AmKATRINA
JF-Expert Member
- Jul 27, 2012
- 882
- 2,044
Jamani, Jamani
Wapendwa wa humu narudia tena, Chana au haribu kabisa tiketi au karatasi yoyote yenye taarifa zako sahihi kwa usalama wako.
Niko hapa Police Kimara, rafiki yangu wa kiume amekamatwa na kuwekwa ndani baada ya tiketi yake ya ki-electronic ya basi moja kutoka Arusha kuja Dar kukutwa kwenye tukio la uhalifu Kimara Bucha.
Yeye rafiki yangu anasema baada ya kushuka Mbezi Magufuli stendi, aliamua kuikunja na kuitupa tiketi yake karibu na lango la kutokea na baada ya hapo akaendelea na safari ya kuelekea kwake Tegeta.
Anasema zilipita siku 2 akapigiwa simu na police kuwa anahitajika kituoni Kimara.
Anasema hakwenda kwa kuhofia huenda ni watu wasio wema kisha akazima simu.
Anasema kesho yake anashangaa kuona police wako nyumbani kwake na wakamuweka chini ya ulinzi kwa kosa la uhalifu uliotokea maeneo ya Kimara bucha.
Na anasema walihisi walimpata kupitia Facebook, (mutual friend mmoja akatafutwa kisha akawaelekeza kwake).
Rafiki yangu si mtu wa kujichanganya sana na watu. Iwe usiku au mchana, akiwa ndani hujui na wala akienda kibaruani hujui.
Anasema ahusiki na tukio na wala hajafanya uhalifu wala kuwa na rekodi yoyote ya uhalifu.
Hapa tunashindwa cha kufanya.
Hatujui kama kweli kahusika au lah!
Sisi tunajua ahusiki ila binadamu hubadilika.
Ila maadam iko mikononi mwa jeshi la polisi tutajua tu hatma yake na wahusika halisi
Chana au haribu kabisa karatasi/tiketi ya basi/meli/treni/ndege/CV/copy yako ya NIDA na nyinginezo zenye taarifa zako sahihi ili kuepuka kupata matatizo.