Uchaguzi 2020 Wana ACT-Wazalendo wamuandikia Barua Msajili wa Vyama vya Siasa kumwambia Maalim na Zitto wamepoteza sifa za kuwa wanachama wa ACT-Wazalendo

kwa hyo walivyoona membe ni mamluki .
Zito na maalim seif wakaamua kumuunga mkono lisu?.
vipi wanachama wengine wa act WAZALENDO wampigie kura NANI?..
unadhani kura zao mbili za maalim seif na zito zitabadilisha matokeo yoyote kwenye uchaguzi?.
VIPI IKATOKEA MEMBE AKASHINDA UCHAGUZI AKAWA RAIS?AKILI SIO PAMBO ZITUMIE KUFIKIRI
Uwez kujua waligundua nn huko ndani ya vikao vyao

Tusiwape lawama tu, au tusijione sisi wa nje tunaakili nyingi kuliko wao
 
kwa hyo walivyoona membe ni mamluki .
Zito na maalim seif wakaamua kumuunga mkono lisu?.
vipi wanachama wengine wa act WAZALENDO wampigie kura NANI?..
unadhani kura zao mbili za maalim seif na zito zitabadilisha matokeo yoyote kwenye uchaguzi?.
VIPI IKATOKEA MEMBE AKASHINDA UCHAGUZI AKAWA RAIS?AKILI SIO PAMBO ZITUMIE KUFIKIRI

Mbona maalif alishaongea vizuri kabisa
Since day one membe alishaambiwa ishu ya kumuunga mkono Lisu kama ikitokea
Na yy alikubali

IIshu nyingine Membe hafanyi kampen Hana ela wakati alidanganya wenzake kuwa ataenda kwa marafiki zake Atapewa bilion 4

Sasa ela Hana, kampen hafanyi, yuko tu na waandishi wa Habari kila siku je ww ungefanya nn kama ungekuwa ni maalim?
 
Kuelekea dakika ya 89

Hili goli limefungwa dakika imeenda ya 80
Hakuna cha goli hapo, wakitaka Z'bar iingie katika Chaos wamuengue Maalim Saif dakika hizi ndio utawajua wazanzibar walipoamkia baada ya awamu hii
 
Sasa kumuunga mkono lisu vipi wakati act wameweka mgombea wao .
Hivi Leo hii atokee kiongozi yeyote wa act WAZALENDO huko Zanzibar aseme anamuunga mkono mwinyi.
Huyo maalim atakubali?.
Mbona maalif alishaongea vizuri kabisa
Since day one membe alishaambiwa ishu ya kumuunga mkono Lisu kama ikitokea
Na yy alikubali

IIshu nyingine Membe hafanyi kampen Hana ela wakati alidanganya wenzake kuwa ataenda kwa marafiki zake Atapewa bilion 4

Sasa ela Hana, kampen hafanyi, yuko tu na waandishi wa Habari kila siku je ww ungefanya nn kama ungekuwa ni maalim?
 
21/10/2020

Msajili wa Vyama vya Siasa Tanzania,
Kivukoni, Ilala CBD, 1 Shabaani Robert Str.,
11101 Dar Es Salaam, S. L. P 63010, Tanzania.
info@orpp.go.tz

Mheshimiwa Msajili,

YAH: UKIUKWAJI WA KATIBA YA CHAMA CHA ALLIANCE FOR CHANGE AND TRANSPARENCY (ACT WAZALENDO), 2015 TOLEO LA 2020.

UKIUKWAJI WA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, 1977.

UKIUKWAJI WA KATIBA YA ZANZIBAR, 1984.

UKOSEFU WA SIFA ZA UANACHAMA KWA NDUGU MAALIM SEIF HAMAD NA NDUGU ZITTO ZUBERI KABWE.

