Kucha kutwa sisi kazi yetu ni kupambana na wananchi wanaoibeza CCM huko mitaani na mitandaoni. Lakini miaka inaenda, mvi zinaota kichwani, nyuso zinajikunja kwa kupigwa na maisha magumu na hatuteuliwi kugombea au kupewa nyadhifa.
Ukifika wakati wa uchaguzi mkuu utasikia CCM ina wenyewe. Hapo ujue tunapigwa vijembe akina sie tusiyo na majina maarufu. Watoto wa wakubwa wanaitwa toka huko nje ya nchi wanakuja wanapewa vyeo sisi wapiga debe na wavaa ma-tshirt na kofia tupo tu.
Ewe mwana CCM mwenzangu shituka. Tunapoimba kuwa CCM ina wenyewe maana yake sisi wengine ni vibarua tu wa wenye chama chao. Kila mwaka majina ni yale yale ya wakubwa. Wengine hata kuongea hawajui lakini wamepewa ma-vyeo kwasababu tu wana damu ya wenye chama.
Sasa tuseme hapana. Tugawne mbao ikibidi.