and nomination of presidential candidate..


2.3
Maelezo yaliyotolewa kwenye vyombo vya habari na Ndugu Maalim Seif Shariff Hamad na Ndugu Zitto Zuberi Kabwe kwamba Kamati ya Uongozi iliketi na kuamua kwamba Chama kimuunge mkono Mgombea mwingine wakati tuna mgombea wetu ni upotoshaji kwani maamuzi hayo yanapaswa kutolewa na Mkutano Mkuu wa Taifa na sio Kamati ya Uongozi au chombo kingine chochote.

2.4 Kitendo cha Ndugu Maalim Seif Shariff Hamad na Ndugu Zitto Zuberi Kabwe kutoa matamko hadharani kwamba wanamuunga mkono Ndugu Tundu Antipas Lissu ambaye ni Mgombea wa Urais kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ni ukiukwaji wa dhahiri wa Katiba ya Chama cha ACT Wazalendo.

Ushahidi wa kauli aliyotoa Ndugu Maalim Seif Shariff Hamad unapatikana:

chini ya kichwa cha habari “MAALIM AMVAA MEMBE, JPM ATOA DARASA LA USHINDI CCM”.

Pia, habari inayomwonyesha Ndugu Maalim Seif Shariff Hamad akiwa anamnadi Ndugu Tundu Antipas Lissu inapatikana:

.


Tarehe 16/10/2020 Ndugu Zitto Zuberi Kabwe alitoa na kusambaza Tamko lenye kichwa cha habari, “Nitampigia Kura Tundu Lissu ili Awe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”.

3.0 UTEUZI WA MGOMBEA URAIS KWA TIKETI YA ACT WAZALENDO
3.1 Ndugu Msajili
, mamlaka ya kumteua Mgombea wa nafasi ya Urais kwa mujibu wa Ibara ya 72(1)(f) ya Katiba ya Alliance for Change and Transparency (ACT Wazalendo) ya 2015, Toleo la 2020 ni Mkutano Mkuu wa Taifa wa Chama hicho ambao hufanyika mara moja kila baada ya miezi sitini.

3.2 Ndugu Msajili, kama ilivyoelezwa hapo juu, Chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT Wazalendo) kupitia Mkutano Mkuu wake kilimteua Ndugu Bernard Membe kuwa Mgombea wake wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Bernard Membe bado ni Mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya ACT Wazalendo. Mgombea huyu hajajitoa kwenye uchaguzi huu.

3.3 Ndugu Msajili,
vilevile Chama Cha ACT Wazalendo hakijatoa taarifa yoyote kwa Tume ya Uchaguzi kujiondoa kumpendekeza Ndugu Bernard Membe kama Mgombea. Bado Ndugu Bernard Membe amependekezwa na Chama cha ACT Wazalendo.

4.0 UKOMO WA UANACHAMA WA ACT WAZALENDO
4.1 Ndugu Msajili,
imeelezwa hapo juu kwamba kwa mujibu wa Katiba ya Alliance for Change and Transparency (ACT Wazalendo) ya 2015, Toleo la 2020 Ibara ya 13(1)(iv) mwanachama atakoma kuwa mwanachama ikiwa atapoteza sifa za uanachama kama zilivyoainishwa kwenye Katiba yetu.

4.2 Ndugu Msajili, Ibara ya 13(4) ya Katiba ya ACT Wazalendo ya 2015, Toleo la 2020 imevunjwa na Ndugu Maalim Seif Hamad na Ndugu Zitto Zuberi Kabwe kwa makusudi. Hakuna Mkutano Mkuu wa Taifa uliofanyika au uwepo wa Maazimio Maalum yaliyofanywa na Mkutano Mkuu wa Taifa uliomteua Ndugu Bernard Membe kuwa Mgombea kwamba wanachama wanaruhusiwa kukisaidia au kumsaidia, kushawishi, kujiunga, kutoa tamko la kuunga mkono chama kingine au mgombea wakati Chama kimeweka mgombea kwenye uchaguzi wowote kwa mujibu wa Sheria ya Nchi.

4.3 Ndugu Msajili,
vitendo vya Ndugu Zitto Zuberi Kabwe na Maalim Seif Hamad ni ukiukaji wa Katiba ya ACT Wazalendo na matokeo yake kwa mujibu wa Ibara ya 13(4) ya Katiba yetu ni kukoma kwa uanachama.

5.0 UTARATIBU WA USHIRIKIANO WA KISIASA (COALITION) KATI YA VYAMA VYA SIASA VILIVYOSAJILIWA.
5.1 Ndugu Msajili,
Sheria ya Vyama vya Siasa inaruhusu vyama kushirikiana kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa. Hata hivyo Ndugu Zitto Zuberi Kabwe tarehe 16/10/2020 alishutumu ofisi yako kwa kutamka maneno yafuatayo, “kutokana na uwepo wa sheria kandamizi ya Vyama vya Siasa ushirikiano wa kisheria tumeona hauna maana kwetu kama Chama kwani Msajili wa Vyama hawezi kuidhinisha jambo linalokwenda kuindoa CCM madarakani”.

