Naamini serikali wana lengo zuri la kuhakikisha kuwa maadili mazuri yanafuatwa na Watanzania mahali popote walipo. Kama ujumbe huo ni wa kweli (na assume hivyo) basi ninaomba serikali yetu katika kutusaidia kutekeleza ujumbe wao huo.
a. Watangaze kwenye magazeti ya serikali, redioni, TV n.k kuwa matusi yamepigwa marufuku na Mtanzania yeyote awe chumbani kwake, kijiweni, sokoni, n.k haruhusiwi kusema neno lolote la matusi na watutangazie adhabu itakayowapata watakaokiuka.
b. Pia itakuwa vizuri watuwekee maneno ya matusi ambayo yanapigwa marufuku kusikika au kutumika pamoja na vitendo. Uhuru wa maneno ni mkubwa zaidi kuliko uhuru wa vitendo. Hivyo wakituorodheshea matusi na madaraja ya matusi (kama first class, second class, nk) tutajua ni maneno gani tunaweza kuyatumia. Hivyo watatusaidia kujua kama fuska, mjinga, mzembe, fisadi n.k ni matusi ya daraja gani?
c. Wakishatoa hiyo definition tunaomba waongeze maafisa usalama wa maadili (Moral Police) ili washinde mitaani na kwenye mtandao kutafuta nani amesema nini na kuchukua hatua mara moja.
d. Wakimaliza kwenye maneno ninawashauri waanze kuangalia mavazi ya Watanzania ili tujue watanzania wanatakiwa kuvaa nguo za namna gani kama alivyojaribu Bi. Hawa Ghasia. Kwa sababu baadhi ya nguo zinachochea mawazo ya matusi, naamini itakuwa vizuri kama serikali itatangaza nguo za namna gani zivaliwe na Watanzania. Nashauri vazi la kanzu, gagulo na kaniki yawe ni mavazi ya lazima kwa Watanzania!
e. Wakimaliza hayo ninawashauri waje na utaratibu wa kuhakikisha kuwa watu hawachukuliani mademu au wanaume. Hii itapunguza maneno mengi ya mtaani ambayo huchochea maneno ya matusi. Utaratibu huo unaweza kuhusisha teknolojia ya kisasa ya mawasiliano ambapo kama Mbunge mmoja wa CCM alivyowahi kupendekeza wale wote wanaochukua wake/waume za watu wawekwe alama. Napendekeza wavae ribbon za aina fulani hivi. Za rangi ya zambarau ni nzuri zaidi.
f. Kwa vile maafisa wengi wa serikali na utumishi wa umma wanatumia muda mrefu kutumia email za matusi na picha za ngono (ushahidi upo) na vichekesho ambavyo wakati mwingine vinapakana na vya "kighaidi" napendekeza serikali iweke nembo kwenye compyuta zote za serikali ili wale wanaoependa kuangalia picha za ngono kompyuta zao zigome na waendelee na kazi.
g. Kwa vile ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka ni tatizo dogo nchini, napendekeza watawala wetu waendelee na kuhangaika na Jambo Forums na wapange vikao vya jinsi gani ya kuishughulikia huku wezi wa fedha za umma na wanaotumia mabaya madaraka yao wakiendelea kutanua. Kwa vile JF ndio tatizo kubwa kabisa linaloikabili nchi yetu sasa hivi, napendekeza "task force" mpya iundwe na Waziri Mkuu (wanaweza kumuomba Mhe. Lowassa kwa ushauri wa jinsi ya kufanya hivyo) ili iweze kushughulia dharura hii ya Jambo Forums.
Wakishafanya hivyo, mimi nawaunga mkono kwa ushauri wao huo wa bure!!