Sisi, Crytus Adrian Kabete (Kadi Na. 1010540) na Nasma Ramadhan Assedy (Kadi Na. 1008440) ni wanachama hai wa Chama cha ACT Wazalendo. Ndugu Msajili, tunapenda kuchukua nafasi kuleta kwako taarifa rasmi kama wanachama na wapiga kura walioandikishwa kuhusu masuala ambayo kwa kiasi kikubwa ni uvunjaji na ukiukwaji wa Katiba ya Chama chetu, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Katiba ya Zanzibar, Sheria ya Vyama vya Siasa, 1992 na Sheria za Uchaguzi. tunaomba kuwasilisha taarifa hiyo kama ifuatavyo;

1.0 IBARA YA KATIBA YA ACT WAZALENDO ILIYOVUNJWA

1.1 Ibara ya 13(4)
ya Katiba ya Alliance for Change and Transparency (ACT Wazalendo) ya 2015, Toleo la 2020 inaeleza kwamba, “pamoja na sababu nyingine kama zilivyoelezwa katika katiba hii na kanuni zitakazotungwa na Halmashauri Kuu, mwanachama yeyote ambaye atasaidia, kushawishi, kujiunga, kutoa tamko la kuunga mkono chama kingine au mgombea wakati Chama kimeweka mgombea kwenye uchaguzi wowote kwa mujibu wa Sheria ya Nchi atakuwa amepoteza uanachama wa ACT”.

1.2 Kwa mujibu wa Katiba ya Alliance for Change and Transparency (ACT Wazalendo) ya 2015, Toleo la 2020 Ibara ya 13(1)(iv) mwanachama atakoma kuwa mwanachama ikiwa atapoteza sifa za uanachama kama zilivyoainishwa kwenye Katiba hiyo.

2.0 VITENDO/KAULI ZA UVUNJIFU WA KATIBA YA ACT WAZALENDO

2.1 Ndugu Msajili
, Chama cha ACT Wazalendo kupitia Mkutano Mkuu wa Taifa kilimpendekeza na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilimteua Ndugu Bernard Membe kuwa Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa sababu uamuzi wa kusimamisha mgombea wa nafasi ya Urais ni uamuzi wa msingi (core function) ya Mkutano Mkuu wa Taifa hakuna kikao au chombo kingine chochote chenye mamlaka ya KUTENGUA au KWENDA KINYUME na maamuzi hayo isipokuwa Mkutano Mkuu wa Taifa wenyewe. Mkutano Mkuu wa Taifa haukutoa azimio maalum kwamba endapo Mgombea wetu hatafanya kampeni basi viongozi wa kitaifa wamuunge mkono Mgombea wa Chama kingine.

2.2 Ndugu Msajili, kwa mujibu wa kifungu cha 6A(3) na (4) cha Sheria ya Vyama vya Siasa, 1992 kama ilivyorekebishwa na Sheria ya Marekebisho, G.N. 1 ya 2019 Mkutano Mkuu na Kamati Kuu wa/ya Chama cha siasa HAZIRUHUSIWI kukasimisha madaraka yake ya msingi (core functions) kwa chombo kingine chochote. Kifungu hicho kinasomeka hivi;

A political party general meeting and national executive committee or any similar organ shall not delegate their core functions prescribed in the party constitution

For the purpose of subsection (3), core functions means-

(a) in the case of the party national general meeting, be enactment and amendment of party constitution, election of party national chairman, deputy national chairman and nomination of presidential candidate..

2.3
Maelezo yaliyotolewa kwenye vyombo vya habari na Ndugu Maalim Seif Shariff Hamad na Ndugu Zitto Zuberi Kabwe kwamba Kamati ya Uongozi iliketi na kuamua kwamba Chama kimuunge mkono Mgombea mwingine wakati tuna mgombea wetu ni upotoshaji kwani maamuzi hayo yanapaswa kutolewa na Mkutano Mkuu wa Taifa na sio Kamati ya Uongozi au chombo kingine chochote.

2.4 Kitendo cha Ndugu Maalim Seif Shariff Hamad na Ndugu Zitto Zuberi Kabwe kutoa matamko hadharani kwamba wanamuunga mkono Ndugu Tundu Antipas Lissu ambaye ni Mgombea wa Urais kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ni ukiukwaji wa dhahiri wa Katiba ya Chama cha ACT Wazalendo.

Ushahidi wa kauli aliyotoa Ndugu Maalim Seif Shariff Hamad unapatikana:

chini ya kichwa cha habari “MAALIM AMVAA MEMBE, JPM ATOA DARASA LA USHINDI CCM”.

Pia, habari inayomwonyesha Ndugu Maalim Seif Shariff Hamad akiwa anamnadi Ndugu Tundu Antipas Lissu inapatikana:

.

