Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 1,096
- 4,948
Kuna majadiliano na mawasiliano yanafanyika kuhusu utaratibu mzuri wa waliokuwa wanasiasa ndani ya chama cha CHADEMA wakalazimishwa na JPM wahamie CCM wanajipanga kurejea CHADEMA.
Mkakati huu unaratibiwa vyema na viongozi wa juu wa Chadema ikiwa ni maandalizi ya uchaguzi mkuu 2025.
Wakati huo huo akina halima Mdee tayari wameandika barua yakuomba radhi kwa chama chao na wanatarajiwa kuwasilisha barua hiyo rasmi makao Makuu ya Chadema.
Katika mikakati iliyopo sasa na inayoshukiwa na baadhi wa Makada wa CCM ambao wanaamini watakatwa majina yao 2025 ni kwamba endapo watakatwa basi hawatakaa staafu siasa bali wataingia upande wa pili kupigania haki zao.
Moja ya mbinu inayokusudiwa kutumika nikuhakikisha kwamba wagombea wote watakaoteuliwa bila sifa ndani ya CCM wanapata wapinzani wakubwa na wenye nguvu kwa wapiga kura kama ambavyo uchaguzi wa mwaka 2010 na 2015 ilifanyika.
Wakati huo pia Gwiji la siasa Mzee Slaa amepanga kufanya mazungumzo na hasimu wake kifikra Mhe. Lisu katika kile ambacho kinaelezwa kuendelea kunogesha mapambano ya haki ndani ya nchi.
Je, CCM itakubali kuona wanasiasa waliolazimishwa kuhama vyama wanakabidhi ofisi na magari nakurejea kwenye harakati za ukombozi?