5.2 Ndugu Msajili,
ni wazi kwamba ofisi yako haina mamlaka ya kuidhinisha au kutoidhinisha Mkataba wa Ushirikiano (Coalition Agreement) baina ya Vyama vya Siasa. Kwa sababu hiyo madai kwamba Msajili wa Vyama hawezi kuidhinisha jambo linalokwenda kuindoa CCM madarakani” hayakuwa na msingi wowote ila yalilenga kuhalalisha uvunjifu wa Katiba yetu ya ACT Wazalendo kama ilivyojidhihirisha.

5.3 Ndugu Msajili, maamuzi ya ushirikiano na vyama vingine vya siasa ikiwa ni pamoja na kuunganisha Chama kwa mujibu wa Katiba ya ACT Wazalendo ni moja ya maamuzi muhimu ambao lazima ufanywe na Mkutano Mkuu wa Taifa na chombo hicho hakiwezi kukasimisha madaraka hayo kwa chombo kingine bila kufuata utaratibu uliwekwa na Katiba yetu.

5.4 Ndugu Msajili, kwa mujibu wa Ibara ya 18(i) ya Katiba ya ACT Wazalendo Kamati ya Uongozi ya kila ngazi au Kamati Kuu Taifa zinaweza kukasimu baadhi ya madaraka kwa Sekretarieti yake kwa azimio la wingi wa kura za wajumbe wa kikao. Mkutano Mkuu unaweza kukasimu kwa Halmashauri Kuu baadhi ya madaraka yake, lakini kwa azimio maalumu kwa ajili hiyo. Lazima kuwe na Azimio Maalum.

6.0 MAMLAKA YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA
6.1
Kwa mujibu wa Katiba ya ACT Wazalendo mwanachama yeyote anayekiuka Katiba hiyo anaweza kufukuzwa au kupewa adhabu nyingine kama onyo au karipio. Mwanachama ambaye anakosa sifa ya uanachama kwa mujibu wa Katiba ya ACT Wazalendo uanachama wake UNAKOMA.

6.2 Ndugu Maalif Seif Shariff Hamad
na Ndugu Zitto Zuberi Kabwe wote wamekosa sifa za uanachama wa ACT Wazalendo hivyo sio wanachama wala viongozi wetu.

6.3 Ndugu Msajili, kwa mujibu wa kifungu cha 6A(2) cha Sheria ya Vyama vya Siasa, 1992 kama ilivyofanyiwa marekebisho, Vyama vyote vya Siasa vinapaswa kuongozwa na kusimamia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, Katiba ya Zanzibar, Katiba za Vyama hivyo na misingi ya Demokrasia na Utawala Bora. iliyo chini ya uangalizi wako.

6.4 Ndugu Msajili, kutokana na ukiukwaji wa wazi wa Katiba ya ACT Wazalendo na hivyo Ndugu Maalim Seif Shariff Hamad na Ndugu Zitto Zuberi Kabwe uanachama wao KUKOMA, unayo mamlaka chini sheria ya Vyama vya Siasa, 1992 vifungu vya 5(a) na 5B(1) kama msimamizi wa sheria hiyo na utekelezaji wake wa jumla. Chini ya Sheria hiyo ya Vyama vya Siasa, vifungu vya 8(C)(1) & (2), unaweza kuitisha rejesta (register) ya majina ya viongozi na wanachama wa ACT Wazalendo na kuhakikisha kwamba majina yao yameondolea kwani wamekosa sifa za uanachama.

HITIMISHO:

Ndugu Msajili,
suala la ukomo wa uanachama wa Ndugu Maalim Seif Shariff Hamad na Ndugu Zitto Zuberi Kabwe sio suala la wanachama wa ACT Wazalendo pekee. Suala hili linamhusu mtu yeyote ambae ni raia wa Tanzania na haswa mpiga kura kwani wawili hawa ni wagombea na viongozi wa juu ndani ya Chama chetu. Kitendo chao cha kukiuka Katiba yao kwa kushawishi wapiga kura kumchagua mgombea mwingine wakati Chama chetu kina Mgombea kwa mujibu wa sheria za nchi kimeleta sintofahamu ndani ya Chama kwani;

kimesababisha baadhi ya wagombea wetu kukosa kuungwa mkono kwa sababu tunaonekana hatuna msimamo,

wagombea wengi wa udiwani na ubunge ambao walijitoa kwa hali na mali na kuingia gharama kubwa kujiandaa na uchaguzi wamevunjika moyo sana kwa kauli za viongozi hao.

Kauli zao zitawasababisha baadhi ya wapiga kura wasusie kupiga kura kwa Mgombea wetu, Ndugu Bernard Membe, kwa kuamini hata shinda kwani tayari hata Chama chake hakimuungi mkono hivyo ni kuwanyima haki yao ya msingi ya kuchagua.


