baz kaiza
JF-Expert Member
- Jan 27, 2015
- 14,971
- 18,641
Suala la kutokunekana kwa aliyekua makamu wa Rais Emanuel Nchimbi na wana CCM kua kimya limefanya tuonekane kama mazuzu kwamba CCM ya watu wasiopungua watu 100 tuliobaki wote ni takataka ndani ya CCM chama chenye wanachama milioni 15 kinashindwa kushinikiza hawa watu 100 wa mwachilie Emanuel Nchimbi. CCM ya sasa imejaza machawa unakuta mtu mzima miaka 60 lakini ni chawa wa Mwenyekiti wa chama kutwa kucha ni kujikomba tu kwa Mwenyekiti hakuna mtu wa kutoka na kuhoji Huyu aliekua makamu wa Rais yuko wapi ? Wana CCM wote kimya kama mazuzu au kuku wa kisasa. Polepole alipotea kwenye mazingira ya kutatanisha mtu aliekua Balozi kabisa na katibu mwenezi wa chama lakini CCM tunashindwa kutoka kwa nguvu moja na kudai Polepole sasa Balozi Emanuel Nchimbi yuko kizuizini lakini wana CCM tulivyo mazuzu tumeshindwa kutoka kwa umoja na kudai Emanuel Nchimbi hiii ni CCM ya aina gani? Kama makamu wa Rais anaweza kupotea kwenye mazingira ya kutatanisha na Wana CCM tukawa kimya kuna haja gani ya kua mwana CCM ambae misingi ya CCM ni kusema ukweli daima.
