Wana CCM kataeni UHUNI uliofanyika Dodoma

Wana CCM kataeni UHUNI uliofanyika Dodoma

Halafu kwa kumsaidia mpinzani mwenzangu ni kwmba Jiwe kipindi kile ilitoka form moja tu...hakuruhusu form zaidi ya moja maana mzee wa gusa ninuke alikuwa anataka kuchukua ashindane nae....kilichofanyika jana ni jambo lilelile ila kwa style nyingine....Hawa jamaa Wana mbinu nyingi sana kwny kufanikisha jambo lao....tutabaki kupiga mayowe humu ndani ila ndo hvyo jambo lishaisha🤣🤣🤣....
Na unapopiga mayowe kama mpinzani ili u achieve nini?WENYE Chama chao wameamua unapiga mayowe kama sio upunguani ni nini?
Ungetumia muda muda wako kuchagua kundi kwenye Chama chako ungekuwa umefanya la maana.
 
Wenye chama akina nani wewe?. Huoni kuwa kimeporwa na kipo ktk mikono ya genge dogo tu.

Hii mada haihusu walamba posho, machawa na watafuta teuzi. Inahusu wakulima na wafanyakazi wenye chama chao.
 
Kama wewe siyo mwana CCM, NINI KINAKUUMA? Nilitarajia haya yasemwe na kuamuliwa na wana CCM wenyewe
🖕🏿🖕🏿🖕🏿🖕🏿🖕🏿🖕🏿🖕🏿🖕🏿🖕🏿🖕🏿🖕🏿🖕🏿🖕🏿🖕🏿🖕🏿🖕🏿🖕🏿🖕🏿🖕🏿
 
Wenye chama akina nani wewe?. Huoni kuwa kimeporwa na kipo ktk mikono ya genge dogo tu.

Hii mada haihusu walamba posho, machawa na watafuta teuzi. Inahusu wakulima na wafanyakazi wenye chama chao.
Hao walioamua ndio wawakilishi wa hao wanachama wengine.Kimeporwa kutoka wapi?Uelewa wako wa mambo ni mdogo sana.Kwa hiyo Bunge likiamua jambo linakuwa limepora haki?Kwenye demokrasi kuna kitu kinaitwa representative democracy yaani demokrasia ya uwakilishi.Nilikuuliza swali ibara ipi ya katiba ya CCM imevunjwa?Hujajibu unabaki kulalama.
 
Wametumia mob psychology na group thinking, kushtukiza na kupenyeza ajenda yao.
SAHIHI

Ni sanaa ya utawala...

Pia ujuzi wa kucheza na 'akili za umma/kikundi cha watu'; utundu wa operesheni za kisaikolojia...

Hakuna 'halali' wala 'haramu' khasa katika 'jina la mchezo'; ila umma na mambo yake hulipa gharama ya (1) kuwa ama na (2) kutokuwa na "mwangaza" wakati mmoja hata mwingine...

Usimchukie mchezaji--chukia mchezo: "Mkate na Sarakasi"...

Ama, jiangazie nafsi yako na mulikia na wenzako kadiri ya hivi kuwa ni 'kheri'.

Chama cha Mapinduzi ni chama kwa ajili ya 'Mwangaza Bora' wa umma na 'siasa zake';

Watu wa Mwangaza katika umma wa Chama cha Mapinduzi ndiyo waamuzi...

Japo mtu yeyote mwenye kujua ilivyobora ni muamuzi vivyo hivyo.

Hmmm
 
Wahafidhina kule Zanzibar wamechanganukiwa kabisa, namba hazisomi, wanasema huu waliofanyiwa sio uhuuni ni ubasha, alisikia mhafidhina mmoja pale kisonge akisema "JK na kundi lake wametuekea kidole baina ya makalio"
 
Genge La Wahuni Wachache Ndani Ya Chama Ni Hatari Mno
Wahuni Hata CCM Wapo, Tuwakatae Popote Pale
Wahuni Wapo,
By Comrade Pole Pole
 
Kujibu mosi yako, nakubaliana na wewe kwamba ushauri hauna itikadi, LAKINI UJUWE kuukubali au kuukataa ushauri tikadi hutumika.
Kwa hiyo umetumia itikadi gani kuukataa ushauri huu? Ya CCM - Ujamaa na kujitegemea?

Mimi nasema "UJINGA" nao ni itikadi eti. Bila shaka umetumia hiyo...
Kujibu ishu yako ya pili, narudia, kama wana CCM wanakaa kimya juu ya kilichotoikea huku wakikipigia makofi, ACHA WAFU WAZIKANE.
Wana CCM wepi hao walikaa kimya? Hao 2000+ waliokuwa Dodoma wakashitukizwa na maamuzi haya..?