Chama chetu kimekuwa kikijipambanua kusimamia misingi ya utawala bora na uwazi lakini kwa kitendo ambacho kimefanywa na viongozi hawa wakuu ni wazi kabisa kwa makusudi wameamua kuachana na misingi hiyo kwa maslahi yao binafis ya kutafuta uongozi kwa njia yoyote. Hii sio demokrasia tunayoipigania na matokeo yake ni kuvuruga Chama, wanachama na viongozi kwa ujumla. Ni matarajio yetu kwamba suala hili utalipa uzito unaostahili na kulifanyia kazi kwa haraka.

Tunaomba kuwasilisha kwako,

Crytus Adrian Kabete (Kadi Na. 1010540) na
Nasma Ramadhan Assedy (Kadi Na. 1008440)

Nakala:


Mwenyekiti,
Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania (NEC),
Dodoma.

Mwenyekiti,
Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC)
Zanzibar.

Mwanasheria Mkuu, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dodoma.


Mwanasheria Mkuu, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,
Zanzibar.
Ccm wanahangsika sana

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
 
Kwani hapakuwahi kuwepo Serikali ya maridhiano/mseto huko Zanzibar na Maalimu Seif kupewa Cheo sikumbuki vizuri kama ni cha umakamu au nini sijui? Je, wewe hilo umelisahau ndio maana unamchukulia Maalimu Seif as if ni mkurupukaji!!
Serikali ya maridhiano ipo mpaka Leo. Huyu Maalim Seif si alisusa mpaka Leo cheo cha makamu WA kwanza wa RAIS kipo wazi
Sasa Kama sio ukurupukaji ni nini mkuu
 
Comments ziko humu zinaonyesha kabisa kwamba wapinzani wakipewa nchi ndiyo watakuwa wavunjaji wakubwa Wa katiba kuliko watawala waliopo.

Bora zimwi likujualo kuliko hilo la pembeni
 
Ccm walitegemea cdm watampokea Membe, au kuungana na ACT yake ili wamtumie. Ila sasa hivi wanamtumia kutaka kumtoa Seif kwenye reli.
Huyo Membe wanajuana na Zito maana Membe ni kinara wa kuanzishwa hiyo ACT enzi za JK. Maalim Seif ndio hajui kinachoendelea humo ACT, lakini Zito na Membe wanajua kila kitu kuhusu uwepo wa hicho chama.
Wanaotaka kumtoa kwenye reli Maalim Seif ni Membe Wakishirikiana na zitto si ndio mkuu
Sasa inawezekanaje
Huku zitto akiwa anawahitaji wa Zanzibar kujenga chama chao na Membe [emoji116]
Sasa inawezekanaje zitto aweze kujenga chama kwa kutumia wa Zanzibar huku na yeye akimuhujumu Maalim Seif
Nipige shule hapo mkuu
Screenshot_20201023-233033.jpg
 
Poa tu ila wajue tulipofika hakuna hatua zo zote zitachukuliwa. Kuondoa picha ya Zitto kwenye karatasi ya tume Kigoma na Maalim kule Zenji sio rahisi kiivyo zaidi niombe Lissu na Maalim wapite basi. msajili labda awatimue ila Act bila hao wawili bora Cuf
 
Membe na JK ndio wenye chama kwa taarifa yako.
Dah! Kweli Maalim seifu kilaza pamoja ukongwe wake kwenye siasa ila alishindwa kujua kabisa kuwa ACT ni chama cha Membe na Kikwete kiasi hadi anajiunga na chama ambacho kumbe ni cha wana ccm.

Ila Lissu aliwahi kusema kuwa ACT sio wapinzani,Chadema na CUF tu ndio wapinzani ila watu hawakumsikiliza.
 
Ccm walitegemea cdm watampokea Membe, au kuungana na ACT yake ili wamtumie. Ila sasa hivi wanamtumia kutaka kumtoa Seif kwenye reli.
Seifu keshapewa ahadi ya cheo ana shida gani? Ikulu hauendi hivi hivi.
 
Wapumbavu kweli

Wakati watu wanaunda chama wao walikuwa wapi?

Wapuuzi wakubwa Sana watu wamekipigania chama from the scratch leo mnaleta upuuzi wenu baada ya kununuliwa na CCM.
Na baada ya mchanganyo mkali ndipo mtakapo baini kwamba kumbe hata maalim seif nae si mpinzani bali ni plan B
 
Hao wanachama wa ACT wasikilizwe na msajiri wanayo malalamiko yenye tija.
 
Kwanini wamwandikie msajili was vyama vya siasa kuwavua uanachama Zitto na Maalimu? Kwanini wasitumie kamati kuu au mkutano mkuu wa chama kuwavua uongozi walamikiwa?
 
Hata kamati inapaswa ifuate katiba!
Kamati ndiyo iliamua kuiunga mkono Chadema na siyo mwanachama mmoja mmoja.
Hao waliomwandikia msajili siyo wanachama wa ACT ,Bali ni MaCCM yenyewe.

Hao wanaojiita ndiyo wameandika hiyo barua ,wametumika tu kwa kivuli Cha CCM.
Tafute mbinu nyingine,hiyo ni yakizamani sana.
 
Back
Top Bottom