Tarehe 16/10/2020 Ndugu Zitto Zuberi Kabwe alitoa na kusambaza Tamko lenye kichwa cha habari, “Nitampigia Kura Tundu Lissu ili Awe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”.

3.0 UTEUZI WA MGOMBEA URAIS KWA TIKETI YA ACT WAZALENDO
3.1 Ndugu Msajili
, mamlaka ya kumteua Mgombea wa nafasi ya Urais kwa mujibu wa Ibara ya 72(1)(f) ya Katiba ya Alliance for Change and Transparency (ACT Wazalendo) ya 2015, Toleo la 2020 ni Mkutano Mkuu wa Taifa wa Chama hicho ambao hufanyika mara moja kila baada ya miezi sitini.

3.2 Ndugu Msajili, kama ilivyoelezwa hapo juu, Chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT Wazalendo) kupitia Mkutano Mkuu wake kilimteua Ndugu Bernard Membe kuwa Mgombea wake wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Bernard Membe bado ni Mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya ACT Wazalendo. Mgombea huyu hajajitoa kwenye uchaguzi huu.

3.3 Ndugu Msajili,
vilevile Chama Cha ACT Wazalendo hakijatoa taarifa yoyote kwa Tume ya Uchaguzi kujiondoa kumpendekeza Ndugu Bernard Membe kama Mgombea. Bado Ndugu Bernard Membe amependekezwa na Chama cha ACT Wazalendo.

4.0 UKOMO WA UANACHAMA WA ACT WAZALENDO
4.1 Ndugu Msajili,
imeelezwa hapo juu kwamba kwa mujibu wa Katiba ya Alliance for Change and Transparency (ACT Wazalendo) ya 2015, Toleo la 2020 Ibara ya 13(1)(iv) mwanachama atakoma kuwa mwanachama ikiwa atapoteza sifa za uanachama kama zilivyoainishwa kwenye Katiba yetu.

4.2 Ndugu Msajili, Ibara ya 13(4) ya Katiba ya ACT Wazalendo ya 2015, Toleo la 2020 imevunjwa na Ndugu Maalim Seif Hamad na Ndugu Zitto Zuberi Kabwe kwa makusudi. Hakuna Mkutano Mkuu wa Taifa uliofanyika au uwepo wa Maazimio Maalum yaliyofanywa na Mkutano Mkuu wa Taifa uliomteua Ndugu Bernard Membe kuwa Mgombea kwamba wanachama wanaruhusiwa kukisaidia au kumsaidia, kushawishi, kujiunga, kutoa tamko la kuunga mkono chama kingine au mgombea wakati Chama kimeweka mgombea kwenye uchaguzi wowote kwa mujibu wa Sheria ya Nchi.

4.3 Ndugu Msajili,
vitendo vya Ndugu Zitto Zuberi Kabwe na Maalim Seif Hamad ni ukiukaji wa Katiba ya ACT Wazalendo na matokeo yake kwa mujibu wa Ibara ya 13(4) ya Katiba yetu ni kukoma kwa uanachama.

5.0 UTARATIBU WA USHIRIKIANO WA KISIASA (COALITION) KATI YA VYAMA VYA SIASA VILIVYOSAJILIWA.
5.1 Ndugu Msajili,
Sheria ya Vyama vya Siasa inaruhusu vyama kushirikiana kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa. Hata hivyo Ndugu Zitto Zuberi Kabwe tarehe 16/10/2020 alishutumu ofisi yako kwa kutamka maneno yafuatayo, “kutokana na uwepo wa sheria kandamizi ya Vyama vya Siasa ushirikiano wa kisheria tumeona hauna maana kwetu kama Chama kwani Msajili wa Vyama hawezi kuidhinisha jambo linalokwenda kuindoa CCM madarakani”.

5.2 Ndugu Msajili,
ni wazi kwamba ofisi yako haina mamlaka ya kuidhinisha au kutoidhinisha Mkataba wa Ushirikiano (Coalition Agreement) baina ya Vyama vya Siasa. Kwa sababu hiyo madai kwamba Msajili wa Vyama hawezi kuidhinisha jambo linalokwenda kuindoa CCM madarakani” hayakuwa na msingi wowote ila yalilenga kuhalalisha uvunjifu wa Katiba yetu ya ACT Wazalendo kama ilivyojidhihirisha.