Yaani hii, ni kama ya Mbowe na CHADEMA. Anafuatwa na chawa 10 nyumbani kwake akasema, ooh nimeombwa na chama nigombee tena matokeo yake sasa anakula za uso..

CCM sio nyie 2000+ mliokuwa Dodoma. CCM ni mamilioni ya wanachama walio nje. SAMIA ITAKULA KWAKE, WEWE SUBIRI TU...
Unachoweza kufanya, kama taratibu zinaruhusu, KAWASHITAKI
Na mashitaka hayo yako kwa wananchi taratibu...
 
Kwenu wana CCM mnaojitambua, wenye mapenzi mema na chama na mustakbali mwema wa nchi hii.

Hicho mlichofanyiwa Dodoma ni uhuni mtupu, hakipo ndani ya kanuni, taratibu wala culture ya chama.

Inakuwaje mnakubali genge dogo la watu wachache wanakaa chemba ili waje wawastukize kwa jambo nyeti kama hilo la kupata mgombea wa nafasi za Urais wa JMT na ZNZ?.

Kwa nini mgeuke rubber stamp tu ya maamuzi ya genge dogo lililokwepa taratibu za chama zilizozoeka?

Hebu jiulizeni, huyo anayekwepa mchakato wa kawaida wa kugombea anaogopa nini, kawakosea nini wana CCM hadi aruke vikao vya maamuzi vya chama kama mwanga arukavyo kwenye ungo?.

Ndugu wana CCM, mkikubaliana na uhuni huu maanq yake mnatengeneza precedence ya UHUNI mkubwa zaidi kufanyika ndani ya chama.

Aliyewahi kuwa katibu mkuu mwenezi wa CCM bwana Polepole amewahi kusema kuwa ndani ya CCM kuna WAHUNI na bila shaka mmethibitisha wenye hili jambo kwa UHUNI usio na chembe ya haya wala aibu, kwa kuletewa mgombea kwa mlango wa nyuma bila ngazi tofauti za chama na taratibu zake kufuatwa.

Najua bado mna hyesteria ya mkutano, wengine posho zimewatia upofu, Pengine mastarehe ya muda mfupi yaendayo na mkutano bado mna hangover nayo. Lakini Jiulizeni hiki kilichofanyika ni sawasawa.

Hebu simameni sasa muanze kukataa uhuni huu wa watu wachache kupika mambo sirini halafu wanakuja kuwastukiza kama mmekamatwa ugoni vile.

Msikubali kuwa pawns au kete za kutumika tu katika hii chess ya mustakbali wa chama na nchi. Anzeni kuonyesha hisia zenu waziwazi.

Hii siyo CCM ya Nyerere, hii ni CCM ya kihuni.
Sema baba
 
Wanaoweza kukataa ni CHADEMA Tu, Vijana wa CCM pale kimewapeleka Njaa. HAKUNA mwenye uwezo wa kufanya kitu
 
Uhuni upi?Wapi kwenye ibara za Katiba ya CCM katiba hiyo imevunjwa?Unaongelea jambo usilolijua ili uonekane na wewe umechangia.Mkutano Mkuu wa CCM ndio chombo cha juu cha uamuzi.Na ndicho kilichoamua.Wewe usiyehusika na lolote kwenye uamuzi huo unapiga kelele pembeni ili iweje?
Katiba ya ccm inaeleza majukumu ya mkutano mkuu.
Kilichofanywa hakipo kikatiba wala kikanuni.
Kiufupi ni uhuni uliofanyika
 
Huku tuko vilaza na mafala tu, kama una akili ungechukua fomu kumng'oa madarakani mchaga
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Hii ishu inaweza kumuondolea Samia credibility mbele ya wananchi na CCM yenyewe, maana imekaa kama anataka uongozi bila merits bali kwa "kuwezeshwa" huku taratibu xa chama zikinajisiwa.

Magufuli na ubandidu wake wote wa kisiasa hakuthubutu kufanya hivi kwenye uchaguzi wa 2020 Japo alikuwa na uwexo wa kufanya hivyo.

Hii move Itabackfire!

Hehe bananchi bataongea maneno yote safari hii..........watu walifuraahii jamaa alivyoondoka wakajua kazi imeisha....ila kwa sasa ndo kama mambo yanaanza ........mama Abdul kajifunza na hafanyi makosa safari hii
 
Katiba ya ccm inaeleza majukumu ya mkutano mkuu.
Kilichofanywa hakipo kikatiba wala kikanuni.
Kiufupi ni uhuni uliofanyika
Elezea ibara iliyovunjwa kikatiba au kikanuni.Unaijua katiba ya CCM ya mwaka 1977?
Majukumu ya Mkutano Mkuu ni yapi?Wacha kuzungumzia usichokijua.
 
Back
Top Bottom