Wana kigoma wamenambia Kama sina hela wala connection nimiliki uchawi nipate heshima

Wana kigoma wamenambia Kama sina hela wala connection nimiliki uchawi nipate heshima

Prakatatumba abaabaabaa

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2022
Posts
1,842
Reaction score
6,087
Huu msemo nineukuta kigoma hapa maeneno ya ujiji, nilienda kutembelea njia za watumwa, Livingstone n.k nimeambiwa story ya mzee mmoja aliekuaa anaitwa juma njemba huyu jamaa nasikia alikua noma gwijii, akikwambia leo jioni haifiki ujue umeenda hivyo wala hakuna mjadala, lakini alikua hakupi adhabu bila kujiridhisha,

Dunia tunayoishi imejaa ujinga mwingi, utapeli,wizi na mambo mengi yanayokera, ukisema utumie njia ya amani mzunguko wake ni mrefu ukisema utumie mapanga kama wenzangu wakurya basi gereza ina kuhusu, nadhani hii njia ya uchawi ndio nzuri, nimeona huko daresalam malalamiko ni mengi mtu anakuuzia kiwanja ambacho kimeshauzwa (anakutapeli) sasa kwanini mtu kama huyu usimroge akavimba mbupu?..polisi wenyewe ndio hivyo hao ndio wanaongoza kwa utapeli, wakijua unamiliki pesa wako tayari kukuua na kukupoteza rejea walivyomuua yule muuza madini kule Mtwara, mpaka leo kesi inazunguka tu, fikiria yule kijana wa Arusha alivyovunjwa mfupa wa ugoko kituoni, kwanini sasa usimroge?

Bado niko kwenye utafiti wakujua madhara yake ni yapi?..... Soon namimi naenda kua gwiji.
 
Back
Top Bottom