5.3 Ndugu Msajili, maamuzi ya ushirikiano na vyama vingine vya siasa ikiwa ni pamoja na kuunganisha Chama kwa mujibu wa Katiba ya ACT Wazalendo ni moja ya maamuzi muhimu ambao lazima ufanywe na Mkutano Mkuu wa Taifa na chombo hicho hakiwezi kukasimisha madaraka hayo kwa chombo kingine bila kufuata utaratibu uliwekwa na Katiba yetu.

5.4 Ndugu Msajili, kwa mujibu wa Ibara ya 18(i) ya Katiba ya ACT Wazalendo Kamati ya Uongozi ya kila ngazi au Kamati Kuu Taifa zinaweza kukasimu baadhi ya madaraka kwa Sekretarieti yake kwa azimio la wingi wa kura za wajumbe wa kikao. Mkutano Mkuu unaweza kukasimu kwa Halmashauri Kuu baadhi ya madaraka yake, lakini kwa azimio maalumu kwa ajili hiyo. Lazima kuwe na Azimio Maalum.

6.0 MAMLAKA YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA
6.1
Kwa mujibu wa Katiba ya ACT Wazalendo mwanachama yeyote anayekiuka Katiba hiyo anaweza kufukuzwa au kupewa adhabu nyingine kama onyo au karipio. Mwanachama ambaye anakosa sifa ya uanachama kwa mujibu wa Katiba ya ACT Wazalendo uanachama wake UNAKOMA.

6.2 Ndugu Maalif Seif Shariff Hamad
na Ndugu Zitto Zuberi Kabwe wote wamekosa sifa za uanachama wa ACT Wazalendo hivyo sio wanachama wala viongozi wetu.

6.3 Ndugu Msajili, kwa mujibu wa kifungu cha 6A(2) cha Sheria ya Vyama vya Siasa, 1992 kama ilivyofanyiwa marekebisho, Vyama vyote vya Siasa vinapaswa kuongozwa na kusimamia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, Katiba ya Zanzibar, Katiba za Vyama hivyo na misingi ya Demokrasia na Utawala Bora. iliyo chini ya uangalizi wako.

6.4 Ndugu Msajili, kutokana na ukiukwaji wa wazi wa Katiba ya ACT Wazalendo na hivyo Ndugu Maalim Seif Shariff Hamad na Ndugu Zitto Zuberi Kabwe uanachama wao KUKOMA, unayo mamlaka chini sheria ya Vyama vya Siasa, 1992 vifungu vya 5(a) na 5B(1) kama msimamizi wa sheria hiyo na utekelezaji wake wa jumla. Chini ya Sheria hiyo ya Vyama vya Siasa, vifungu vya 8(C)(1) & (2), unaweza kuitisha rejesta (register) ya majina ya viongozi na wanachama wa ACT Wazalendo na kuhakikisha kwamba majina yao yameondolea kwani wamekosa sifa za uanachama.

HITIMISHO:

Ndugu Msajili,
suala la ukomo wa uanachama wa Ndugu Maalim Seif Shariff Hamad na Ndugu Zitto Zuberi Kabwe sio suala la wanachama wa ACT Wazalendo pekee. Suala hili linamhusu mtu yeyote ambae ni raia wa Tanzania na haswa mpiga kura kwani wawili hawa ni wagombea na viongozi wa juu ndani ya Chama chetu. Kitendo chao cha kukiuka Katiba yao kwa kushawishi wapiga kura kumchagua mgombea mwingine wakati Chama chetu kina Mgombea kwa mujibu wa sheria za nchi kimeleta sintofahamu ndani ya Chama kwani;

kimesababisha baadhi ya wagombea wetu kukosa kuungwa mkono kwa sababu tunaonekana hatuna msimamo,

wagombea wengi wa udiwani na ubunge ambao walijitoa kwa hali na mali na kuingia gharama kubwa kujiandaa na uchaguzi wamevunjika moyo sana kwa kauli za viongozi hao.

Kauli zao zitawasababisha baadhi ya wapiga kura wasusie kupiga kura kwa Mgombea wetu, Ndugu Bernard Membe, kwa kuamini hata shinda kwani tayari hata Chama chake hakimuungi mkono hivyo ni kuwanyima haki yao ya msingi ya kuchagua.

Chama chetu kimekuwa kikijipambanua kusimamia misingi ya utawala bora na uwazi lakini kwa kitendo ambacho kimefanywa na viongozi hawa wakuu ni wazi kabisa kwa makusudi wameamua kuachana na misingi hiyo kwa maslahi yao binafis ya kutafuta uongozi kwa njia yoyote. Hii sio demokrasia tunayoipigania na matokeo yake ni kuvuruga Chama, wanachama na viongozi kwa ujumla. Ni matarajio yetu kwamba suala hili utalipa uzito unaostahili na kulifanyia kazi kwa haraka.

Tunaomba kuwasilisha kwako,

Crytus Adrian Kabete (Kadi Na. 1010540) na
Nasma Ramadhan Assedy (Kadi Na. 1008440)

Nakala:

Mwenyekiti,
Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania (NEC),
Dodoma.

Mwenyekiti,
Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC)
Zanzibar.

Mwanasheria Mkuu, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dodoma.

Mwanasheria Mkuu, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,

Upumbavu huu. Utopolo na ujinga uliopitiliza.
 
Na Kama ishu ni kumuunga mkono lisu ilitakiwa iwe NI msimamo wa Chama Cha act WAZALENDO wote sio watu wawili..
Na isitoshe katiba yao ya ACT WAZALENDO IMESHAWABANA.
watasema nini?
Mbona maalif alishaongea vizuri kabisa
Since day one membe alishaambiwa ishu ya kumuunga mkono Lisu kama ikitokea
Na yy alikubali

IIshu nyingine Membe hafanyi kampen Hana ela wakati alidanganya wenzake kuwa ataenda kwa marafiki zake Atapewa bilion 4

Sasa ela Hana, kampen hafanyi, yuko tu na waandishi wa Habari kila siku je ww ungefanya nn kama ungekuwa ni maalim?
 
Na Kama ishu ni kumuunga mkono lisu ilitakiwa iwe NI msimamo wa Chama Cha act WAZALENDO wote sio watu wawili..
Na isitoshe katiba yao ya ACT WAZALENDO IMESHAWABANA.
watasema nini?
Umebanwa na mavi, tangu lini chama kizima kikaamuwa mambo wakati viko vyombo vimekasimiwa madaraka?

Maamuzi ya kumuunga mkono Lisu ni uamuzi wa kamati ya uongozi yeye mamlaka kwa mujibu wa katiba ya ACT.
 
Ndio maana maalim amesema kwenye kikao cha kamati kuu ya chama kilishaamua na Membe alikuwepo na alikubali

Pili msajili wa vyama Hana uwezo wa kumvua mtu uanachama wa chama chochote

Chenye kuvua uanachama ni kamati kuu ya chama, Sasa hiyo kamati kuu ya chama ambayo itamvua uanachama maalim na Zito ni ipi?
 
Sasa kumuunga mkono lisu vipi wakati act wameweka mgombea wao .
Hivi Leo hii atokee kiongozi yeyote wa act WAZALENDO huko Zanzibar aseme anamuunga mkono mwinyi.
Huyo maalim atakubali?.
Ona unavyoweweseka, Mwinyi ni kibaraka wa Tanganyika.

Chaguo ls Wazanzibar ni Maalim.
 
Membe alikubali kumuunga mkono lisu?
Ndio maana maalim amesema kwenye kikao cha kamati kuu ya chama kilishaamua na Membe alikuwepo na alikubali

Pili msajili wa vyama Hana uwezo wa kumvua mtu uanachama wa chama chochote

Chenye kuvua uanachama ni kamati kuu ya chama, Sasa hiyo kamati kuu ya chama ambayo itamvua uanachama maalim na Zito ni ipi?
 
ikifuatwa sheria na jinsi ilivoandikwa kwa usomi wa hali ya juu hao vijana wa ACT wapo sawa.katiba imekiukwa na hio ngoma hutoboi hata ukasimame korti yoyote duniani.
hao vijana wapo sahihi ukiisoma bila kuwa bayas upande wowote ule una ona kabisa viongozi waliklash katiba
 
Huyo zito mnayemtetea ataivuruga act na atawavuruga chadema.
Umebanwa na mavi, tangu lini chama kizima kikaamuwa mambo wakati viko vyombo vimekasimiwa madaraka?

Maamuzi ya kumuunga mkono Lisu ni uamuzi wa kamati ya uongozi yeye mamlaka kwa mujibu wa katiba ya ACT.
 
Yaani kipindi kama hiki kwa wale masikini wa kisiasa wasipokuwa na maisha bora basi wasubiri kufa kihoro.

Yaani chenga ni nyingi sanaa, sasa watu kama hawa wawili sijui wamekula shs ngapi do..!!
ukiwa bayas lazima useme haya.nakushauri rudi ukae usomee vipengele useme kipi kimevunjwa kipi sio sawa bayas iweke pemben
 
Ikiwa Katiba ya ACT inazungumza hivyo basi na hao wawili wanaojiita Wanachama wa ACT na wao sio Wanachama tena.

Wanapo-omba wagombea wao waondoshwe kugombea ili wagombea wa vyama vingine wapite.
Hicho hicho wanachokilalamikia na wao ndicho wanachofanya.

Unaomba wagombea wa chama chako waondoshwe ili wagombea wa vyamba vingine washinde- hii haiwezi kuwa mapenzi kwa chama chako.
 
Bora wewe unesema kweli.
Ila hwa jamaa wa chadema uwa WANAJIONA WAKO SAHIHI SABABU NI JAMBO LA UPANDE WAO.
na hicho ndo kitu kinachowaponza chadema KUJIONA WAKO SAHIHI ZAIDI KULIKO WENZAO.
mtu katiba ya ACT anaiona kuhusu mtu wa act WAZALENDO kumuunga mkono mgombea wa chama kingine.
Cha ajabu mtu anapinga
ikifuatwa sheria na jinsi ilivoandikwa kwa usomi wa hali ya juu hao vijana wa ACT wapo sawa.katiba imekiukwa na hio ngoma hutoboi hata ukasimame korti yoyote duniani.
hao vijana wapo sahihi ukiisoma bila kuwa bayas upande wowote ule una ona kabisa viongozi waliklash katiba
 
Kamati ndiyo iliamua kuiunga mkono CHADEMA na siyo mwanachama mmoja mmoja.
Hao waliomwandikia msajili siyo wanachama wa ACT ,Bali ni MaCCM yenyewe.

Hao wanaojiita ndiyo wameandika hiyo barua ,wametumika tu kwa kivuli Cha CCM.
Tafute mbinu nyingine,hiyo ni yakizamani sana.
mr mdudu yu a toking tu mach .em rudi usome vizur hio barua acha bayas.
pointi aut wap famba maana naona kila kipengele kime kotiwa kabisa
mim kama mwanasheria hio kes naikimbia sion lup holi popote
 
Hapo act WAZALENDO kinachotokea sasa hivi ni KUVURUGANA..
Chama kimebaki hakielewi kishike wapi
Ikiwa Katiba ya ACT inazungumza hivyo basi na hao wawili wanaojiita Wanachama wa ACT na wao sio Wanachama tena.

Wanapo-omba wagombea wao waondoshwe kugombea ili wagombea wa vyama vingine wapite.
Hicho hicho wanachokilalamikia na wao ndicho wanachofanya.

Unaomba wagombea wa chama chako waondoshwe ili wagombea wa vyamba vingine washinde- hii haiwezi kuwa mapenzi kwa chama chako.
 
Maalim seif hata alivyokuwa kule cafu utetezi wake wakati anavunja katiba utasikia kamati kuu ndio iliyoridhia
Kamati iliyojaa misukule yake kutokea cafu mbaka ACT wanatumia akili zile zile za cafu cafu bado awajajifunza kuheshimu KATIBA
Katiba ya Act inatamka mbaka mkutano mkuu wa wanachama ndio utoe ridhaa kwa kamati kuu ya chama
Leo Maalim seif anakwepa mkutano mkuu kwa mujibu wa katiba
Anasema kamati kuu imeshaamua na membe alikuwepo
Ndio katiba ya Act inavyosema Lah,babu asomi katiba..
 
Back
Top Bottom